Pemba waomba barabara inayoenda kwenye kaburi la maalim Seif iwekwe lami ili kuwapa wepesi maelfu ya watu wanaozuru kaburi kila siku

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
44,323
2,000
Wananchi wa Pemba wameiomba SMZ iijenge kwa kiwango cha lami barabara iendayo kwenye kaburi la Maalim Seif kwani imeharibika sana hali inayopelekea magari kupakiwa umbali wa km 3 kutoka eneo la kaburi.

Ombi hilo limetolewa mbele ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar mh Othman Masoud aliyezuru kaburi hilo kwa ajili ya kusoma dua.

Chanzo: ITV habari

My take; Huyu Maalim Seif yawezekana ni nabii.
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,770
2,000
Kwa hiyo wameifanya kaburi ya marehemu Maalim sehemu ya kuabudu? Ndo mafundisho ya dini yao, au Mtume SAW??
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
716
1,000
Wananchi wa Pemba wameiomba SMZ iijenge kwa kiwango cha lami barabara iendayo kwenye kaburi la maalim Seif kwani imeharibika sana hali inayopelekea magari kupakiwa umbali wa km 3 kutoka eneo la kaburi.

Ombi hilo limetolewa mbele ya makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar mh Othman Masoud aliyezuru kaburi hilo kwa ajili ya kusoma dua.

Source ITV habari

My take; Huyu maalim Seif yawezekana ni nabii sijajua kule Geita
🤣🤣🤣🤣Mfukunuzi katika ubora wako, ngoja waje wazee wa legacy
 
Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
2,053
2,000
Kama ndivyo sawa, ila mleta uzi alisema inawezekana MAALIM ni nabii, sijui anatumia kigezo gani
Nafikiri kigezo ni jinsi LEGACY yake inavyojijenga yenyewe automatically kwa kupigania UTU wao HAKI na USAWA kiasi watu wanamlilia MUNGU awaletee Maalim mwingine kma yule

Tofauti na ile LEGACY ya CHATO inayolazimishwa japo maalim hajawajengea MADARAJA wala hajawanunulia NDEGE kwa CASH watu wa PEMBA na UNGUJA
 
Mbunge Wa Kitaa

Senior Member
May 25, 2014
114
250
Nafikiri kigezo ni jinsi LEGACY yake inavyojijenga yenyewe automatically kwa kupigania UTU wao HAKI na USAWA kiasi watu wanamlilia MUNGU awaletee Maalim mwingine kma yule

Tofauti na ile LEGACY ya CHATO inayolazimishwa japo maalim hajawajengea MADARAJA wala hawajanunulia NDEGE kwa CASH watu wa PEMBA na UNGUJA
Mkuu una chuki Binafsi, Legacy ya Hayati JPM hailazimishwi. JPM ameitumikia nchi yake kwa nguvu kubwa mno toka akiwa Waziri. Mimi na wewe yawezekana hata level ya Mtaa bado hatujafanikiwa. Tutofautishe chuki binafsi na ukweli kuhusu mtu. Mimi sikuwa mpenzi sana wa Maalim Seif lakini namkubali, jamaa alikuwa mwanasiasa kweli. JPM huku kitaa watu bado wana huzunika na aliaminika na watu wengi kuliko wale ambao hawakuwa upande wake. Kila mtu hawezi pendwa na wote lakini ukweli hubaki ni ukweli kuwa mtu unaweza usimpende lakini kafanya mengi kwa Taifa lake. Tujitahidi na sisi tuitumikie nchi hata kwa level ya mtaa badala ya kuwa vinara wa kuwasema watu wakati sisi hata mtaani hatujafanya jambo. Tofauti za hoja hazimfanyi mtu awe mbaya kwako. Mungu Ibariki Tanzania. Wananchi wa Pemba wasikilizwe na kama fungu lipo wajenge barabara kwa ajili ya kuwafanya watu kufika katika kaburi la Maalim Seif Sharif Hamad.
 
luck

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,141

mkuu unaanzaje kutetea liu.wa.ji hilo lililojaa chuki za kila aina
 
Mbunge Wa Kitaa

Senior Member
May 25, 2014
114
250
mkuu unaanzaje kutetea liu.wa.ji hilo lililojaa chuki za kila aina
Mimi sikuuona uuaji wa JPM zaidi ya kuona fablication za watu hasa wana siasa wa chama chetu CHADEMA. Kuna mambo sikumuunga mkono kama Rais wangu lakini Mengi nilimuunga mkono ambayo niliona yana manufaa kwa nchi yetu. Ukiwa Rais lawama zote ni zako na mazuri ni yako. Mimi kilio changu ni kuwa na siasa zenye tija kwa nchi za kushindanisha sera. Hapa nina kiu kubwa kuona hayo yakija. Tumsamehe kama binadamu kwa yale ambayo hakufanya vizuri, tuchukue Mazuri kama watanzania na wanasiasa yatalifaa taifa mbeleni huko pamoja na sasa.
 
  • Thanks
Reactions: ris

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom