Pembe za faru wa JK zabambwa Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pembe za faru wa JK zabambwa Mwanza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohammed Shossi, Jan 18, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Monday, 17 January 2011 20:24 0diggsdigg

  Frederick Katulanda, Mwanza
  POLISI mkoani Mwanza, imewakamata watu wawili akiwamo afisa wa wanyama pori, Allchraus Jacob (31), wakijaribu kuuza pembe za kifaru maarufu kwa jina la George (12) akifahamika kama faru wa Rais Jakaya Kikwete, aliyeuawa na majangili, Desemba mwaka jana.Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na polisi mkoani Mwanza, zimemtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni mkulima wa wilayani Bunda, Kasika John (44).

  Faru huyo maarufu kwa jina la George (12) na wengine wanne, wamekuwa wakifahamika zaidi kama faru wa JK, kutokana na Rais Kikwete kuwapokea faru hao wakati wanaingizwa nchini Mei 21 mwaka 2010 na kuahidi kuwapa ulinzi mkubwa kuliko ule anaopewa yeye.

  George (12), aliuawa Desemba 12 mwaka jana majira ya saa 12.30 jioni, eneo la Nyabeho katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na wauaji hao kutoweka na pembe zake zote. Hata hivyo mzoga wake ulipatikana Desemba 14.

  Kukamatwa kwa watuhumiwa hao, kumekuja siku chache tangu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alipotangaza kulijitosa kwenye doria ya kuwasaka majangili wanaotuhumiwa kumuua Faru huyo.

  Waziri Maige aliendesha doria hiyo Januari 2, mwaka huu kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ambapo walikwenda katika eneo la Moru ndani ya hifadhi hiyo huku akitoa maagizo ya kuimarishwa kwa doria za mara kwa mara.

  Alisema lazima majangili wote waliomuua Faru huyo aliyekuwa akiitwa George ambaye aling’olewa pembe na mzoga wake kuachwa eneo la tukio, wanakamatwa na kwamba juhudi zimeaanza kuonekana kwani tayari watuhumiwa 10 walikuwa wamekamatwa.
  Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja iwapo waliokamatwa jana ni miongoni mwa wale 10 ambao Waziri Maige aliwataja.
  Jana Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Nonosius Komba alisema jeshi lake lilifanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa watu waliokuwa wakitafuta soko la pembe za faru na kuweka mtego.

  "Tuliwakamata watu hao wawili wakati wakijaribu kuwauzia maofisa wa polisi waliojifanya wateja pembe za faru huyo," alisema kaimu kamanda huyo wa polisi.

  Kamanda Komba alieleza kuwa watu hao walitiwa mbaroni Januari 15 mwaka huu saa 5: 30 asubuhi, eneo la Nyakato National, baada ya polisi hao kukutana nao katika gari waliloliandaa kama la mteja aliyekuwa akitaka kununua vipusa hivyo.

  “Kwa maelezo yao wanasema pembe hizo zina soko kubwa sana katika nchi za Falme za Kiarabu na Japan ambako hutumika kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume," alisema kamanda Komba na kuongeza:

  "Zikinunuliwa husagwa na kuwa unga na watumiaji wake huweka katika chai ama maji ya moto na hivyo kuwasaidia kama dawa.”

  Kamanda Komba alisema pembe hizo sasa zitapelekwa kwa mkemia na watalaamu wa maliasili ili kuzithibitisha iwapo ni pembe za faru na kama faru huyo ni yule aliyeibwa kwenye mbuga ya Serengeti Desemba 12 mwaka jana.

  Faru huyo dume aliyekuwa akijulikana kwa jina la George (12), aliletwa nchini na kampuni ya uwekezaji ya Grumeti Reserve na Kikwete aliahidi kuwa wanyama hao watapewa ulinzi mkali kuliko ule anaopewa yeye.

  Kabla ya taarifa za kuuawa kwake hazijatolewa kwa waandishi wa habari Desemba 14 mwaka jana, kuliitishwa kikao kati ya uongozi wa Frankfurt Zoloogical Society, Grumeti Reserve na Tanapa ambacho kilijadili tukio hilo kwa saa tatu mfululizo.

  Baadaye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi Tanzania (Tanapa), Edward Kishe alithibitisha tukio hilo akisema, ”Ni kweli faru huyo aliuawa Desemba 12 na mzoga wake ukapatikana Desemba 14 mwaka huu ukiwa hauna vipusa.”

  Alisema kabla ya hapo kifaa cha mawasiliano ambacho faru huyo na wenzake wanne waliwekewa, kilipoteza mawasiliano na walinzi, na walipofuatilia walibaini kuwa faru huyo alikuwa ameuawa na majangili katika eneo Nyabeho lililoko karibu na vijiji vya Ikoma na Robanda.

  Alipotakiwa kutoa ufafanuzi kama tukio hilo halitakuwa limewavunja moyo na kuharibu uhusiano na wadau waliosaidia, alikataa na kudai hata huko Afrika Kusini matukio kama hayo yamekuwa yakitokea.

  Kuhusu ahadi ya kuwawekea faru hao ulinzi mkali unaozidi wa rais, mhifadhi mkuu wa Serengeti, Mtango Mtahiko alisema tukio hilo limewastua sana kwa kuwa wanafanya jitihada kubwa za kuwalinda faru, ambao ni aina moja kati ya tano za wanyama wakubwa barani Afrika ambao ni kivutio kikubwa cha utalii.

