Pendekezo Fyatu: Upinzani Ususie Mijadala ya Sheria za Dharura

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,546
40,187
bunge1.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna msemo kuwa "you messed it up, you clean it up!" Yaani, kama umechafua, usafishe mwenyewe. Matatizo yote katika sekta ya madini na nishati, na matatizo mengine yote yanayotokana na hayo - kuanzia sera, sheria, kanuni na mikataba mbalimbali ni matokeo ya utawala wa CCM. Ni matokeo ya sera, uongozi na maono yake kwa taifa. Hili halina mjadala wala ubishi.

Sasa kama serikali ya CCM imeona imevurunda kwenye maeneo hayo na kuwa sasa inataka kusafisha iachwe tuone kama itasafisha kweli. Wapinzani wasitumiwe na wala wasikubali kutumika kama fagio la kufagilia uchafu wa CCM. Miaka mingi nyume watu wa CCM walipoona hawawezi kusema wazi machafu ya uongozi na utawala wao waliyapenyesha kwa viongozi wa upinzani. Lakini kila ukifika wakati viongozi wa upinzani wanakiona cha moto, hakuna kiongozi wa CCM anayesimama nao, hadi watakapoamua kujitoa CCM!

Sasa kwanini upinzani ulalamikie "hati za dharura"? Kwanini upinzani uonekane kutaka kufanya kile ambacho wananchi waliichagua CCM kufanya? Bunge lina wabunge wengi wa CCM na serikali inaongozwa na serikali ya CCM chini ya Mwenyekiti Magufuli. Na tumeshaona kuwa Magufuli ameonesha nia ya kusafisha safisha. Sakata la makanikia ni mfano wa karibu zaidi na mingine ipo mingi.

Sasa, kwanini wapinzani walalamikie, kwanini CCM wasome miswada hii na kuikosoa kwa kina ili wawasaidie CCM? Niliandika miaka mingi nyuma kuwa "siyo jukumu la upinzani kuisaidia CCM kutawala". (SOMA HAPA MAKALA YANGU YA JF 2011) Hakuna chama cha upinzani ambacho hakiko kwenye serikali ya umoja kinachotakiwa kusaidia chama kilicho madarakani kutawala!

Hivyo, kwa vile serikali ya CCM imeamua kuleta tena miswada ya dharura ya mabadiliko ya sheria mbalimbali, kwa vile wameamua kufanya hivyo bila kuanzisha mjadala wa ndani wa kisera ndani ya chama chao, na kwa vile wameamua kufanya hivyo bila kukusanya maoni mbalimbali ya wazi kwa wadau mbalimbali wa taifa letu, na wameamua kufanya hivyo wakijua kabisa kuwa maeneo haya yana unyeti na umuhimu mkubwa kwa maslahi ya taifa, uchumi na uwekezaji, basi ni jukumu lao kujadili na kutoa maoni wao PEKE YAO ili wao peke yao wabebe lawama au pongezi kwa matokeo ya matendo yao hayo.

Hivyo, vyama vya upinzani Bungen na nje ya Bunge VIACHE kukosoa kabisa maamuzi haya ya CCM, wasitoe mawazo yoyote ya kuonesha makosa, wala wasitoe maoni yoyote ya kuboresha miswada hii. Utakapokuja mjadala Bungeni wapinzani wakae kimya (hawahitaji kutoka Bungeni). Hawahitaji kuomba mwongozo wowote kwa Spika, hawana haja ya kupingana na "kiti" kwa wakati wowote. Wao siku ya mjadala itakapofika wawe watazamani wa maamuzi na utekelezaji wa uongozi wa CCM.

Kama CCM wameamua kushika makali na mpini wa kisu, waachwe wenyewe wajikate. Tatizo la sera zetu mbalimbali na matokeo ya sera hizo ni maamuzi ya CCM. Sasa, they messed it up, let them clean it up or pay up!

Utakapofika uchaguzi mwingine. Upinzani usijitahidi kuwa sehemu ya najisi.

Pendekezo hili ni fyatu; lakini siyo fyatu kivile.
 
