Pemba: Moto wa Petrol wasababisha Vifo vya watu watatu

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,773
3,471
Salaam waungwana,

Jana usiku petrol ilisababisha moto na kuuwa watu watatu ambae ni baba, mama na mtoto, moto huo huko katika kijiji cha Shumba Mjini Wilaya ya Micheweni Pemba.

Petrol hiyo ambayo alikuja nayo baba mwenye nyumba wakati akiwa akitoka agoni (kambi ya wavuvi) huko Kenya.

Habari hizi sikuzipata kwa usahihi maana hata mimi nimetupiwa tu picha kupitia WhatsApp.

465873a354cb8a95b9810f8e6c5c6b64.jpg

17361696_10155927683867195_365369375305771499_n.jpg
17353177_10155927683947195_5821707316418556300_n.jpg


=======

PICHA: Moto waua watu watatu wa familia moja Pemba
MAMIA ya wananchi leo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali na Afisa Mdhamini afisi ya Makamu wa pili wa rais Pemba, Ali Salim Mata kwenye mazishi ya watu watatu wa familia moja, akiwemo mtoto wa miaka sita, waliofariki kutokana na nyumba yao kuteketea kwa moto, uliosababishwa na mafuta ya petroli shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba

pbam2.jpg

vitu vilivyoungua na kusalimika kwa moto vya marehemu Makame Omar Mata (60) baada ya nyumba yake kuteketea kwa moto na watu watatu akiwemo mtoto wa miaka sita walifariki shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
pbam.jpg

NYUMBA vya marehemu Makame Omar Mata (60), ilioteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu watatu, akiwemo baba, mama na mtoto wa miaka sita, ajali hiyo iliotokezea shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ilitokana na mafuta ya petroli, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
pba-m.jpg

NYUMBA vya marehemu Makame Omar Mata (60), ilioteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu watatu, akiwemo baba, mama na mtoto wa miaka sita, ajali hiyo iliotokezea shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ilitokana na mafuta ya petroli, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
pmb-m.jpg

BAADHI vitu vilivyoungua na kusalimika kwa moto vya marehemu Makame Omar Mata (60) baada ya nyumba yake kuteketea kwa moto na watu watatu akiwemo mtoto wa miaka sita walifariki shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
pba-m3.jpg

Makame (25) alieungua moto, kwenye ajali ya moto uliotokezea ndani ya nyumba yao na kuuwa watu watatu, akiwa kwenye hospitali ya Micheweni akipatiwa matibabu, baada ya nyumba yao kuteketea yote, moto huo ulisababishwa na mafuta ya petroli, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
pba-m2.jpg

OMAR Makame Omar (19), alisalimika na kuungua kwa moto, ulioteketeza nyumba yao na mama yake, ndugu yake wa miaka sita na baba yake mzazi kufariki, kutokana na kuripuka kwa mafuta ya petrol, shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba, (Picha na Marzuku Khamis, Pemba).
pbam4.jpg

SHEHA wa shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Rahma Mohamed Shaame akizungumza na waandishi wa habari, juu ya tukio la kufariki watu watatu kwenye shehia yake, baada ya nyumba yao kuungua moto, iliosababishwa na mafuta ya petroli, (Picha na Marzuku Khamis, Pemba).
pbam3.jpg

NYUMBA vya marehemu Makame Omar Mata (60), ilioteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu watatu, akiwemo baba, mama na mtoto wa miaka sita, ajali hiyo iliotokezea shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ilitokana na mafuta ya petroli, (Picha na Haji Nassor)
pba-m5.jpg

MAMIA ya wananchi wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali na Afisa Mdhamini afisi ya Makamu wa pili wa rais Pemba, Ali Salim Mata kwenye mazishi ya watu watatu wa familia moja, akiwemo mtoto wa miaka sita, waliofariki kutokana na nyumba yao kuteketea kwa moto, uliosababishwa na mafuta ya petroli, shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 
Kule ambako mioto ingefaa ikafanye kazi yake barabara haiendi kufanya hivyo na badala yake inaenda kufanya kazi ambako hakustahili kabisa!!!

RIP marehemu wote.
 
chanzo cha ajali kimeshajulikana ila watu wa uswahili tunajijua
Utaskia '' Katupiwa jini vo''
 
Kule ambako mioto ingefaa ikafanye kazi yake barabara haiendi kufanya hivyo na badala yake inaenda kufanya kazi ambako hakustahili kabisa!!!

RIP marehemu wote.
Unamaanisha nini?
 
Unamaanisha nini?
Ninachomaanisha ni kwamba; nyumba yetu ipo karibu na pori lisiloingilika kutokana na kujaa mafisi, nguruwe, minyani na mapanya buku kiasi kwamba hatuna amani! Hata tukilima; mazao hatuyaoni manake yanaaza kufungiwa kazi tangu yakiwa machanga!

Moto ungekuwa unaenda kuteketeza hayo mapori na mafisi yaliyomo ndani yake ili hatimae tuishi kwa amani na tuone matunda ya jasho letu!

Una lingine?!
 
Back
Top Bottom