  Alisema wanajitahidi kuongeza nguvu kwenye ulinzi ili kukabiliana na matukio hayo. Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2009 hadi sasa, zaidi ya tembo 15 wameuawa na meno kuchukuliwa.

  Hata hivyo alisema hawajajua soko kuu la meno ya tembo liko wapi ,hata hivyo alikiri kuwa kuna taarifa za kuwepo kwa soko zuri la meno ya tembo na kuwa wanashirikiana na polisi kwa upelelezi.

  Mei 21 mwaka huu Faru watano ambao ni Cleo (ke), Ethna (ke), Lunnar (ke), Benj (me) na George (me) ambaye ameuawa.

  Akipokea faru hao, Rais Kikwete alisema Afrika Kusini imeongeza uwezo kwa Tanzania kwa kuleta faru hao weusi na kuwa ongezeko hilo ni la manufaa kwa taifa na kuahidi kuwa "huduma zake na ulinzi zitakuwa za kipekee zaidi yangu mimi”.

  Naye waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga alisema kwa miaka 1970-1980 ujangili ulipunguza faru na kwamba "sasa tutahakikisha hakuna ujangili kwa faru... tutaweka askari maalum wa kuwalinda wanyama hao”.

  Mkurugenzi wa Sangita Grumeti, Brian Harris alisema faru hao walitolewa kwenye zuu na kuwa kazi zote ikiwa ni pamoja na kununua na kuwasafirisha ziligharimu Sh7.5 bilioni.

  Mkurugenzi wa Frankfurt Zoloogical Society, Gerard Bigurube ambaye awali alikuwa mkurugenzi mkuu wa Tanapa, alisema wajibu wao ni kuwezesha usafiri, mafunzo kwa askari na kuhakikisha hakuna madhara kwa wanyama hao.

  Habari zaidi zinasema kuwa maslahi madogo kwa askari na viongozi kupuuza ushauri wa kuwaweka faru hao kwenye hifadhi ndogo yamechangia kuzorota kwa ulinzi wa wanyama hao.

  Habari zinasema askari wachache wa hifadhi hulazimika kufanya doria mchana na usiku ili kukabiliana na wimbi kubwa la majangili wanaotumia silaha mbalimbali, zikiwemo za kivita.

  Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa mara baada ya kuletwa faru hao askari wadogo walishauri wawekwe kwenye zuu lakini uongozi wa hifadhi uliwapuuza na kudai wangeimarisha doria kwa kuwa walifungiwa vifaa maalum vya mawasiliano.

  Baadhi ya askari ambao hawakutaka majina yao yaandikwe walisema kasi ya ujangili haitaweza kupungua kutokana na mianya ya kiutendaji iliyopo ndani ya hifadhi hiyo, likiwemo suala la maslahi duni.

  Walisema askari hulipwa Sh10,000 wawapo doria bila kuangalia ni wakati wa operesheni kama ilivyo wakati huu ambao inadaiwa pori hilo limevamiwa na majangili wenye silaha za kivita.

  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, kaimu mkurugenzi mkuu wa Tanapa, Edward Kishe alikana na kudai kuwa wanajitahidi kuwatimizia maslahi yao, lakini hakubainisha kama wameyaboresha kwa kiasi gani.

   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Inaelekea hili tatizo la nguvu za kiume ni kubwa sana katika jamii yetu na nje pia, maana kila ninapopita mitaani huona matangazo za waganga wa kuongeza/kuvuta mpenzi na kuongeza nguvu za kiume. Ukisoma magaazeti hasa ya udaku utaona matangazo zaidi ya kumi ya kuongeza nguvu za kiume. Wasiwasi wangu asijekutokea mwendawazimu mmoja akasema hata pembe ya binadam inaongeza nguvu za kiume watu wakaanza kuviziana.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hii Kali. Ngoja tui google tuone kama ni kweli
   
 4. k

  ksalama0 Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa nini watumishi wa ngazi za chini walio wengi hawasikilizwi ingawa wanatoa maoni mazuri ambayo yanawasaidia wakubwa wa kazi ili utendaji uende vyema? Je ni wakubwa kuona aibu kuwa uamuzi mzuri umetoka kwa mfanyakazi wa ngazi ya chini? Hebu maboss muwe wasikivu kwa kuchuja mawazo ya wafanyakazi wenu wa ngazi za chini itawasaidia kufanya kazi zenu kwa ubora zaidi na bila kunung'unikiwa na mfanyakazi yeyote. Nawakilishaaaa!!!
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Yeah, kama ni kweli basi bora sisi ndo tuwe wakwanza kufaidi maana tatizo la nguvu za kiume hata hapa tz lipo. kwa nini dawa ipo lakini inapelekwa nje?
   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu tatizo kama lipo ni dogo sana sio kama mahitaji yanavyoonyesha, tatizo lililopo wanaume wengi wanapenda "kukomoa" hii in a long run baadae inaleta madhara makubwa kwenye organs za uzazi wa mwanaume na kutokufanya kazi kabisa. Nguvu uliyonayo ndio stahiki yako itumie ipasavyo na si kuiongezea.
   
Loading...