Pendekezo: Ili kutatua migogoro CHADEMA, wanaokosea wasifukuzwe!

mwemanga

Senior Member
Oct 22, 2012
120
195
Fukuza Fukuza viongozi na wanachama ktk chadema sio ufumbuzi wa kutatua matatizo ya migogoro ndani ya chama.

Mimi sikubaliani na kitendo cha kuwafukuza wanachama au kuwavua uongozi wale wote wanao onekana kwa jamii ya chadema kuwa ni sehemu ya tatizo.

Nina sababu kuu mbili

1. Ninaamini kuwa wengiwao huwa wana fanya makosa kwa sababu ya kutojuwa utaratibu, sababu wengi wa viongozi ni wachanga kisiasa pia hawajui vema maadili ya uongozi sasa jukumu la kuwafundisha utaratibu wa uongozi ni la chama taifa kwa kupeleka utaratibu wa mafunzo kwa viongozi na wanachama.

2. Viongozi wengi na madiwani wengi wamejiunga chadema baada ya kukatwa na ccm katka kura za maoni za vyama walivyo toka sasa tukawapokea bila kuwapa mafunzo yeyote tukawa simamisha kugombea baada kuwa madiwani au viongozi hatukuwasomesha ukada wala kujua miiko ya uongozi au uwakirishi sasa wanapo kosea BAKORA YA KUWAADHIBU ISIWE KUFUKUZA.

Kufukuza hakuondowi tatizo bali kuna tengeneza maadui pia sio njia mzuri kufukuzana hivyo viongozi watumie njia nyingine
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,742
2,000

Hayo mawazo yako sio sahihi, CCM wamefika hapo walipo kwa sababu ya kulea maovu wapo waliokisaliti chama cha CCM na Serikali ya CCM lakini hadi sasa wapo na ndo sababu iliyofanywa chama kuchukiwa na wananchi, Kwa upande wa CDM hiki wanachokifanya sasa ni sahihi kabisa kwani kama kweli kiongozi ndani ya CDM anamapenzi mema na chama pamoja na juhudi za ukombozi wa Taifa ili hatafanya makosa kwani kuenguliwa katika kundi ni pigo kwako na jamii inayokuzunguka.
 
tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,516
1,195
Maoni yako ni mazuri, ila kabla ya kuyatoa pata nafasi ya kuongea na mchange na mwampamba, BAN iko nje nje!
 
Chaimaharage

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
211
0
CDM msifanye kosa walilofanya CCM la kulea maovu eti kuvumiliana. Chama kinaongozwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kila mfuasi na kiongozi hana budi kuzifuata. Sasa mtu anapo fanya maksudi wakati anajua hayo halafu asamehewe hayo ndiyo yanayo igharimu CCM sasa. Mtu asipo fuata kanuni na sheria fukuza..hakuna haja ya kubaki na kundi kubwa lisilokuwa na tija. Mfano katibu wa Bavicha Mwanza yote hayo aliyajua, lakini kwa sababu zake na hao waliomtuma kafanya maksudi, fukuzilia mbali uchafu.

Ndani ya CDM tunajua mamluki wamo wengi na wanatakiwa hadi 2014 mwishoni wawe wamemaliza kazi waliyo tumwa. Kama hamuamini subirini itakapo fika 2014 utaona wengi wanajitoa eti "tunarudi kundini" magambani. Watakao ona upepo wa magamba kuchukua nchi tena siyo mzuri watajifanya kukomaa bila kutoka ili kusikilizia joto. Lakini wengi kwa kuwa wanakula posho za kufanya kazi waliyopewa itabidi watoke tu kwa aibu.

Ukiona mtu pamoja na hali ya maisha tuliyonayo anashabikia magamba basi kama hafaidiki nayo basi ana mtindio wa akili. Mfano mtu ana nyumba ya nyasi lakini nje ametundika bendera ya CCM. Wakati wengine wanamwambia "tuchague tutakupunguzia gharama za vifaa vya ujenzi ili ujenge nyumba bora" yeye aliweka pamba masikioni na ndiyo hali inayo mkuta baada ya maamuzi mabovu, lakini ajabu mtu huyo huyo bado ameweka bendera ya CCM mbele ya nyumba, mtu huyo kweli utasema ana akili timamu?
 
NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,748
2,000
Tatizo halikuwahi kukabiliwa kwa a) kusubiri litakwisha. b) kukwepa. c) kumwachia mwingine aje kulimaliza nk. Kuwajibika ndiko huku. Unayedhani katenda kosa kwa kutojua itajulikana baada ya maelezo. Wengine wanatenda kwa makusudi au kwa kuwa hawakupata wanachotarajia kimaslahi. Hata huku CHADEMA wako waroho wa madaraka, mafisani, wabadhirifu na wezi kama walivyo vyama vingine.

Tofauti ya CHADEMA na wengine ni kuwajibishana kwa makosa!! Na hili ndilo ambalo hutasikia CCM akisema ni baya. Chini chini wanafurahi kwa sababu watu wakifukuzwa CHADEMA wanarejea CCM. Kwa CCM hili ni swala la kuwa na wanachama wengi, watalifurahia.
 
Havizya

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
433
2,000
Mwemanga, elewa ukimwacha kiroboto kwenye kidole aendelee kukung'ata, mwishowe funza kisha mguu kukatwa! Hakuna asiyeitambua dhambi bwana. They have to be sacked off immediately
 
Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,210
2,000
yawezekana ulikuwa na hoja nzuri ila namna ya kuiwasilisha ndio tatizo. Mtu kutoka ccm kuja cdm sio kigezo cha kuharibu na kusamehewa. Kama hakuja kwa mapenzi yake ataondoka bila mapenzi yake. Kadhalika wapo ambao hawakuwahi kuwa wanachama wa chama kingine zaidi ya cdm na bado wanasumbua
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,589
2,000
Fukuza Fukuza viongozi na wanachama ktk chadema sio ufumbuzi wa kutatua matatizo ya migogoro ndani ya chama.

Mimi sikubaliani na kitendo cha kuwafukuza wanachama au kuwavua uongozi wale wote wanao onekana kwa jamii ya chadema kuwa ni sehemu ya tatizo.

Nina sababu kuu mbili

1. Ninaamini kuwa wengiwao huwa wana fanya makosa kwa sababu ya kutojuwa utaratibu, sababu wengi wa viongozi ni wachanga kisiasa pia hawajui vema maadili ya uongozi sasa jukumu la kuwafundisha utaratibu wa uongozi ni la chama taifa kwa kupeleka utaratibu wa mafunzo kwa viongozi na wanachama.

2. Viongozi wengi na madiwani wengi wamejiunga chadema baada ya kukatwa na ccm katka kura za maoni za vyama walivyo toka sasa tukawapokea bila kuwapa mafunzo yeyote tukawa simamisha kugombea baada kuwa madiwani au viongozi hatukuwasomesha ukada wala kujua miiko ya uongozi au uwakirishi sasa wanapo kosea BAKORA YA KUWAADHIBU ISIWE KUFUKUZA.

Kufukuza hakuondowi tatizo bali kuna tengeneza maadui pia sio njia mzuri kufukuzana hivyo viongozi watumie njia nyingine

Unaonekana kama kuna watu umewapandikiza chamani kwa malengo ya uharibifu, wasifukuzwe ili uwe unawabadilishia majukumu kila majira upendavyo.
 
meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,333
2,000
kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa zitto hajui taratibu za chama?
mtu anayeunda kikosi cha kuchafua chama chake...????nimekasirika sana.....kweli mchawi ni mtu wa ajabu sana!
 
Wingu

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,320
1,225
Mtu Kama Ben Saanane sio wa kumwacha nenda fungua Thread ya kujisifia ametumia ID mbili mpaka aibu
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,382
2,000
Suluhisho siyo kufukuzana bali ni kuambiana ukweli tu.Na ukweli ndio utakaoijenga Tanzania yetu.
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
2,000
Kuwa kiongozi wa kisiasa ni kuchukua jukumu la kusimamia ustawi wa jamii katika namna pana sana, mtu wa namna hiyo hategemewi kwenda kinyume na taratibu za chama chake kwa namna yoyote ile ama sivyo wananchi hawawezi kuwa na imani ya uwezo wa uongozi wa mtu huyo.

Chadema wako sahihi kabisa wanapowatimua watu wa namna hiyo, hata mti ili ustawi inalazimika kukata baadhi ya mashina hasa kama yanakua kuelekea eneo lisilo stahili, hivyo Chadema endelezeni katakata bila woga wowote ule.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom