Pemba Chini ya CCM kuneemeka au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,645
119,246
Wanabodi,
Huu ni uzi kuhusu kitu kinachoitwa "trend Reading" kwa jina la Kiswahili ni "kusoma mielekeo". Katika uzi huu, nazungumzia mielekeo ya Kisiwa cha Pemba, kilichokuwa ngome kuu ya CUF, baada ya lile igizo la uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar kwa CUF kususa, CUF wamefanya a grave mistake!, kosa la kifo!, kamwe hawatarejea tena kuimiliki hii ngome yake ya Pembe!, this is the end of CUF!, na hili litathibitishwa uchaguzi Mkuu wa 2020!, CUF haitapata kitu Zanzibar, haitapata kitu Pemba, it's the end of iliyokuwa CUF!.

Jee mielekeo ni nini? . Mielekeo ni mambo yatakayokuja kutokea ambayo yamesababishwa na mambo yaliyotangulia kutokea kabla na mambo yanayotokea sasa, ili kujua mambo yatakayokuja kutokea siku zijazo. Kwa kifupi hii ndio maana halisi ya somo la Historia ambayo ni " the study of the past in relation to the present to determine the future". Kujua mambo ya kale na kuyahusianisha na mambo ya sasa ili kujua mambo yajayo.

Kwa kisiwa cha Pemba, hii ndio ilikuwa ngome kuu ya Chama cha CUF, ambapo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, Pemba yote imekuwa ikishikiliwa na chama cha Wananchi CUF katika nafasi zote za Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Uwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, na hadi sasa, wabunge wote wa Pemba ni kutoka Chama cha Wananchi CUF, lakini kufuatia Chama cha CUF kususia Uchaguzi, Chama cha Mapinduzi, kimeiteka ngome kuu ya CUF na kuikalia kufuatia ushindi wa kishindo uliopatikana na kutokana na igizo la uchaguzi huo wa marudio. CCM haitafanya makosa, kama kimada anapomdaka mume wa mtu, atafanya manjonjo ili mume asikumbuke kwake!.

Japo CUF kina wabunge ndani ya bunge la JMT, wabunge hawa, hawana impact yoyote kule Pemba kwa sababu Bunge la JMT, ni Bunge jina tuu, kuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la Muungano jina tuu, kiukweli, Bunge la JMT, sio Bunge la Muungano, ni Bunge la Iliyokuwa Tanganyika, ila linashughulikia na Mambo yote ya Muungano kwa huku Tanzania Bara Tuu!. Hivyo Bunge ni la Bara, ila limevaa koti tuu la Muungano, hivyo Wabunge wa CUF ndani ya Bunge, hawana impact yoyote kwa Pemba, kwa sababu Bunge la JMT ni bunge jina tuu la JMT ila kiuhalisia ni Bunge la Bara hivyo sio Bunge la Muungano.

Kuthibitisha kuwa Bunge letu sio bunge la Muungano, sheria zote za muungano zinazotungwa na Bunge 'Bara' hazina mamlaka ya kutumika Zanzibar, hadi sheria hizo ziridhiwe na Baraza la Wawakilishi, hii inamaanisha BLW ndiocho supreme organ ya utungaji wa sheria Zanzibar, kituo ambacho wajuvi wa mambo ya katiba, wanakiona kama ni kichekesho, yaani kikatiba, Zanzibar ni sehemu ya JMT, na katiba ya JMT ndio the supreme, na Bunge la JMT ndio supreme organ ya utungaji wa sheria, ambapo Spika wa Bunge la JMT was supposed to be the supreme Speaker, na sheria zikitungwa na Bunge, lazima kwanza ziridhiwe na rais wa JMT (accent) ili ziwe sheria na kuanza kutumika ndani ya JMT, lakini eti sheria hizo, haziwezi kutumika sehemu fulani ya JMT, hadi BLW liridhie, kati ya Bunge la JMT na BLW, nani zaidi?!, yaani sheria imepitishwa na Bunge la JMT, na kuridhiwa na rais wa JMT, itumike ndani ya JMT, halafu haiwezi kutumika eneo fulani hadi iridhiwe na mdudu fulani anayeitwa BLW, hiki ni kichekesho na dharau kubwa kwa mamlaka ya rais wa JMT. No wonder, Rais wetu wa JMT, Waziri wetu Mkuu wa JMT, Spika wetu wa Bunge la JMT, Jaji wetu Mkuu wa Mahakama Kuu ya JMT, they are all nobodies kwenye set up ya Zanzibar, kwa sababu ndani ya Muungano, Zanzibar nayo inajiita ni nchi, ina rais wake, bunge lake, na mahakama yake!.

