Pemba Mwisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pemba Mwisho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Sep 21, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa nini tunaiandalia mabaya Pemba?
  Salim Said Salim
  NI saa 2 za asubuhi. Gari iliyonichukua kutoka mji mdogo wa Chake inakaribia kufika Kijiji cha Kiuyu Minungwini, Jimbo la Ole, Kaskazini Pemba, umbali wa kilomita 25. Katika kijiji hiki na vijiji jirani lilikuwa liendelee zoezi la uandikishaji wapiga kura lililosimamishwa mwezi uliopita kutokana na watu kususia kujiandikisha na kuzuia wengine wasifanye hivyo. Sababu ni madai kuwa vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi vinatolewa kwa ubaguzi na maelfu wamenyimwa ili wasiweze kuandikishwa kupiga kura. Tukiwa kama mita 300 kufika kituoni, Shule ya Msingi ya Kiuyu Minungwini, naona askari polisi na wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Magereza, KMKM, Jeshi la Kujenga Uchumi na Magereza) wametanda kila pembe.
  Maofisa wa KMKM walikuwa ndani ya vyumba vya uandikishaji waking'ara na sare zao za rangi nyeupe kama vile wapo kwenye boti baharini.
  Hapo tena liliingia kwa mwendo wa kasi gari lenye askari wapatao 10 wa FFU waliobeba bunduki na mabomu ya machozi na bendera nyekundu ikipepea. Niliona makundi mawili ya watu, moja la wanaume na jingine la kina mama. Wanaume walikuwa wanabishana na askari polisi na wanawake walikuwa wanaimba "Haudundwi wala hauchezwi…utatiwa kwapani", yaani hapana uandikishaji wapiga kura na hakuna zoezi kama hilo litakaloruhusiwa kuendelea.
  Niliposogea niligundua askari wanawataka watu wapatao 300 waliokuwepo hapo wakae mbali na kituo kama hawapo tayari kwenda kujiandikisha.
  Lakini kwa pamoja walisema hilo haliwezekani kwa vile wamefika kudai haki ya kupiga kura na kwa kuwa wamenyimwa vitambulisho hawaandikishwi. Lakini wenzao waliosema walipewa kwa vile ni CCM, hawataandikishwa na atayekwenda chumba cha uandikishaji watamshughulikia.
  Mara akachomoza kijana wa kama miaka 25 hivi. Alipokuwa akielekea chumba cha uandikishaji, kina mama walimrukia na kumuangusha chini na kuimba "Haudundwi wala hauchezwi..utatiwa kwapani." Polisi walipoingilia kati kumsaidia walijikuta wanapambana na vijana waliokuwa wanawaambia wakipatiwa wote vitambulisho na haki ya kupiga kura hapatakuwa na ugomvi.
  Hapo tena vijana wa FFU waliteremka na kutanda kila pembe huku wakielekeza mtutu wa bunduki kwa watu waliokuwepo hapo.
  Kauli zilizosikika hapo, baadhi yao kwa wazee na jamaa mmoja ambaye ni mgonjwa wa akili zilikuwa kielelezo cha watu walioamua kwa pamoja kudai kwa gharama yoyote ile haki ya kupiga kura. Kwa bahati nzuri Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Yahya Hemed, alifika na kuhakikisha askari hawatumii nguvu za ziada na kusisitiza hapigwi mtu wala hayalipuliwi mabomu ya machozi, lakini polisi haitavumilia fujo.
  Niliwasogelea kina mama kuwauliza kama walifanya juhudi kupata vitambulisho na mmoja Siti Ali Hamad, aliniambia ameshauza kuku wake wote kwenda ofisi ya Msajili wa Vitambulisho na amekuwa akizungushwa, ‘njoo kesho ...njoo kesho,' wakati vijana wa CCM na watu ambao sura zao hajawahi kuziona Pemba wanapewa vitambulisho.
  Mwingine alinionyesha hati za kupiga kura za chaguzi sita, tangu za mfumo wa chama kimoja, lakini bado hapewi haki ya kujiandikisha kwa uchaguzi wa mwaka 2010.
  Nilipomueleza Mkuu wa Wilaya, Omar Khamis Othman, malalamiko haya, aliniambia si kweli na kuwa yeye binafsi alimsaidia mtu asiyemjua karibu shilingi 150,000 ili apate kitambulisho na wale wote wasiokuwa na vitambulisho hawajavitaka.
  Hali nayo ilikuwa mbaya katika kituo cha Kambini na Kiuyu Mjini. Hapo Kambini walikuwepo vijana zaidi ya 150 na kila niliyemuuliza aliniambia amefika kwa sheha zaidi ya mara tatu na baadhi yao kutakiwa waende na wazee wao na walipofanya hivyo pia haikuwasaidia.
