Pendekezo: CCM Ikiangushwa Chama Tawala Kipya Kitangaze Siku ya Mapumziko Nchi Nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendekezo: CCM Ikiangushwa Chama Tawala Kipya Kitangaze Siku ya Mapumziko Nchi Nzima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dumelambegu, Sep 9, 2012.

 1. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania,

  Kama ni kunyonywa, tumenyonywa,
  Kama ni kunyanyaswa, tumenyanyaswa,
  Kama ni kuonewa, tumeonewa sana,
  Kama ni kuuawa mikononi mwa wa watawala wetu, tumeuawa sana,
  Kama ni kucheleweshewa maendeleo, tumecheleweshwa sana,
  Kama ni kuteseka, tumeteseka sana,
  Kama ni kudharirishwa, tumedharirishwa sana,
  Kama ni ku. . . . . . . .

  Naweza kuendelea kuorodhesha mabaya yote na kujaza jamvi hili lakini niseme tu kwa ufupi kwamba yote hayo yamefanyika tukiwa chini ya chama cha mapinduzi tangu nchi yetu ipate uhuru. Hata hivyo, NURU YA MATUMAINI imeanza kuangaza na watanzania wengi tayari wameanza kusherehekea ushindi ambao muda si mrefu utapatikana. Ushindi huo si mwingine bali ni kukiangusha chama hiki kilichopoteza mwelekeo. Najua siku hiyo ipo na yaja tena i karibu sana.

  Baada ya kukidondosha chama hicho, napendekeza chama tawala kipya kiiagize serikali yake itangaze siku mbili za mapumziko ili wananchi wapate muda wa kusherehekea ushindi au kwa lugha nyingine uhuru wa pili kwa taifa letu.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Kaka umenifurahisha sana,nimecheka sana bro.
   
 3. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,468
  Likes Received: 2,137
  Trophy Points: 280
  Hii kali si wale waliotunyonya tuwachunguze na kuwashitaki wenye makosa ya kuthibitika. Ujue itakuwa hakunaga.
   
 4. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu avatar yako nimeipenda..........nani awezaye zuia hii nguvu yote ya umma?
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu unatoa pendekezo wakati hata Chadema bado hawajapata mgombea urais, aijulikani kama mgombea urais wa Chadema atakuwa Lema, Mbowe, Dr Slaa, Zitto.
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,063
  Trophy Points: 280
  Isiwe siku moja tu bali iwe wiki nzima; tutakula na kunywa mazao ya nchi yetu tuliyopewa na Mola wetu. Tutakula nafaka zetu, tutachinja maelfu ya mifugo yetu, tutakula matani ya samaki wetu. Hata na walevi siku hiyo watasherehekea. mwenye kunywa mnazi na anywe, wa chimpumu na wanywe, wa dengerua na wanywe, wa mbege na wanywe, hakika tutafurahia urithi wa mababu zetu.

  Tusherehekee kuutokomeza ufisadi.

  Tusherehekee kuutokomeza uongo.

  Tusherehekee kutokomeza propaganda chafu.

  Tusherehekee kutokomeza uonevu na mauwaji ya polisi na vyombo vingine vya dola.

  Tusherehekee kuutokomeza mauwaji ya vikongwe na albino wetu.

  Tusherehekee kuwa na vyombo vipya vya utawala - Bunge Jipya, Mahakama Mpya, na Serikali Mpya.

  Tusherehekee kuwa na Bunge ambalo ni chombo cha kweli cha uwakilishi wa wananchi; Bunge ambalo si la kuzomea wala la mawaziri kusema uongo; wala si mahali pa Spika na wenyeviti wake kunyamazisha sauti za wananchi.

  Bunge ambalo mawaziri wanatajiandaa kikamilifu kupeleka hoja za serikali.

  Serikali ambayo kazi ya mawaziri si kejeli na dharau kwa wananchi bali uwajibakji uliotukuka.

  Serikali ya Rais mwenye mamlaka na mtendaji kwa niaba ya wananchi; asiyelea ufisadi na uzembe.

  Rais ambaye wanachi hajipanga masaa mawili kabla kuisikiliza hotuba yake na akishaiwasilisha huwa gumzo nchi nzima kwani imetatua au kutoa majibu ya kero zao.

  Rais asiyechezewa chezewa na watendaji wa chini yake kana kwamba urais wake una ubia.

  Tusherehekee kuwa na Mahakama isiyokuwa na vihiyo.

  Mahakama ambayo Jaji akiamua shauri hata ukienda The Hague, hukumu inabaki hivyo hivyo.

  Tusherehekee mwanzo mpya na taifa jipya kwa wahadzabe, watindiga, na kabila na dini zote.

  How great that day shall be!
   
 7. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ritz, am sory kwa pumba zako. Sisi hatuna haja wala kiu ya madaraka kama nyie mko tayari kuua ili mradi ubaki madarakani. Sasa hiyo album mpya ya mauaji mbona imechuja haraka, inakuja toleo gani.?
   
 8. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napendekeza:-
  1:-Siku mbili/2 za mapumziko na kusahau utumwa japo kwa Siku mbili/2
  2:-Siku tatu/3 za msiba na maombolezo kitaifa maana ata ccm ikiingizwa (MOI)haita simama tena.
  3:-Siku mbili/2 za mafisadi warudishe hela zote njee na ndani ya nchi.
   
 9. FOR 2015

  FOR 2015 JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 539
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yeyote awaye,,,hilo ni pendekezo.....and the man did not identify any the political party
   
 10. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Maneno yako ni nusu ya kunitoa machozi!.. Yes!
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja za Dumelambegu na Dudus kwa 100%.

  Pia ni vizuri watu kama Ritz wakaelewa kuwa envisioning ni sehemu muhimu katika hisia za mwanadamu katika kufikia kuyapata kwa uhalisia yale anayoyatamani. Kwa hiyo wakubali na kuruhusu watu kuweka haja na matamanio ya mioyo yao juu ya nchi yao.
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Nitafurahi kama TBC 1 na redio za umma zitatumika kihalali siku hiyo kwa faida ya wananchi wote kwa mara ya kwanza toka tarehe 9/12/1961.

  Warushe sherehe hizo live bila chenga na waoneshe hatua za ukombozi ambazo kwa makusudi wanakataa kuzitangaza sasa hivi. Wananchi wote waliouawa ktk ukombozi wa nchi hii tokea Tarime, Arusha, Igunga, Iringa, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Songea na kila kona wote watapewa siku katikati ya shereehe hizo ili ndugu na jamaa za wafiwa waone kuwa damu na michango yao haikusahauliwa na wala haikuwa bure
   
 13. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Dumelambegu umenikuna sana kwa uzi huu. Naunga mkono pendekezo kwa asilimia mia zote. Kwa mateso tunayoyapata chini ya magamba, itakuwa vema tukipumzika wiki nzima.
   
 14. Root

  Root JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,217
  Likes Received: 12,928
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hiyo it will be the only moment in life it only happen once
   
 15. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  Huu uzi umekimbia wakuu du, lkn nashukuru nimewakuta


  Na Dunia Itasimama,


  · Migodi yetu

  · Ofisi zetu

  · Magari yetu ya serkali

  · Bandari zetu

  · Wanyama na mbuga zetu

  · Masikini wafanyakazi wetu

  · Maskini wanafunzi wetu shle msingi na za kata

  · Vyuo vyetu vya umma(udsm,udom,ardhi, muhas)nk

  · Hospitali zetu  • [*=left]masikini walemavu wetu
   [*=left]kina mama watapendeza
   [*=left]watoto hawataandamana tena
   [*=left]wanyama watasimama kwa kuwa hawatauzwa tena ulaya
   [*=left]wote tutatibiwa tanzania

  Vyote vitasimama nakuweka mkono qwa kulia kifuani na kutazama juu
   
 16. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  halafu wew dudus kama wewe ni Mh. MB ungeiwekaga hii hkuchangia hotuba ya waziri mkuu nchi itikisike, yaani

  KWA mawazo haya ndio maana nimeipaenda JF
   
 17. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  NAOMBA ni print hii dudus
   
 18. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135


  Duh! mimi nilifikiri waongeza masaa ya kufanya kazi nakuondoa au kupunguza siku za kupumzika ili tuzalishe zaidi na kutengeneza ajira nyingi zaidi, wewe unawaza mapumziko tena?

  Upumzike kwa lipi unajua siku 2 zitaugharimu uchumi wa nchi kiasi gani?
  fikiria tena, hatuna tena muda wa kupoteza tumekuwa tukitembea kwa muda mrefu sana sasa ni lazima tuanze kukimbia achana na mambo ya sherehe ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo sasa hivi inapaswa tupige kazi tuu hakuna kulala ikiwezekana j3 mpaka j2, kama kweli tunataka kutoka hapa tulipo, mimi kwangu ikiwezekana hata Raisi mpya aapishwe usiku baada ya kutoka kazini kesho asubuhi ni kazi tu!

   
 19. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,063
  Trophy Points: 280
  Ruksa Mkuu. Contents hapa JF ni community-based; tena ni open source. Permission has been granted to copy, modify, redistribute to any extent without permission or acknowledgment, - expressly or implied . Hapa sio yale mambo ya IMEZUILIWA au CONFIDENTIAL. Go ahead Mkuu.
   
 20. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Eliah G Kamwela says thanks for this very useful post.
   
Loading...