Sasa nikirudi kwenye hatima ya Kisiwa cha Pemba chini ya CCM, Pemba itahesabiwa alikuwa ni yule mwana mpotevu ambaye alipotea toka kwa baba yake, na sasa amerejea kwenye mikono ya baba yake!, hivyo atafanyiwa karamu kubwa. Atapewa kila anachokitaka na kuletewa hata kila asichokitaka. ataletewa tuu ali mradi kitaonekana kina mfaa!, atadekezwa kuhakikisha uchaguzi wa 2020, CUF haipati kitu.

Jee Pemba ya CCM, itakuwa ni Pemba ya raha tele?, ulinzi tele?, maendeleo tele?, uwekezaji tele?, ajira tele?, na itapatiwa preferential treatment kwenye kila kitu?, ili kujenga imani kwa Wapemba kuishabikia CUF, ilikuwa ni makosa, ili itakapofika 2020, wakati wa kuamua tena, wananchi wa kisiwa cha Pemba wapate fursa ya kuipima hii miaka 5 ya CCM Pemba, na kuilinganisha na miaka 20 ya CUF Pemba, nani amefanya nini?!. Kwa vile 2020, Wapemba watapata fursa nyingine ya kuamua ama CCM ama CUF, then nawahakikishia kipindi hiki, CCM Zanzibar, haitafanya makosa tena, nguvu zote itazihamishia Pemba, ili 2020, Wapemba wenyewe kwa ridhaa yao, wataivote out CUF katika uchaguzi huru na wa haki, na sio kupitia tena kwenye igizo la uchaguzi!.

Au kwa vile Pemba walikuwa wanaichagua CUF, kwa imani, na sasa CCM imeishika Pemba kimabavu kupitia lile igizo la uchaguzi wa marejeo, hivyo sasa Pemba watajuta kuichagua CUF, hivyo sasa Pemba chini ya CCM, cha moto watakipa, na kujuta kuichagua CUF, hadi wajisikie walifanya makosa kuitegemea CUF, kuliko kuichagua tena CCM 2020, ni heri wakairudisha CUF yao waliyoizoea!. Jee hii miaka 5 ya CCM Pemba, itakuwa ni miaka ya neema kwa Wapemba au majuto?. Kwa maoni yangu, uchaguzi wa mwaka 2020, CUF itavuna majuto ya kususia uchaguzi, ukisusa sie twala!, CCM inakula na haitaachia!.

Namalizia kwa lile swali la msingi, "Jee Pemba Chini ya CCM, Itaneemeka Au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!".

Nawatakia Ijumaa Kuu Njema.

Paskali
 
Wanabodi,
Huu ni uzi kuhusu kitu kinachoitwa "trend Reading" kwa jina la Kiswahili ni "kusoma mielekeo". Katika uzi huu, nazungumzia mielekeo ya Kisiwa cha Pemba, baada ya lile igizo la uchaguzi wa Marejeo wa Zanzibar.