Usemalo ni kweli kuiba waibe wao leo hii wanakuja kusema wanaibiwa,nimewaza kwa akili ya lusinde na kushangaa tunaibiwa na nani kudavadua nakuta wezi ndio haohao wanaosema wanaibiwa....wapinzani wawaachie huo muswada mana ndio wahusika wakusign then wanakata mauno bungeni
 
Mimi naunga mkono wapinzani wakae kimya bungeni kwenye hiyo miswada wasichangie chochote kile wawaache maccm yaamue yenyewe.
Na akili zao (ccm) zilivyofupi wataacha kujadili hiyo miswada na kuanza kujadili wapinzani
 
bunge1.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Kuna msemo kuwa "you messed it up, you clean it up!" Yaani, kama umechafua, usafishe mwenyewe. Matatizo yote katika sekta ya madini na nishati, na matatizo mengine yote yanayotokana na hayo - kuanzia sera, sheria, kanuni na mikataba mbalimbali ni matokeo ya utawala wa CCM. Ni matokeo ya sera, uongozi na maono yake kwa taifa. Hili halina mjadala wala ubishi.

Sasa kama serikali ya CCM imeona imevurunda kwenye maeneo hayo na kuwa sasa inataka kusafisha iachwe tuone kama itasafisha kweli. Wapinzani wasitumiwe na wala wasikubali kutumika kama fagio la kufagilia uchafu wa CCM. Miaka mingi nyume watu wa CCM walipoona hawawezi kusema wazi machafu ya uongozi na utawala wao waliyapenyesha kwa viongozi wa upinzani. Lakini kila ukifika wakati viongozi wa upinzani wanakiona cha moto, hakuna kiongozi wa CCM anayesimama nao, hadi watakapoamua kujitoa CCM!

Sasa kwanini upinzani ulalamikie "hati za dharura"? Kwanini upinzani uonekane kutaka kufanya kile ambacho wananchi waliichagua CCM kufanya? Bunge lina wabunge wengi wa CCM na serikali inaongozwa na serikali ya CCM chini ya Mwenyekiti Magufuli. Na tumeshaona kuwa Magufuli ameonesha nia ya kusafisha safisha. Sakata la makanikia ni mfano wa karibu zaidi na mingine ipo mingi.

Sasa, kwanini wapinzani walalamikie, kwanini CCM wasome miswada hii na kuikosoa kwa kina ili wawasaidie CCM? Niliandika miaka mingi nyuma kuwa "siyo jukumu la upinzani kuisaidia CCM kutawala". (SOMA HAPA MAKALA YANGU YA JF 2011) Hakuna chama cha upinzani ambacho hakiko kwenye serikali ya umoja kinachotakiwa kusaidia chama kilicho madarakani kutawala!

Hivyo, kwa vile serikali ya CCM imeamua kuleta tena miswada ya dharura ya mabadiliko ya sheria mbalimbali, kwa vile wameamua kufanya hivyo bila kuanzisha mjadala wa ndani wa kisera ndani ya chama chao, na kwa vile wameamua kufanya hivyo bila kukusanya maoni mbalimbali ya wazi kwa wadau mbalimbali wa taifa letu, na wameamua kufanya hivyo wakijua kabisa kuwa maeneo haya yana unyeti na umuhimu mkubwa kwa maslahi ya taifa, uchumi na uwekezaji, basi ni jukumu lao kujadili na kutoa maoni wao PEKE YAO ili wao peke yao wabebe lawama au pongezi kwa matokeo ya matendo yao hayo.

Hivyo, vyama vya upinzani Bungen na nje ya Bunge VIACHE kukosoa kabisa maamuzi haya ya CCM, wasitoe mawazo yoyote ya kuonesha makosa, wala wasitoe maoni yoyote ya kuboresha miswada hii. Utakapokuja mjadala Bungeni wapinzani wakae kimya (hawahitaji kutoka Bungeni). Hawahitaji kuomba mwongozo wowote kwa Spika, hawana haja ya kupingana na "kiti" kwa wakati wowote. Wao siku ya mjadala itakapofika wawe watazamani wa maamuzi na utekelezaji wa uongozi wa CCM.

Kama CCM wameamua kushika makali na mpini wa kisu, waachwe wenyewe wajikate. Tatizo la sera zetu mbalimbali na matokeo ya sera hizo ni maamuzi ya CCM. Sasa, they messed it up, let them clean it up or pay up!

Utakapofika uchaguzi mwingine. Upinzani usijitahidi kuwa sehemu ya najisi.

Pendekezo hili ni fyatu; lakini siyo fyatu kivile.
Ni sawa unasema wapinzani hata bajeti wasiwe wanachangia maana wanaisaidia serikali y ccm!Akili yako imechuja,jitafakari!
 
'Upinzani' wa Tanzania ni upinzani wa ajabu sana.

Kiuhalisia hao wapinzani si wapinzani.

Kiuhalisia ni washauri wa CCM.

Ukiwafuatilia kwa makini utagundua kuwa mara nyingi huwa wanaishauri CCM jinsi ya kuendesha na kufanya mambo.

Mimi kamwe siwezi kumpa ushauri mpinzani wangu.

Nitamwacha akosee na aharibu ili azidi kuniongezea fimbo za kumchapia.

Hawa hawa wapinzani ndo walioaminisha Watanzania kuwa Lowassa ni fisadi....hadi CCM wenyewe wakaamini na kuamua kumtema halafu eti hao waliotuaminisha kuwa jamaa ni fisadi ndo wakamchukua na kuanza kutuaminisha kuwa yeye siyo fisadi.

Hakuna upinzani Tanzania. Waliopo ni washauri na wasindikizaji wa CCM.
 
Mzee Mwanakijiji hapo umetega ndoano!! Ikiwa wapinzani watapenda kufa kifo chema basi wafuate ushauri wako huu fyatu!! Ni lini hao ccm wamewahi kuhukuMIKA kwa hayo. Yote waliyosababisha ambayo wewe mwenyewe umeyaainisha? Kwanza nani wa kuwahukumu? Kwa Nguvu ipi? Mambo yatakapoharibika kwa maamuzi ya hao ccm watu wataonaje effect ya wapinzani? Yaani nini itakuwa faida ya uwepo wa wapinzani? Hebu acha fiksi!! Bora angalau waseme "Tulisema" kuliko kutosema kabisa! Nguvu kidogo waliyonayo wapinzani leo imetokana na kusema hizo mess za ccm tu!! Hawajawahi kupewa nafasi ya ku apply fikra zao kwenye uhalisia! Kwa hali ya siasa ya Nchi zetu hizi Mpinzani kazi yake ni upinzani!! Usipofanya hivyo ni bora usiwepo kabisa.
 
'Upinzani' wa Tanzania ni upinzani wa ajabu sana.

Kiuhalisia hao wapinzani si wapinzani.

Kiuhalisia ni washauri wa CCM.

Ukiwafuatilia kwa makini utagundua kuwa mara nyingi huwa wanaishauri CCM jinsi ya kuendesha na kufanya mambo.

Mimi kamwe siwezi kumpa ushauri mpinzani wangu.

Nitamwacha akosee na aharibu ili azidi kuniongezea fimbo za kumchapia.

Hawa hawa wapinzani ndo walioaminisha Watanzania kuwa Lowassa ni fisadi....hadi CCM wenyewe wakaamini na kuamua kumtema halafu eti hao waliotuaminisha kuwa jamaa ni fisadi ndo wakamchukua na kuanza kutuaminisha kuwa yeye siyo fisadi.

Hakuna upinzani Tanzania. Waliopo ni washauri na wasindikizaji wa CCM.
We Ni bure tu! Tulia
 
Unauongelea huu upinzani ambao CHADEMA hata katiba yao haina ukomo wa madaraka?

Unauongelea huu upinzani ambao Maalim Seif na Lipumba ndio wafalme wa Ukatibu Mkuu na Uenyekiti?

Unauongelea huu Upinzani waliomtangaza Lowasa ni fisadi pale mwembe Yanga leo ndio mkombozi wa watanzania?

Unauongelea huu upinzani ambao Zitto alitaka kugombea uenyekiti akaitwa Msaliti?

Unauongelea huu upinzani ambao rais Magufuri akisimamisha kazi wabadhilifu wanasema anasimamisha bila kufuata tararatibu?

Unauongelea huu upinzani ambao baada ya rais kuunda tume kuchunguza nchi imeibiwa kiasi gan katika madini wakaanza kupinga?

Au unauongelea upinzani gani mkuu? Nchi hii ina kikundi cha wahuni ambao hawaelewi wanataka nn na wanapinga nn ndio wanaongoza kwa jina la UPINZANI.
 
Back
Top Bottom