  Nilipomuona sheha wa Kambini, Ali Said Ali, na kumueleza malalamiko ya vijana hao alisema hakuna hata mmoja aliyefika kwake na kukataa kumpa fomu za kitambulisho na kutaka nimuonyeshe anayedai hivyo.
  Niliporudi kuwaleza wale vijana, wasichana watatu walijitokeza na nikaenda nao mpaka alipokuwepo sheha.
  Wasichana hao Raya Haji (19) Asha Omar Hamad (20) na Asha Msellem Hamad (20) walikubaliana twende pamoja kwa sheha na hapo kila mmoja alimueleza namna alivyofika kwake zaidi ya mara tatu na kufukuzwa kama mbwa.
  Palizuka mabishano makali kati ya sheha na wale wasichana na nikaacha kazi ya uandishi wa habari na kuwa msuluhishi.
  Siku ya pili mambo yalikuwa mazito zaidi. Wakati makarani wa uandikishaji wakisinzia kwa vile hakuna aliyeingia kujiandikisha, polisi walipeleka gari la maji ya kuwasha Kiuyu. Gari lilipokaribia kina mama walilipokea kwa furaha wakiwaambia askari: "Njooni mtuoshe kwani sisi ni wachafu na siku nyingi hatujaoga kwa vile maji ni ya shida."
  Kijana mmoja wa kiume alizusha kichekesho aliposema: "Mkimaliza kutuosha sisi na hayo maji mazuri yenye uturi lipelekeni hilo gari Bagamoyo ili na ndugu zetu wa huko wapate raha hii mtakayotupa."
  Hayo yalikuwa maneno ya dhihaka, lakini yalibeba ujumbe mzito. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikiliza!
  Kwa muhtasari safari ya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010 Visiwani inapitia dhoruba kali na kutoa dalili za kuwapo vurugu zaidi usoni.
  Uchomaji nyumba na watu kupigwa majumbani na vitisho walivyopewa waandishi wa habari ni ushahidi tosha kuwa hapa lipo tatizo . Nalo linatokana na watu kukosa haki ya kupiga kura na sababu kubwa ni madai ya kutopewa vitambulisho.
  Hali hii ni mbaya kisiwani Pemba, ambapo kwa siku nzima hata mtu mmoja haandikishwi na sura kama hiyo imejitokeza Kaskazini Unguja ambapo pia zoezi linaendelea.
  Kinachoshangaza ni kuona takwimu zinazotolewa zinaonyesha watu wengi wamepatiwa vitambulisho, hasa Pemba, lakini maelfu wanasema si kweli. Suala ni hao waliopata ni nani na wametoka wapi? Wapo wanaosema labda ni wanga na vibwengo.
  Njia nzuri ya kuupata ukweli ni kwa Idara ya Vitambulisho kutoa orodha ya majina na anwani za waliopewa vitambulisho ili ukweli ujulikane, kwa vile upo wasi wasi kuwa wapo waliopata kitambulisho zaidi ya kimoja ili waweze kupiga kura zaidi ya moja, kama inavyosemekana kutokea chaguzi zilizopita au kupewa wale wanaoitwa wapiga kura mamluki walioletwa kutoka Bara (nani kawaleta kama kweli waliletwa, sijui).
  Nilichokiona Pemba ni mateso ya raia. Kuipata haki ya kupiga kura ni kazi pevu. Wapo waliotumia zaidi ya shilingi 50,000 kufanya safari za kutafuta kitambulisho na kukikosa.
  Kisichokuwa na ubishi ni kwamba zoezi la uandikishaji wapiga kura Zanzibar lina matatizo na limezusha hisia za kuwepo mizenge ya uchaguzi. Hali hii haitoi sura nzuri kwa huko tunakokwenda. Rais Amani Abeid Karume alisema mara nyingi kila Mzanzibari atapata kitambulisho na haki ya kupiga kura, lakini hili halionekani kufanyika,Raisi anaonekana ni muongo.
  Ninarudia kuwaomba Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kuhakikisha kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania, awe wa Bara au Visiwani.
  Ni vizuri wakapewa haki hiyo kwani kuwanyima, hasa Wapemba kwa vile ni ngome ya upinzani kama inavyoonekana, kutatuletea balaa, tutakuja kujijutia. Tumeshapata balaa na maafa ya kutosha kutokana na uchaguzi. Sasa tuwasaidie wananchi wetu kupumua kwa kuwa na uchaguzi huru na wa haki na si wa vitendo kutofautiana na kauli zetu
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhhhhhh.
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hii ndio ile kitu Pres Obama aliizungumzia aliposema "Our cherished rights of liberty and equality depend on the active participation of an awakened electorate."