Jee mielekeo ni nini? . Mielekeo ni mambo yatakayokuja kutokea ambayo yamesababishwa na mambo yaliyotangulia kutokea kabla na mambo yanayotokea sasa, ili kujua mambo yatakayokuja kutokea siku zijazo. Kwa kifupi hii ndio maana halisi ya somo la Historia ambayo ni " the study of the past in relation to the present to determine the future". Kujua mambo ya kale na kuyahusianisha na mambo ya sasa ili kujua mambo yajayo.

Kwa kisiwa cha Pemba, hii ndio ilikuwa ngome kuu ya Chama cha CUF, ambapo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, Pemba yote imekuwa ikishikiliwa na chama cha Wananchi CUF katika nafasi zote za Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Uwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, na hadi sasa, wabunge wote wa Pemba ni kutoka Chama cha Wananchi CUF, lakini kufuatia Chama cha CUF kususia Uchaguzi, Chama cha Mapinduzi, kimeiteka ngome kuu ya CUF na kuikalia kufuatia ushindi wa kishindo uliopatikana na kutokana na igizo la uchaguzi huo wa marudio.

Japo CUF kina wabunge ndani ya bunge la JMT, wabunge hawa, hawana impact yoyote kule Pemba kwa sababu Bunge la JMT, ni Bunge jina tuu, kuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la Muungano jina tuu, kiukweli, Bunge la JMT, sio Bunge la Muungano, ni Bunge la Iliyokuwa Tanganyika, ila linashughulikia na Mambo yote ya Muungano kwa huku Tanzania Bara Tuu!. Hivyo Bunge ni la Bara, ila limevaa koti tuu la Muungano, hivyo Wabunge wa CUF ndani ya Bunge, hawana impact yoyote kwa Pemba, kwa sababu Bunge la JMT ni bunge jina tuu la JMT ila kiuhalisia ni Bunge la Bara hivyo sio Bunge la Muungano.

Kuthibitisha kuwa Bunge letu sio bunge la Muungano, sheria zote za muungano zinazotungwa na Bunge 'Bara' hazina mamlaka ya kutumika Zanzibar, hadi sheria hizo ziridhiwe na Baraza la Wawakilishi, hii inamaanisha BLW ndiocho supreme organ ya utungaji wa sheria Zanzibar, kituo ambacho wajuvi wa mambo ya katiba, wanakiona kama ni kichekesho, yaani kikatiba, Zanzibar ni sehemu ya JMT, na katiba ya JMT ndio the supreme, na Bunge la JMT ndio supreme organ ya utungaji wa sheria, ambapo Spika wa Bunge la JMT was supposed to be the supreme Speaker, na sheria zikitungwa na Bunge, lazima kwanza ziridhiwe na rais wa JMT (accent) ili ziwe sheria na kuanza kutumika ndani ya JMT, lakini eti sheria hizo, haziwezi kutumika sehemu fulani ya JMT, hadi BLW liridhie, kati ya Bunge la JMT na BLW, nani zaidi?!, yaani sheria imepitishwa na Bunge la JMT, na kuridhiwa na rais wa JMT, itumike ndani ya JMT, halafu haiwezi kutumika eneo fulani hadi iridhiwe na mdudu fulani anayeitwa BLW, hiki ni kichekesho na dharau kubwa kwa mamlaka ya rais wa JMT. No wonder, Rais wetu wa JMT, Waziri wetu Mkuu wa JMT, Spika wetu wa Bunge la JMT, Jaji wetu Mkuu wa Mahakama Kuu ya JMT, they are all nobodies kwenye set up ya Zanzibar, kwa sababu ndani ya Muungano, Zanzibar nayo inajiita ni nchi, ina rais wake, bunge lake, na mahakama yake!.

Sasa nikirudi kwenye hatima ya Kisiwa cha Pemba chini ya CCM, Pemba itahesabiwa alikuwa ni yule mwana mpotevu ambaye alipotea toka kwa baba yake, na sasa amerejea kwenye mikono ya baba yake!, hivyo atafanyiwa karamu kubwa. Atapewa kila anachokitaka na kuletewa hata kila sichokitaka ali muadi kitaonekana kina mfaa!.

Jee Pemba ya CCM, itakuwa ni Pemba ya Raha tele?, ulinzi tele?, maendeleo tele?, uwekezaji tele?, ajira tele?, na itapatiwa preferential treatment kwenye kila kitu?, ili kujenga imani kwa Wapemba kuishabikia CUF, ilikuwa ni makosa, ili itakapofika 2020, wakati wa kuamua tena, wananchi wa kisiwa cha pemba wapate fursa ya kuipima hii miaka 5 ya CCM Pemba, na kuilinganisha na miaka 20 ya CUF Pemba, nani amefanya nini?!. Kwa vile 2020, Wapemba watapata fursa nyingine ya kuamua ama CCM ama CUF, then nawahakikishia kipindi hiki, CCM Zanzibar, haitafanya makosa tena, nguvu zote itazihamishia Pemba, ili 2020, Wapemba wenyewe kwa ridhaa yao, wataivote out CUF katika uchaguzi huru na wa haki, na sio kupitia tena kwenye igizo la uchaguzi.

Au kwa vile Pemba walikuwa wanaichagua CUF, na sasa CCM imeishika kimabavu kupitia lile igizo la uchaguzi, hivyo sasa Pemba watajuta kuichagua CUF, hivyo sasa Pemba chini ya CCM, cha moto watakipa, na kujuta kuichagua CUF, hadi wajisikie walifanya makosa kuitegemea CUF, kuliko kuichagua tena CCM 2020, ni heri wakairudisha CUF yao waliyoizoea!. Jee hii miaka 5 ya CCM Pemba, itakuwa ni miaka ya neema kwa Wapemba au majuto?.

Namalizia kwa lile swali la msingi, "Jee Pemba Chini ya CCM, Itaneemeka Au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!".

Nawatakia Ijumaa Kuu Njema.

Pasco

MATATIZO YAKO TANGANYIKA , ILI MTU KAMA WEWE PASCO USISHUGHULIKE NA MATATIZO YA TANGANYIKA NDIO NYERERE AKAIVAMIA ZANZIBAR . KILA WAKATI KUTAZUSHWA KILA AINA YA MATATIZO ZANZIBAR ILI KUINUSURU TANGANYIKA:

HIVI SASA WBUNGE WABUNGE HAWALIPWA MISHAHARA YAO , PIA WANAJESHI HAWAJALIPWA , KUZUIA MACHAFUKO , NI KUPELEKA JESHI ZAIDI HUKO PEMBA PAMOJA NA POLISI . HII NDIO DAWA

WAZNZ MILELE HAWATOWEZA KUJINASUA KATIKA HALI HII MPAKA WAANZE KUWAAMSHA WATANGANYIKA KAMA WEWE .

AU WEWE NI MTU WA USALAMA ??? UMETUMWA NA UNALIPWA LUMUMBA ??
 
Sasa hivi ndio wakati muafaka wa kupitisha mambo muhimu na kuondoa ukakasi na vizingiti vya mambo/ sheria ambazo zingeamuliwa na Bunge la JMT na kukwama kwenye Baraza la wawakilishi.
Sasa hivi sheria za bara zitapita kirahisi Zanzibar kwa maslahi ya dola ya JMT.
 
Hata iweje, hao Wawakilishi toka CCM hawatapewa support yoyote kule Pemba. Wapemba wanaichukia CCM, Wapemba wako tayari washinde na njaa kuliko kuimba nyimbo za CCM huku wakishibishwa kwa mikate na maziwa. Hao Wawakilishi watajutia maamuzi ya Jecha kufuta uchaguzi halali uliowapa madaraka wawakilishi halali toka CUF na hatimaye kulazimisha uchaguzi wa marudio ambao umewaweka madarakani wale walio wachache (the Minority)...Kwa hali ilivyo sasa kule Pemba ni sawa na umwondoe mbunge Godbless Lema kwa mabavu pale Arusha Mjini na badala yake umweke madarakani Monaban halafu utarajie apewe support toka kwa wakazi wa jiji hilo, thubuuutu, wakazi wa Arusha hawaitaki kabisa CCM. Pemba haitakuwa na maendeleo yoyote katika kipindi hiki cha miaka mitano ya maigizo. Wapemba wamesusia kila kitu, tusijidanganye.
 
