Matope
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 892
- 679
Kamanda Siro alisema tume inawasababishia na kuwapa wakati mgumu.
WaTanzania sasa tunaelekea kule ambako vyombo vya ulinzi huenda mwisho wake vikaungana na wananchi, jambo ambalo limeonekana nchi nyingi, haiwezekani utumie vyombo vya ulinzi kuteketeza wananchi, wananchi ambao ndio wanaounda vyombo hivyo na kuvifanya viwepo kwa ndugu na jamaa zao na kodi wanazolipa.
Ipo limiti ya vyombo hivyo kufanya kazi kwenye nchi inayoongozwa kiraia kutokana na ridhaa za watu, leo hii CCM inafanya mambo kihuni na kama haitoshi inavihusisha vyombo hivyo pasina sababu ya msingi au yenye uzito, kama hapa tulipo huu si wakati wa kutumia vyombo hivyo, CCM inavitumia bila ya aibu na kuwatishia hata kuwafuta kazi wasipotimiza utumwa wa udhalilishaji.Vyombo hivi inabidi vijitathmini vinafanya kazi kwa ajili ya CCM au serikali na wananchi, hapa tulipo kiukweli hakuna serikali ni katiba mbovu tu iliyowekwa na haohao CCM.
Dhamana iliyopo sasa ni kwa jeshi na vyombo vingine vya ulinzi kuhakikisha kipindi hiki kinapita kwa utulivu na amani bila ya kukosa haki.Hili linalofanywa na tume ya uchaguzi iliyowahusishamakada wa CCM watupu na sasa inadaiwa kuhusishwa pia vyombo vya uslama vya Taifa, hayo yanafanywa na CCM,wasimamizi wa Tume ya uchaguzi Pemba tayari wameshagundulika ni kutoka usalama wa Taifa,unategemea nini ? Maana hawa wamefanywa watumwa na CCM na sio serikali.
Kitakacho tokea Pemba kama tume ikijitia upofu sio kiachwe Pemba peke yake kiwepo Tanzania nzima kama alivyosema mgombea mmoja wa Uraisi, Wapemba au Zanzibar hawaidai haki hio kwa ajili yao bali kwa ajili ya Tanzania nzima, tusika na kuukalia uchumi kama alivyosema Mwalimu Nyerere,uchumi mnaukalia, hapa ni umoja kwa Watanzania wote wapenda amani, utulivu na haki, tuungane na Wapemba ikiwa Tume ya CCM haitasikia madai, kilichotokea Pemba kimetokea Tanzania nzima
Kinuke pemba kwamba ndo kinuke nchi nzima?? Wewee ulisikia wapi???
Unaweza kuchoma tairi hapo Mwenye junction?????