Polisi wadai Pembe za faru zilizokamatwa feki

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Pembe za faru zilizokamatwa feki - Polisi

Na Berensi Alikadi, Bunda

KIKOSI cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Serengeti kilichopo wilayani Bunda, mkoani Mara kimesema kuwa watu wawili waliokamatwa na pembe zinazodaiwa kuwa za faru si watumishi wa kikosi hicho.

Akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Mkuu wa kikosi hicho Kanda ya Serengeti, Hassan Nkusa, amesema kuwa hakuna mfanyakazi wa kikosi chake aliyekamatwa na kwamba wafanyakazi wake wote wapo kikosini.

Alisema kuwa ameshangaa kusikia habari hizo kuwa kuna watu wawili wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza na pembe za mnyama aina ya faru anayesadikiwa kuwa ni yule aliyekuwa akiitwa George, ambaye aliuawa hivi karibuni katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Nkusa aliwataja watu waliotajwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mwanza kuwa ni Akilus Jacob na Kasika John Joseph, ambao wote inasadikiwa kuwa ni wakazi wa Bunda na kudai kuwa madai yaliyotolewa kuwa Alikilus Jacob ni mfanyakazi wa kikosi hicho ni ya uongo.

Mkuu huyo alifafanua kuwa hivi karibuni kuna watu wawili Shabani Hamis Ngochoge na mke wake, Monica Hamis, wakazi wa mjini Bunda walikamatwa na Jeshi la Polisi wakiwa na pembe bandia za faru ambazo zilikuwa zimetengenezwa kwa kutumia ngozi ya mnyama aina ya nyati na kwamba walikuwa katika harakati za kuziuza kwa sh milioni kumi kwa raia wa Kenya kabla ya kufikishwa mahakamani na sasa kesi yao inaendelea.

Alisema huenda watu hao wakawa na mtandao mkubwa wa kutengeneza pembe hizo bandia na kuwauzia wananchi hivyo aliwataka watu kuwa macho na watu hao kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola pindi watakapowaona.

Nkusa alimshushia lawama nzito kaimu mkuu huyo wa polisi kwa kuutangazia umma habari za uongo kabla hajafanya uchunguzi na bila kuwasiliana naye ili aweze kumthibitishia kama kweli watu hao waliokamatwa ni wafanyakazi wa kikosi anachokiongoza yeye.

Kwa kweli mimi pamoja na wenzangu hapa ofisini tumemshangaa sana huyo kaimu kamanda kwa kutoa taarifa za uongo kwa wananchi ambazo mimi naziona kama zilikuwa na lengo la kunipaka matope na kuniharibia kazi, haiwezekani mimi na askari wangu tuliokabidhiwa dhamana ya kulinda maliasili harafu tufanye kitendo hicho, alisema Nkusa kwa masikitiko makubwa.

Naye Mkuu wa kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Ziwa kilichopo jijini Mwanza, Elias Mzee, alipohojiwa kama kweli pembe hizo zilizokamatwa ni za faru, alisema kuwa pembe hizo si za faru bali zimetengenezwa kijanja na kwamba walizifanyia utafiti jana kwa kutumia wataalamu wa Idara ya Wanyamapori na kugundua kuwa ni feki.

Juzi Kaimu Kamanda wa Polisi, Nonosius Komba, alitangaza katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa jeshi lake lilikuwa limefanikiwa kukamata pembe za faru aitwaye George aliyekabidhiwa Rais Kikwete katika Hifadhi ya Serengeti.

Tanzania Daima jana ilimtafuta kaimu kamanda huyo ili kujua ni kwanini alitoa taarifa za uongo na kuudanganya umma lakini simu yake haikuweza kupatikana.
 
Isije ikawa hawa polisi wamezificha pembe hizo na sasa kudai ni feki...................ili kuwanusuru watuhumiwa......................siwaamini polisi wetu hata kidogo................
 
Isije ikawa hawa polisi wamezificha pembe hizo na sasa kudai ni feki...................ili kuwanusuru watuhumiwa......................siwaamini polisi wetu hata kidogo................

Zile pembe nasikia dili sana huko Asia wanatengenezea dawa za kuongeza nguvu za kiume
 
Polisi wa Tanzania ni wanamazingaombwe wakubwa sana,mwaka jana madawa ya kuleva zaidi ya kilo 50 yaliokamatwa mpakani Tunduma.Yaligeoka Unga wa Ngano yalipofika Makao Makuu ya Polisi Dar.So akuna Ubishi
 
Nkusa alimshushia lawama nzito kaimu mkuu huyo wa polisi kwa kuutangazia umma habari za uongo kabla hajafanya uchunguzi na bila kuwasiliana naye ili aweze kumthibitishia kama kweli watu hao waliokamatwa ni wafanyakazi wa kikosi anachokiongoza yeye.

Hakuwa na haja ya kusema yote hayo kama kweli ana busara...............
 
Yale yale ya mbeya, madawa ya kulevya baada ya wiki yakageuzwa kuwa unga wa sembe na jamaa akapewa special zone ya kipolisi.
 
Back
Top Bottom