Kwa 100% ninaamini umaarufu/confidence ya wananchi wa Arusha kwa Lema imefikia 21.1%, na huko Pemba wasipotoa support serikali itatekeleza maana matatizo ya wananchi wa Pemba na maeneo mengine ya hii nchi yanajulikana.
 
Pemba ni ngome ya kihistoria na mahusiano yake na CUF hayawezi kufifishwa kwa miaka mitano. Uhasama wa CUF na CCM unaanzia zamani sana kabla ya kuwapo CCM na CUF yenyewe. Hawa wote ni warithi wa siasa za kabla ya mapinduzi.

Kuwachanganya ZNP, ZPPP na ASP ndani ya CCM kulisaidia kidogo maana kiasi flani vijana kama Salim waliweza kuwa wanaCCM hadi leo. Ila historia imetuambia baada ya vyama vingi kuibuka vyama against ASP vimeibuka na kuwa na nguvu tena.

Naamini CUF itarudi imeimarika 2020, kwa kuwa agenda ya muungano wa mkataba na Zanzibar huru ambayo ndio kiu ya Wazanzibar haviwezi kufanikishwa na Shein wala CCM hii. Na ndio hapo CUF watakapoitesa CCM tena.
 
Mie niko pemba hali nnavyo iona kuliko tulivyo tarajia kwa kweli wananchi wengi wamekubali matokea na ugomvi wa watu wa pemba si CCM bali ni maendeleo na madai yao makubwa ni kuwa pemba imetengwa watu wapemba hawaichukii CCM bali wanachukia kutengwa na kuwa nyuma kimaendeleo
 
Wanabodi,
Huu ni uzi kuhusu kitu kinachoitwa "trend Reading" kwa jina la Kiswahili ni "kusoma mielekeoewn. Katika uzi huu, nazungumzia mielekeo ya Kisiwa cha Pemba, baada ya lile igizo la uchaguzi wa Marejeo wa Zanzibar.

Jee mielekeo ni nini? . Mielekeo ni mambo yatakayokuja kutokea ambayo yamesababishwa na mambo yaliyotangulia kutokea kabla na mambo yanayotokea sasa, ili kujua mambo yatakayokuja kutokea siku zijazo. Kwa kifupi hii ndio maana halisi ya somo la Historia ambayo ni " the study of the past in relation to the present to determine the future". Kujua mambo ya kale na kuyahusianisha na mambo ya sasa ili kujua mambo yajayo.

Kwa kisiwa cha Pemba, hii ndio ilikuwa ngome kuu ya Chama cha CUF, ambapo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, Pemba yote imekuwa ikishikiliwa na chama cha Wananchi CUF katika nafasi zote za Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Uwakilishi wa Baraza la Wawakilishi, na hadi sasa, wabunge wote wa Pemba ni kutoka Chama cha Wananchi CUF, lakini kufuatia Chama cha CUF kususia Uchaguzi, Chama cha Mapinduzi, kimeiteka ngome kuu ya CUF na kuikalia kufuatia ushindi wa kishindo uliopatikana na kutokana na igizo la uchaguzi huo wa marudio.