  Pemba walishaamka siku nyiiiiingiiiiiii. Hebu angalieni mfano wa kuingwa hu; kila Mpemba anasimamia haki yake...kila Mpemba...Wanawake, Wanaume mpaka Raya Haji mwenye umri wa miaka 19 naye anajua ni vipi apiganie haki yake.

  Sheha alipoleta za kuleta, wakamfuatwa kule aliko kumsuta...huku ndio kumkoa nyani..Pemba Style.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hongereni Wapemba. nOBODY, BUT YOURSELVES WILL LIBERATE YOUR COUNTRY.
   
 5. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  wapembe ni wenyekujua haki zao!!!!
  obama says "hope over fear,unity of purpose over conflict and discord". "To those who cling to power through corruption and deceit and the silencing of dissent,know that you are on the wrong side of history,but that we will extend a hand if you are willing to unclench your fist."
  That all are equal,all are free and all deserve a chance to pursue their full measure of happiness.
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hayo ni madogo sana kuna mengi yanafichwa.

  Maskini Tanzania inayojiita nchi ya amani.
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Yanayotokea leo huko Pemba ni aibu kubwa kwa Taifa hili na mustakabali wa amani ya nchi hii.
  Wapemba tunaowajua ni wapole,wao maneno tu ya utani, leo hii hata wanawake wanapandishwa munkari ,wanageuzwa kuwa wakali kwa kudai haki zao.
  Karume na JK lazima wakae pamoja na kusawazisha jambo hili kabla damu hajaanza kumwagika
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280

  amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga...
  sidhani kama yafaa sana njia hiyo itumike kuleta amani wakati njia za kidiplomasia zipo.
  serikali ya ccm iache uroho wa madaraka.
  amani ya pemba inaharibiwa na chama tawala ccm
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi naona ni bora jumuiya za kimataifa ziliangalie hili na ikiwezekana kuzuilia misaada mpaka haki itendeke
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jumuiya hizo ni part and parcel of the whole problem, wao wemetoa hela za wapiga kura wao kwa ajili ya kuimarisha demokrasia hapa kwetu. Demokrasia inachezewa kwa hela za wafadhili hawawi serious na kitu hicho something is seriously wrong with them.

  Angalia kuwa multinationals nyingi zinapenda statu quo iendelee any change kwao ni balaa hivyo na wao wanapuliza kwa mbali bila wananchi kujua.

  Natamani maeneo mengine yangekuwa conscious kama Pemba, Tarime etc hamna pilau, kanga wala kofia. Huko ni siasa za kweli tu.
   
 11. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Watanzania wakilijua hilo, wataanza vita ya kukataa ufadhili. Utashangaa misaada ya kibinadamu itakavyomiminika watu wakianza kuzichapa. Dalili zote zinaonekana
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kwa rasilimali zetu hatuhitaji kabisa ufadhili, pesa tunayo tena nyingi tu ya kutosha kila kitu. Misaada ya kibinadamu kwa kipi cha ajabu hakuna tetemeko wala mafuriko kuhitaji misaada ya kibinadamu.

  Misaada yote ni ya kisiasa UNDP kugharimia uchaguzi, so and so kugharimia daftari la kudumu, so an so dola kadhaa kwenda kwenye Tume za uchaguzi sasa what country is this begging from XYZ to enable your own people elect you.

  Pamoja na vurugu wanasema kidogo tu halafu aliyetembeza bakuli eti anavimba msituingilie na hao the so called wafadhili wanakaa kimya, nadhani wao kama watoa fedha walitakiwa kuonesha hasira zao kwa hali ya juu sana na kusimamisha kila kitu kama njia ya kuelekea kwenye demokrasia inafungwa bila sababu.
   
Loading...