TANZIA Pemba: Watu 9 wafariki dunia baada ya boti kuzama baharini. Zoezi la uokoaji kuendelea asubuhi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Watu 9 wamefariki dunia na wengine 6 kuokolewa wakiwa hai baada ya boti kuzama baharini Kisiwani Pemba wakati watu hao wakitokea Chakechake kwenda kisiwa cha Panza kwenye shughuli za mazishi.

Zoezi la uokozi limesitishwa usiku na litaendelea Januari 5, 2022 asubuhi.

Shahidi katika tukio hilo amedai kuwa wazamiaji waneona maiti zaidi ya 12 zilizokwama lakini wameshindwa kuziopoa kutokana na giza kuingia.

Ameongeza kuwa Boti ilikuwa imebeba wanaume watupu baada ya wanawake kukosa nafasi kutokana na chombo hicho kujaa sana.
-
Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Pemba, Richard Mchomvu amethibitisha ajali hiyo.

Boti ya kwanza ambayo ilibeba mwili wa marehemu ilivuka salama lakini nyingine ambayo ilikuwa na ndugu wa marehemu na waombolezaji wengine wanaokisiwa kufikia 30 ilipata shida baharini na kuzama.

Mpaka sasa waliookolewa ni watu sita wote wanaume na kuna maiti 9 zimeopolewa, zote za wanaume watu wazima. Zoezi la uokozi litaendelea kesho asubuhi saa 12. Kuna watu bado wapo kwenye maji.
- RPC Mchomvu
 
انا لله وانا اليه راجعون

Hakika sisi ni wa ALLAH na kwake tutarejea

Poleni sana wazanzibari wote
 
Poleni sana wafiwa.
Tuliwahi kupewa angalizo kwamba unaposafiri ndani ya maji, jitahidi kuvaa nguo nyepesi na sendozi (viatu vya kuchomeka), inarahisisha wakati wa kujiokoa katika majanga kama haya!
 
Back
Top Bottom