Japo CUF kina wabunge ndani ya bunge la JMT, wabunge hawa, hawana impact yoyote kule Pemba kwa sababu Bunge la JMT, ni Bunge jina tuu, kuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Spika wa Bunge ni Spika wa Bunge la Muungano jina tuu, kiukweli, Bunge la JMT, sio Bunge la Muungano, ni Bunge la Iliyokuwa Tanganyika, ila linashughulikia na Mambo yote ya Muungano kwa huku Tanzania Bara Tuu!. Hivyo Bunge ni la Bara, ila limevaa koti tuu la Muungano, hivyo Wabunge wa CUF ndani ya Bunge, hawana impact yoyote kwa Pemba, kwa sababu Bunge la JMT ni bunge jina tuu la JMT ila kiuhalisia ni Bunge la Bara hivyo sio Bunge la Muungano.

Kuthibitisha kuwa Bunge letu sio bunge la Muungano, sheria zote za muungano zinazotungwa na Bunge 'Bara' hazina mamlaka ya kutumika Zanzibar, hadi sheria hizo ziridhiwe na Baraza la Wawakilishi, hii inamaanisha BLW ndiocho supreme organ ya utungaji wa sheria Zanzibar, kituo ambacho wajuvi wa mambo ya katiba, wanakiona kama ni kichekesho, yaani kikatiba, Zanzibar ni sehemu ya JMT, na katiba ya JMT ndio the supreme, na Bunge la JMT ndio supreme organ ya utungaji wa sheria, ambapo Spika wa Bunge la JMT was supposed to be the supreme Speaker, na sheria zikitungwa na Bunge, lazima kwanza ziridhiwe na rais wa JMT (accent) ili ziwe sheria na kuanza kutumika ndani ya JMT, lakini eti sheria hizo, haziwezi kutumika sehemu fulani ya JMT, hadi BLW liridhie, kati ya Bunge la JMT na BLW, nani zaidi?!, yaani sheria imepitishwa na Bunge la JMT, na kuridhiwa na rais wa JMT, itumike ndani ya JMT, halafu haiwezi kutumika eneo fulani hadi iridhiwe na mdudu fulani anayeitwa BLW, hiki ni kichekesho na dharau kubwa kwa mamlaka ya rais wa JMT. No wonder, Rais wetu wa JMT, Waziri wetu Mkuu wa JMT, Spika wetu wa Bunge la JMT, Jaji wetu Mkuu wa Mahakama Kuu ya JMT, they are all nobodies kwenye set up ya Zanzibar, kwa sababu ndani ya Muungano, Zanzibar nayo inajiita ni nchi, ina rais wake, bunge lake, na mahakama yake!.

Sasa nikirudi kwenye hatima ya Kisiwa cha Pemba chini ya CCM, Pemba itahesabiwa alikuwa ni yule mwana mpotevu ambaye alipotea toka kwa baba yake, na sasa amerejea kwenye mikono ya baba yake!, hivyo atafanyiwa karamu kubwa. Atapewa kila anachokitaka na kuletewa hata kila sichokitaka ali muadi kitaonekana kina mfaa!.

Jee Pemba ya CCM, itakuwa ni Pemba ya Raha tele?, ulinzi tele?, maendeleo tele?, uwekezaji tele?, ajira tele?, na itapatiwa preferential treatment kwenye kila kitu?, ili kujenga imani kwa Wapemba kuishabikia CUF, ilikuwa ni makosa, ili itakapofika 2020, wakati wa kuamua tena, wananchi wa kisiwa cha pemba wapate fursa ya kuipima hii miaka 5 ya CCM Pemba, na kuilinganisha na miaka 20 ya CUF Pemba, nani amefanya nini?!. Kwa vile 2020, Wapemba watapata fursa nyingine ya kuamua ama CCM ama CUF, then nawahakikishia kipindi hiki, CCM Zanzibar, haitafanya makosa tena, nguvu zote itazihamishia Pemba, ili 2020, Wapemba wenyewe kwa ridhaa yao, wataivote out CUF katika uchaguzi huru na wa haki, na sio kupitia tena kwenye igizo la uchaguzi.

