Penati ya Messi na Suarez sio ya kwanza, Henry, Pirez walichemsha

poposindege

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
453
175
Jana mchezaji Bora wa dunia mara tano Lionel Messi alifanya kitu cha ajabu wakati alipokwenda kupiga penati dhidi ya timu ya Celta Vigo na kutoa pasi kwa Suarez badala ya kufunga.

Messi alikimbia kidogo na kufanya kama anapiga kuelekea golini lakini aliupiga mpira kidogo kwa pembeni na Luis Suarez akafunga goli na kufanya Barcelona kupata bao la tano. Barcelona ilishinda mchezo huo kwa jumla ya Magoli 6-1 na kuendelea kuongoza Ligi ya La Liga.

Messi angefunga mwenyewe penati hiyo angekuwa anafikisha magoli 300 katika La Liga.
Hata hivyo staili hiyo si ya kwanza katika mchezo wa kandanda. Kwa mara ya kwanza ilikuwa kwa mchezaji Rik Coppens na Andre Piters wa timu ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya Denmark mwaka 1957.

Mwaka 1964 wachezaji Mike Trebilcock na John Newman wakichezea timu ya plymouth dhidi ya Manchester city nao walitumia staili hiyo na walifunga.

Staili hiyo ilipata umaarufu zaidi mwaka 1982 kutoka Gwiji la soka Johan Cruyff na Jesper Olsen. Johan alitoa pasi kwa Jesper na kisha kurudishiwa tena na kufunga.

Mwaka 2005 staili hii iliingia doa pale Robert Pires na Thierry Henry waliposhindwa kufunga na kupoteza nafasi dhidi ya Manchester City.
 
hii style nilishaifanya sana utotoni ktk mechi za mchangani,kilichokuwa kinanifurahisha ilikuwa jinsi timu pinzani zinavyobisha tukiwafunga style hiyo
 

Hapa Messi kaonyesha uungwana sana



Huyu jamaa kwakweli sijapata kuona ktk wachezaji bora waliopita na wa sasa kwa nidhamu na n.k...ni mchezaji mwenye sifa nzuri mno wa kuigwa, hana Majivuno ni mstaarabu,mpole na asiependa shari na kikubwa zaidi yeye ni mtu asiekuwa na tamaa ya kufunga,
 
Lonely Mess hawezi kufunga penati kashajaribu mara nyingi sana na ameishia kupaisha au kumpa kipa!

Bora suarezi kamuondolea aibu hiyo kubwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom