PENDEKEZO: Hotuba ya MEI MOSI 2017 ijibu maswali yafuatayo:

Statistics

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
3,594
7,587
Heri ya Pasaka.

Naomba atakayekuwa kiongozi wa heshima, atakayewakilisha serikali katika siku ya 01-05-2017 BK, jumatatu, katika hotuba yake ajibu maswali yafuatayo:-

1.a) Lini serikali italipa nyongeza ya mshahara uliopaswa kuongezwa July 1, 2016?

b) je, tarehe 01-07-2017 kuna nyongeza?

2. Lini uhamisho wa wafanyakazi hasa walioko Mamlaka ya serikali za Mitaa waliokamilisha taratibu za uhamisho hadi June 2016 watapewa au watanyimwa kibali cha kuhamia walikoomba au watakakopangiwa?

3. Ni lini madai ya wafanyakazi yatalipwa?

4. Kwanini nafasi za kazi za wakuu wa idara na vitengo katika wizara, idara, mikoani na wizarani hazitangazwi hadharani ili wenye sifa waombe?

5. Kwa nini kima cha chini hakijawa TSh. 940,000/= kwa mwezi.

Nakutakia maandalizi mema ya hotuba, na kila jema katika utumishi wako uliotukuka.

Tanzania ni kubwa kuliko masilahi yetu.

Yesu amefufuka, Amina.
 
Jamani hii hoja msiikebehi imebeba uhai wa watu.
Si watumishi tu na mzunguko wa fedha mtaani,maana mtumishi akilipwa na Mangi anauza dukani,baa mad atauza create 20, vijijini watatumiwa matumizi nk
 
Kima cha chini kikiwa 940,000,itabidi ukaajiriwe chato,hii ya sasa yenyewe watu wanapunguza wafanyakazi,hiyo ikifika nadhani mwajiri atakuwa serikali pekee.
 
Mnapanga muongezewe mishahara kwa tija gani ya uzalishaji mnayoifanya?
Mbona hamuwaongelei wakulima na wafugaji wanaojinunulia madawa ya kilimo na mifugo?
Ninyi kila mwaka mnataka mfurahishwe tu bila kuangalia tija gani mmelifanyia taifa hili zaidi kila mwaka kustahili ongezeko?
Haujui mshahara ukipanda hata kodi yako itapanda kwa proportion ile ile?
Ni lini utamsemea mtu me
Mwingine katika sekta nyingine? Ulimaanisha mfanyakaz yupi anaefanya kazi aanzie 900 elfu?
 
kama madai yenu ni hayo siji kwenye sherehe,nitazitoa wapi wakt najnga flyova,chato eapot na kutafuta vyet vya bashite,mnivumilie
 
Mnapanga muongezewe mishahara kwa tija gani ya uzalishaji mnayoifanya?
Mbona hamuwaongelei wakulima na wafugaji wanaojinunulia madawa ya kilimo na mifugo?
Ninyi kila mwaka mnataka mfurahishwe tu bila kuangalia tija gani mmelifanyia taifa hili zaidi kila mwaka kustahili ongezeko?
Haujui mshahara ukipanda hata kodi yako itapanda kwa proportion ile ile?
Ni lini utamsemea mtu me
Mwingine katika sekta nyingine? Ulimaanisha mfanyakaz yupi anaefanya kazi aanzie 900 elfu?
Unajua barua za ajira zinavyosomeka kwa waajiriwa wa serikali?
 
Back
Top Bottom