Au kwa vile Pemba walikuwa wanaichagua CUF, na sasa CCM imeishika kimabavu kupitia lile igizo la uchaguzi, hivyo sasa Pemba watajuta kuichagua CUF, hivyo sasa Pemba chini ya CCM, cha moto watakipa, na kujuta kuichagua CUF, hadi wajisikie walifanya makosa kuitegemea CUF, kuliko kuichagua tena CCM 2020, ni heri wakairudisha CUF yao waliyoizoea!. Jee hii miaka 5 ya CCM Pemba, itakuwa ni miaka ya neema kwa Wapemba au majuto?.

Namalizia kwa lile swali la msingi, "Jee Pemba Chini ya CCM, Itaneemeka Au Kujutia Kuichagua CUF Chaguzi Zilizopita?!".

Nawatakia Ijumaa Kuu Njema.

Pasco
Maalim ameshafanya yake...mkewe keshapanda ndege....huduma wataboreshewa...japo ifikapo 2020 simuoni Maalim CUF laasivyo itajigawa....kuna wanasiasa CUF kwa kukosa ajira(uwakilishi na udiwani)...wameumia na kuna mpasuko waja labda Seif atangaze kuachia madaraka....siasa za majukwaani tu haziwapi motisha baadhi ya wanasiasa!
 
Ukiwaanbia watu ukweli huu watakupiga mawe...tangu mwanzo CUF hawakutakiwa kufuata hisia za wafuasi kwa kudhani wanawakomoa CCM
Baada ya Dr.Shein kuapishwa na wawakilishi kuapishwa akili zitawajia...hawatagombana na CCM bali wao kwa wao....wengi walifuata mkumbo...ni sawa na mwanafunzi hujigamba ila akifukuzwa ndipo hugundua madhara ni yake binafsi na sio kundi.
 
Pasco kabla ya vyama vingi CCM haikuwasiadia Pemba wala kuwapa support.Pemba ni eneo maskini kupita kiasi.Wapemba wengi wameshafukuzwa Kazi serikalini.

Kipigo walichopata Wapemba toka kwa Mazombie,Jeshi na Polisi ndiyo chachu kubwa ya wawakilishi hao kutoweza kufanya kazi.

Wakiulizwa walikuwa wapi wakati wanapiga na kunyanyasa na serikali watajibu nini??
Uadui,Chuki vitatawala kwa.miaka mitano.Hata CCM wenyewe wanajua kwamba kwa Pemba hawatavuna kitu.
 
Sielewi CUF waliingiwa na nini ....haukuwa uchaguzi wa kususa kabisa ....CCM wamewazuga kama wanawahitaji kwenye uchaguzi kuwajaza kiburi kumbe mchoro wa kuiua CUF umeiva ...

Na kuna wapuuzi humu waliwajaza CUF ujinga wakidhani walikuwa wanawakomoa CCM. Matokeo yake CUF wko solemba miaka 5 inapita kavu kavu, Maalim yeye anakula mambo mazuir na familia yake...waliofuata mkumbo, mf. wawakilishi miaka 5 ni mingi sana kuumia
 
Pasco kabla ya vyama vingi CCM haikuwasiadia Pemba wala kuwapa support.Pemba ni eneo maskini kupita kiasi.Wapemba wengi wameshafukuzwa Kazi serikalini.

Kipigo walichopata Wapemba toka kwa Mazombie,Jeshi na Polisi ndiyo chachu kubwa ya wawakilishi hao kutoweza kufanya kazi.

Wakiulizwa walikuwa wapi wakati wanapiga na kunyanyasa na serikali watajibu nini??
Uadui,Chuki vitatawala kwa.miaka mitano.Hata CCM wenyewe wanajua kwamba kwa Pemba hawatavuna kitu.

Nyinyi mko nyuma ya keyboard mnawadanganya wenzenu. Maalim Seif yeye atakula maisha mazuri tu kwa marupurupu aliyo nayo, kimbembe kwa wale wawakilishi na chama kwa ujumla...mtawapa ruzuku na mishahara?
 
Back
Top Bottom