Pendekezo: CCM ikubali kumtosa jaji Rwakibarila ili kuepusha aibu zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendekezo: CCM ikubali kumtosa jaji Rwakibarila ili kuepusha aibu zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Baija Bolobi, Apr 6, 2012.

 1. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Leo siku nzima nimefanya kazi ya kutafuta maoni kwa watawala wetu na baadhi ya majaji wazoefu, walio kazini na wastaafu. Maoni ya wengi katika niliongea nao ni kama hivi ifuatavyo:

  -Mchezo mchafu umefanyika na kwa bahati mbaya ukavuja kabla ya wakati. CCM kwa kushindwa kujizuia wakaagiza DC wa Arusha afunge ofisi ya mbunge hata kabla hukumu haijatangazwa. Hapa JF hukumu hiyo ilikuwa ni gumzo.

  -Mtakumbuka Nape alianza kampeini mjini Arusha mpaka wakili wa Lema akaiomba mahakama imuite aje kuieleza ni kwa nini anadhani uchaguzi utarudiwa. Ukweli ni kuwa tayari wakati huo mazungumzo yalikuwa yameanza na Jaji aliishawapa early indicators za kubatilisha ubunge wa Lema.

  -Majaji na wanasheria wamechukia sana kuona mwenzao amewasaliti kwa kuonyesha jinsi wanavyoingiliwa na wanasiasa. Wanakubali hili ni tatizo lakini linawaaibisha majaji kuliko wanasiasa, maana kimsingi, hawalazimishwi bali wanaombwa kupendelea. Uhuru wa mahakama haupaswi kulindwa na dola bali na mahakama yenyewe kwa kukataa kutumiwa.

  -Majaji wanakubali kuwa jaji Rwakibalira ni "M-serikali". Huu ni msemo maarufu katika korido za mahakama unaowatambulisha majaji ama wanaojikomba kwa wanasiasa, au majaji walio katika idara nyeti iliyochafuka sana (TISS). Hali kadhali Jaji Mujulizi aliyekataliwa na Lema ni "M-serikali" pia.

  -Watu mashuhuri, wanasheria na baadhi ya majaji wanashauri kuwa ni MUHIMU hukumu hii ikatiwe rufaa ili kuondoa aibu kwa judiciary nzima.

  -Wanasiasa makini ndani ya CCM wanaona rufaa ni njia nzuri ya kuiondolea aibu CCM na aibu hiyo aibebe Jaji Rwakibalira peke yake. Mmoja amekwenda mbali na kusema, mahakama ya rufaa ikimpa haki LEMA, CCM impongeze Lema kama njia ya kujiosha mbele ya wapiga na kuandaa mazingira ya awali ya uchaguzi wa 2015.

  -Mwisho, kama Jaji alivuta mshiko, hakuvuta mshiko, alishinikizwa, alijipendekeza, ibaki ni aibu yake badala ya kuwa aibu ya judiciary au dola inayodaiwa kuhonga ili kubatilisha ubunge wa Lema. Aliyefanya hivyo kama yupo, alifanya hivyo kwa matashi yake mwenyewe na si kwa niaba ya dola. Kwa bahati mbaya, Salva wa Ikulu yuko implicated na kuwa aliongea na Jaji mara kadhaa kwa kutumia lugha ya kikwao. Makarani na madereva wa jaji wamethibitisha tuhuma hizi.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wananchi hawana imani na serikali
  Wananchi hawana imani na jeshi la polisi
  Wananchi hawana imani na mahakama

  Katika hali hii serikali inapata wapi maral authoriy ya kuendelea kutawala?

  Hili walichofanya Arusha ni sawa na 'self-inflicted injury'. Sina hakika kama walikaa chini na kutafakari madhara ya hiyo hukumu waliyosuka na jaji? CCM inakufa kwa kasi ya kutisha na tukio kama la Arusha ni sawa na kumwagia petrol kwenye moto.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Tangu hukumu ilipotolewa nimekaa na kuwasiliana na vi-nzi taarifa ambazo zipo na za kuaminika zinatisha.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hebu tupashe kiongozi.
   
 5. d

  dada jane JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu tunaomba uendelee kuwaanika wanafiki.
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu mwaga jamvini nasi tupate harufu ya vi inzi hivyo.
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Kwani jaji rwakibarila ni CCM?
   
 8. M

  MUFURUKI Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Ushauri CDM isikate rufaa.Kuwatia aibu CCM ni kuomba haki kwenye sanduku la kura.Hukumu kwa nini ivuje?
   
 9. m

  mtolewa Senior Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  “ Mimi Jaji Gabriel Rwakibalira, wa mahakama kuu ya Magamba kanda ya Rukwa,
  2012 mahakama yetu, polisi yetu, chama chetu! Nimechagua kuhongwa ili kumvua ubunge jembe Lema «.

  Kila muosha huoshwa, kila mhongahuongwa!
  sishangai hata kwetu ibadakuli wapo!
   
 10. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Umemwaga hizo pumba kwa faida ya nani? Hapa ni kwa watoa hoja na wachangia hoja bana; huna, MUTE!
   
 11. T

  Turning point New Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haki ya mtu haifi !!! ikizikwa itafufuka, ikichomwa moto hutokea majivuni.
   
 12. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huuoni mkia
   
 13. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hawa mafisadi mwisho wao waja hakika nawaambieni!

  Mi ningependelea hawa mafisadi waendeleze huu mchezo mchafu waliofanya hapa A town halafu tujionee matunda yao.

  Nimeshatangulia kusema ktk thread nyingine iliyotangulia ya kwamba hawa magamba wanatikisa kiberiti wajue kama imepungua ama imejaa na hebu tusubirie majibu yao.

  Na hata hivyo majaliwa kesho mpk saa nane na nusu mchana tutakuwa na majibu toka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo na tutapata majibu ya hakika na yenye busara!

  Ndiyo maana naikubali JF! Tuna raia sambuli yote!

  Wadumu WanaJF wote popote walipo na MUNGU atuongoze na kutupa Nguvu na tujitume muda wowote kama siku zote mahala popote tulipo!

  Wao wana pesa! Sisi tuna MUNGU anayeishi na kumiliki sasa na hata Milele!
   
 14. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hakuna rufaa ya haki na nzuri zaidi ya wananchi.
  Naiomba na kuisihi CDM wasikate rufaa mahakamani, watapotezewa muda na miaka itaenda wakate rufaa kwa wana wa nchi wa Danganyika, waende kushitaki wa Danganyika.
  CCM ilidhani watashinda Arumeru na upepo huo ungewasaidia kushinda na Arusha bht mbaya mambo hayajakwenda km njozi zao zilivyokuwa
   
 15. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Cdm wana haki, vlle vile Lema kama Lema binafsi ana haki ya kulindwa heshima yake. Rufaa ni muhimu sana kuliko kukimbilia kurudia uchaguzi.
   
 16. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hoja zako zipi ulizowahi mwaga hapa JF?
   
Loading...