Pembe za Faru (Viagra pori) zatiwa sumu ili kulinda uhai wa Faru

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,596
1,071
Wahifadhi huko Afrika Kusini wamekuja na mbinu mpya ya kuwalinda faru dhidi ya wawindaji haramu. Katika Pori la Hifadhi la Dinokeng wameamua kutia/ kuchanjia pembe au vipusa hivyo sumu na kuwataharadhisha wawindaji haramu (majangili) kwa kuzipaka rangi ya pinki.

Biashara ya vipusa imeshamiri kutokani na imani potofu kuwa ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume. Hata hivyo uvumbuzi wa dawa ya Viagra miaka ya karibuni umetoa ufumbuzi kwa tatizo hili.

Viagra 2.jpg

Viagra ya Pembe za Faru yatiwa yatiwa sumu kulinda.jpg

Kwa mtindo huu ni kwamba watakaotumia dawa zitokanazo na vipusa watakuwa wanakatisha maisha yao.
Takriban faru 200 wameuwawa mwaka huu huko Afrika kusini.

Chanzo cha habari ni : Rhino horns poisoned and painted PINK to keep poachers away in revolutionary scheme in South Africa | Mail Online.
 
Hao jamaa waje na huo ujuzi hapa Bongo
ila iwe kwaajili ya Ndovu maana wanateswa
sana kila siku wanauwawa kama vile wako
ugenini. Ila Mzee K Bariiidii kajua tayari.
 
Ubunifu mzuri sana tunaomba jeikei akachukue hao wataalamu kama anavyotaka kuwaleta wazee wa blunt kuja kufundisha.
 
Hao jamaa waje na huo ujuzi hapa Bongo
ila iwe kwaajili ya Ndovu maana wanateswa
sana kila siku wanauwawa kama vile wako
ugenini. Ila Mzee K Bariiidii kajua tayari.[kwaajili ya Ndovu maana wanateswa]
Bila shaka mkutano unaofanyika huko Iringa utazingatia jmbo hili. Mhesh Msigwa upo hapo??
 
Hao jamaa waje na huo ujuzi hapa Bongo
ila iwe kwaajili ya Ndovu maana wanateswa
sana kila siku wanauwawa kama vile wako
ugenini. Ila Mzee K Bariiidii kajua tayari.

Hiyo na. 2. Na. 1 ni kwamba walikata pembe za faru ili kuwanusuru na majangili. pembe zikahifadhiwa strong room. Faru wamepona kuuawa lakini strong room ikavunjwa!! Hii itafaa hapa kwetu ili kuwanusuru tembo waendelee kuzaa wakati majangili yanazeeka. Baada ya miaka kama ishirini kutakuwa hamna majangili kwani ile succession process itakuwa imetibuliwa!!
 
Uwoya! Kumbe mtoto wa Jangili ni jangili. Mbona operation Uhai ya 1980s chini ya Waziri Mama Mongela haikukimaliza kizazi cha majangili Tanzania? Basi naamini nguvu za kijeshi au polisi sio ufumbuzi wa matatizo.
 
Mimi nina ujizi wa kufunga cctv wakinipa tenda nitawafungia watawanasa wauaji kirahisi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom