Zanzibar 2020 Pemba: Hitimisho la Awamu ya Pili ya Kampeni za Mgombea Urais, Maalim Seif (ACT Wazalendo)

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
609
1,540
71E98A44-9A2A-43CD-8A70-98202A7B919C.jpeg

4B11F3B6-FB07-4F98-9E9C-4A7A310B982D.jpeg

FD0B5FAB-9C9A-4F2F-9B26-1CE1C73E1115.jpeg

2BBAB65E-800C-4097-82EC-66A8B75A89CE.jpeg

5EFCEBDD-D154-46E1-9FD0-8343F9E43148.jpeg


Leo tarehe 02/10/2020 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad akamilisha mkutano wake wa mwisho wa kampeni kwa awamu ya pili kisiwani Pemba.

Maalim Seif ameanza siku yake kwa kuhudhuria Maziko ya Mwalim Muhidin Mohd Muhidin aliefariki jana usiku, ambae aliwahi kuwa Muwakilishi wa jimbo la Mtambile kwa tiketi ya Chama cha CUF.

Maalim Seif amekamilisha Mkutano wake wa hadhara kwa kukutana na Wananchi wa jimbo la Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akizungumza na Wananchi hao Maalim alisema suala la kwanza nikuhakikisha anaufungua uchumi wa Zanzibar kwa kuielekea sekta ya mafuta na gesi asilia, akielezea mipango hio Maalim amesema;

‘’Tayari tumeshafanya mazungumzo na mashirika makubwa ya uchimbaji mafuta na gesi asilia, jambo pekee lililobakia nikiwa Rais ni kusaini mikataba na kuja kuanza kazi, hivyo itakapofikia mwaka 2021 zoezi la uchimbaji litaanza rasmi, na niukweli usiofichika kwamba rasilimali hii italeta mafanikio makubwa kwa taifa letu”.

Katika kuonesha fursa nyengine ya kiuchumi Maalim Seif amesema kuna fursa kubwa kwa Zanzibar kuwa Kituo kikuu cha mawasiliano ambapo Mataifa mbali mbali yanaweza kupitisha bidhaa zao kama kutakuwa na bandari kubwa na uwanja wa ndege wa kisasa, lakini pia hata kuweka minara mikubwa ya kimawasiliano, jambo ambalo litaleta fursa za ajira sambamba na kuingiza kodi katika nchi kwani itakuwa ni kitovu cha biashara kwa Afrika na Dunia kwa ujumla.

Maalim Seif amesema, kwakupitia bandari kubwa itakayojengwa Zanzibar itakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya ajira elfu hamsini jambo ambalo litapunguza kwa asilimia kubwa tatizo la ajira ndani ya visiwa vya Zanzibar.

Kuhusu Kilimo Maalim Seif amesema karafuu ni zao kubwa sana Zanzibar, na karafuu za Zanzibar zinathamani kubwa duniani hivyo atahakikisha anailinda thamani ya zao hilo ili wananchi na Taifa lipate mafanikio kupitia zao lao, na wananchi watakuwa na uhuru wa kuuza wanapotaka.

Maalim Seif pia amezungumzia umuhimu wa masuala ya kijamii kwakugusia maeneo kadhaa ikiwemo:-

AFYA, Maalim ameahidi katika Serikali yake atahakikisha anaboresha huduma za afya ikiwemo majengo, vifaa vya vipimo, madawa na madaktari wenye uwezo, lakini zaidi amesema huduma ya afya itakuwa bure kwa kila raia wa Zanzibar.

ELIMU, Maalim amesema kila mwaka Zanzibar inakuja na matokeo mabaya katika mitihani, na hii nikutokana na sera dhaifu za elimu chini ya Serikali ya Mapinduzi.

Katika kuleta suluhisho ya tatizo hilo Maalim amesema atahakikisha Wanafunzi wanasoma katika majengo yenye ubora, Madawati kwaajili ya kukalia,vitabu vya kujisomea, vitendea kazi vya Waalimu, Mitaala yenye kufahamika na Waalimu wenye weledi pamoja na maslahi mazuri ya mshahara wa Waalimu hao.

Maalim amesema baada ya miezi mitatu ya Utawala wake atafanya kongamano kubwa la masuala ya kielimu Zanzibar kwa kuwajumuisha wadau wa elimu kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuleta ufumbuzi wa masuala ya elimu Zanzibar.

Katika suala hilo la elimu Maalim alimalizia kwa kusema atahakikisha Mwanafunzi wa Kizanzibari atasoma kuanzia elimu ya awali mpaka chuo kikuu bure, pamoja na kufuta madeni yote kwa wanafunzi wote wanaodaiwa mikopo ya elimu ya juu.

Katika suala la Utawala bora Maalim amesema atahakikisha Katika utawala wake hakuna raia atakaeonewa, kila raia atapata haki sawa na mwengine.

Na kuhusu usawa wa visiwa vya Zanzibar Maalim amesema shughuli ya kimaendeleo itakayofanyika kisiwa cha Unguja basi itafanyika pia na kisiwa cha Pemba ili kuleta uwiano ulio sawa.

Mwisho Maalim Seif amemalizia kwakuwataka Wazanzibari wahakikishe wanamchagua katika uchaguzi mkuu huu, na wajiandae kupata faraja na Maisha yenye Neema na furaha chini ya Serikali itakayoongozwa na chama cha ACT Wazalendo.

Abeid Kamis Bakar
/Afisa Habari na Uenezi
ACT Wazalendo Zanzibar.
 
Zanzibar Maailm mwaka huu atashindwa vibaya sana,maana wazanzibar washamjua kuwa ni msanii hawatompa kura tena.
kura zote ni kwa Hussein Mwinyi.
 
Zanzibar Maailm mwaka huu atashindwa vibaya sana,maana wazanzibar washamjua kuwa ni msanii hawatompa kura tena.
kura zote ni kwa Hussein Mwinyi.
Labda kwa goli la mkono na nguvu ya policcm.
Lakini sio Wazanzibari Sisi hasa vijana wa Leo new generation hii hatukubali mpaka kieleweke kupata nchi yetu au lengine
 
Back
Top Bottom