Elections 2010 PEMBETATU YA USHINDI: Kuelekea kuyatikisa Malango ya CCM

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
Tunahitaji Rais mpya, Tumaini Jipya na akili mpya na ni kweli kabisa kipindi hiki ndio cha kufanya mageuzi ya uongozi, tumewajaribu na sasa wameshindwa kuna kila sababu ya kufanya mabadiliko
 
Nalazimika kuandika hili kama kuwatia shime wale wote ambao wanataka kweli mabadiliko nchini kupitia chama hicho kuondoa vizuizi vyote vya kihisia na kiakili na kutumia nafasi hii ya kihistoria kuweza kuigombania ipasavyo nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano.
Ninaamini watakaoipigia Chadema itakuwa ni full suit au a trident....................Hakuna atakayeipigia Chadema halafu ajidhoofishe kwa kumpigia JK au mgombea mwingine wa Uraisi
 
Sipati picha itakuwaje safu ikiwa hii, maana hapa itainclude mpaka wachezaji wa kununu kwenye dirisha dogo
Slaa, Mbowe, Zitto, Mnyika, Mdee, Mpendazoe hao ni baadhi ya wachezaji wakongwe wakisaiidwa na wa dirisha dogo Mwakyembe, Ole sendeka, Magufuli, hicho kitakuwa ni kikosi cha ushindi, siku mia moja (First quarter ya 2011) nchi lazima ipate shape na mwelekeo
 
Mkuu Mwanakijiji.
naona umemwecha kwenye orodha Tundu Lisu ambaye amekuwa akifaya kazi za uharakati kwa jamii na kujijengea heshima kubwa kwa kusaidia jamii kujitambua na kujua haki zao seuse kuzifatilia.
Jamaa ni msemaji na mjenga hoja hodari.

Nakubaliana kimsingi na bandiko lako la pembe tatu ya ushindi...
 
Pembetatu hiyo haiwaondoi wapiganaji wengine... inawahusisha wote chini ya makamanda hao..

By the way.. nimefanya mazungumzo ya kina na Dr. Willibrod Slaa... yatapatikana kwa njia ya CDs pote Tanzania..
 
Sipati picha itakuwaje safu ikiwa hii, maana hapa itainclude mpaka wachezaji wa kununu kwenye dirisha dogo
Slaa, Mbowe, Zitto, Mnyika, Mdee, Mpendazoe hao ni baadhi ya wachezaji wakongwe wakisaiidwa na wa dirisha dogo Mwakyembe, Ole sendeka, Magufuli, hicho kitakuwa ni kikosi cha ushindi, siku mia moja (First quarter ya 2011) nchi lazima ipate shape na mwelekeo

umewasahau shibuda na lwakatare
 
Huyu hapana!
 
Kiukweli tunahitaji mabadiliko tena kwa haraka. Lakini bahati mbaya iliyopo hakuna anayefaa kutuletea haya mabadiliko kwa sasa. Si wapinzani wala chama Tawala.
 
kwa hiyo turudishe wakoloni waje kutuwala
 
Pembetatu hiyo haiwaondoi wapiganaji wengine... inawahusisha wote chini ya makamanda hao..

By the way.. nimefanya mazungumzo ya kina na Dr. Willibrod Slaa... yatapatikana kwa njia ya CDs pote Tanzania..

Hiki ndicho nilitaka kukuuliza na nakumbuka nimewahi kukuuliza facebook "hivi huwezi pata namna uka ongea nao na uwa shauri?"
Am proud of you Mzee,you are genious!!
 
Mwanakijiji said "Ninaamini kuna mambo kama matatu au manne ambayo Chadema wakiamua kweli kuyafanya siyo tu kwamba watashika hatamu ya uongozi lakini wataonekana kwa haki kabisa wamestahili kufanya hivyo na hakuna mtu atakayeweza kuamua vinginevyo".

Mwanakijiji una uchambuzi yakinifu. Sasa ungetumalizia kabisa kuhusu hayo mambo matatu au manne ambayo Chadema inabidi iyafanye ili kupata ushindi, au ni top secret? Basi ingekuwa busara kama ungeweza kuongea na Dr Slaa ili kumpa ushauri huo kama unaona kumwaga mchele hapa sebuleni si vizuri.

Ninakubaliana na wewe kabisa kwamba kujaza watu mikutanoni Chadema isibweteke na kuona kwamba imeshinda. Nakumbuka Lwatonga Mrema alivyokuwa anajaza watu kipindi kile anagombea Uraisi, lakini alishindwa tokana na kubweteka kwani mlundikano wa watu katika mikutano yake ulimdanganya.
 
Kiukweli tunahitaji mabadiliko tena kwa haraka. Lakini bahati mbaya iliyopo hakuna anayefaa kutuletea haya mabadiliko kwa sasa. Si wapinzani wala chama Tawala.
Pole mkuu. Dr. Slaa anaweza. Mpe kura yako
 
Pembetatu hiyo haiwaondoi wapiganaji wengine... inawahusisha wote chini ya makamanda hao..

By the way.. nimefanya mazungumzo ya kina na Dr. Willibrod Slaa... yatapatikana kwa njia ya CDs pote Tanzania..

Hizo CD hapa dar zinapatikana wapi?
 
Kiukweli tunahitaji mabadiliko tena kwa haraka. Lakini bahati mbaya iliyopo hakuna anayefaa kutuletea haya mabadiliko kwa sasa. Si wapinzani wala chama Tawala.

hata wale wasiopenda kufikiria kimapinduzi, watalazimika kufanya hivyo maana. wengi wamezoea matatizo, umaskini mpaka inafikia hatua wanadhani walizaliwa TZ ili wawe maskini!! Lakini dhana hiyo imeshindwa
 
Utatu kama wa kwenye msahafu wa kikristo, (Mungu baba, Mungu mwana na Mungu Roho) ujumlimshe na mitume wengine kama wakina Shibuda, Mnyika, Tundu Lissu..........) TUJIANDAE KUSHEREHEKEA KUAPISHWA KWA DR. SLAA THE 5TH PRESIDAAA...
 
Nafurahi kuona Mzee Mwanakijiji hatimaye umebadilika vizuri. Mwanzoni ulidhani wakati sio huu, (na ukaandika mada ndefu kusema hivyo). Akina Mkandara na sisi wengine tulijitahidi sana kukushawishi kwamba ni sasa.

Sio wakati muafaka wa kujadili aliyechangia zaidi ni nani, ila moyoni mwangu namdhamini sana Mwanasheria wa Dr Slaa (Tundu Lisu). Wameichachafya CCM kwa pamoja hasa wakati wa kesi dhidi ya Slaa ya Ubunge wa Karatu.
 
Nafurahi kuona Mzee Mwanakijiji hatimaye umebadilika vizuri. Mwanzoni ulidhani wakati sio huu, (na ukaandika mada ndefu kusema hivyo). Akina Mkandara na sisi wengine tulijitahidi sana kukushawishi kwamba ni sasa.

Hapana.. watu wengine ndio walisema hivyo, miye sijabadilika niko kama nilivyokuwa five years ago. I can't control how other people infer from what i write.
 
Back
Top Bottom