Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,219
- 40,454
Whether tuhuma hizo ni za kweli au vinginevyo, nawapongeza Polisi kwa jambo moja - wamewaita wakaripoti kituo cha Polisi. Baada ya wao kutii agizo la Polisi, wamepewa dhamana. Hivyo ndivyo Jeshi la Polisi linavyotakiwa kufanya kazi zake.
Mshauri mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi na Uenezi wa ACT Wazalendo Salim Bimani wameripoti katika Kituo cha Polisi Wete Pemba asubuhi ya leo.
Viongozi hao wa ACT Wazalendo wameitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jinai (RCO) Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Wananchi na Wanachama wa ACT - Wazalendo wamekuwa nje ya maeneo ya karibu ya jengo la Polisi la Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa lengo la kujua hatma ya viongozi wao wanaohojiwa na inadaiwa wamejiandaa na kuwachukulia dhamana ikibidi.
UPDATE:
Mshauri Mkuu wa ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Salim Bimani wameshutumiwa kufanya mkutano bila kibali mwezi Desemba 2019 huko Micheweni Zanzibar.
Hata hivyo, Viongozi hao wameachiwa kwa dhamana na kupitia Mtandao wa Twitter Chama chao kimedai kuwa walifanya mkutano wa ndani usiohitaji kibali.
Jeshi la Polisi limewachia kwa Dhamana Mshauri Mkuu wa Chama @ACTwazalendo Maalim Seif Sharif Hamad na M/kiti wa kamati ya Itikadi na uenezi wa Chama hicho Salim bimani Baada ya hii leo kuitwa kufanyiwa mahojiano na Jeshi hilo katika kituo cha Polisi mkoa wa kaskazini Pemba.
Siyo mambo ya kuteka au kupoteza watu. Kuteka watu ni primitivity ya kuwango cha juu kinachotuondoa kwenye haki ya kuitwa binadamu wastaarabu. Hatuwezi kuishi kwenye nchi ya kuwindana kama simba na pundamilia. Sisi ni wanadamu, tunastahili kuonesha utofauti wetu na wanyama wa porini waliokosa akili na hekima.
Ni mapema sana kutamka kama vyombo vya ulinzi na usalama, vinaanza kurudi kwenye kanuni zake za utendaji kazi, au hii ni isolated case.