Peleka cv hapa alafu sikilizia unaweza pata kibarua/ajira

Jenseny

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
1,743
1,732
Pole kwa kumaliza chuo na kutafuta kazi! naamini hakuna kazi ngumu kama kutafuta kazi! pole na usikate tamaaa

zifuatazo ni baadhi ya kampuni chache zilizopo Dar es salaam zinazounganisha waajiriwa na waajiri ukipeleka cv hapa unaweza kupata kazi kwene makampuni ya simu bank na insuarance company.

zote hizi hapa chini ziko mtaa mmoja Morroco(mikocheni ya juu) so unaweza kutoa copy nyingi ukapeleka ukasikilizia

Erolink -nyuma ya sheli ya bonjour pale Morocco kuna barabara inanyoosha nyoosha nayo hadi utaifikia ukifika nyuma ya sheli ya bonjour utawakuta mama ntilie waulize

Intrgrated comm ipo nyuma ya sheli ya bonjour

Infinity communication rudi na njia hiyohiyo uloenda nayo Erolink vuka barabara nyoosha hadi uvuke yadi za John Deer upande wa kulia utaona ofisi za infinity

kampuni nyingine huwaga zinatoa vibarua tu haziajiri vibarua mara nyingi ni vya utafiti

Repoa na Synnovate zipo nyuma
ya ile plaza imenitoka jina ila synnovate ipo ndani ya jengo la ghorofa ambalo kwa nje limechorwa logo za smile uliza tu kwa walinzi hapo nje peleka cv sikilizia Repoa ipo pembeni ya hilo ghorofa

kariri hayo majina ukishapata ofisi moja ulizia ofisi nyingine

KABLA YA KWENDA HAKIKISHA UNA GOOGLE UNAJUA KAMPUNI INAJIHUSISHA NA NINI

HAKIKISHA UNAJUA COMPUTER APPLICATION SOFTWARE KAMA UNAPELEKA CV KWENE MAKAMPUNI YALE YA JUU

HAKIKISHA CV YAKO INA MAWASILIANO YANAYOPATIKANA 24 hrs

KWA WALE WA MBALI MBAGALA CHANIKA BAGAMOYO HAKIKISHA CV YAKO UNAANDIKA UNAISH MITAA YA KARIBU NA MJINI

UKIPIGIWA SIMU ONGEA KISTAARABU NA USIKUBALI KUTOA HELA AU KUKUTANA NA MTU UKIWA PEKE YAKO

USITOE PENZI ILI UPATE AJIRA JAPO KAMA UMEMPENDA TRAINER NI WW MWENYEWE

PELEKA CV SIKILIZIA INAWEZEKANA IKAWA BAHATI YAKO

HEBU ANDIKA SEH NYINGINE UNAYOIJUA

0621068486
 
asante sana. samahani naomba kuuliza, kwa mfano napeleka CV somewhere natakiwa niambatanishe na copies za academic na nyingnezo?
cv tu! walikuita ndo inatakiwa wakikuita kwene usaili ndo utaenda na origin cert na copy za vyeti
 
Repoa???? Simple hivyo???? Achen utani..labda una ndugu.
Esrf tu wana utaratibu wa kupokea leo ije hivi
 
Kwa REPOA sidhani kama unaweza kupata kiurahisi hivyo ila hizo nyingine inawezekana.Mimi nilipeleka Erolink ni mwaka wa tano sasa sijaitwa.Ukweli ni kwamba hata kwenye hizo recruitment agencies wameshaingiza kujuana na kupendeleana,kama huna mtu unayemjua,kupata ni ndoto sana achilia mbali kwamba client anatoa milioni moja kama mshahara wako huyo recruitment agent anakupa laki mbili.
Kuhusu Synovate (Kwa sasa Ipsos) wao wanahusika na mambo ya utafiti (research),hawa nilishafanya nao kazi,kwa kweli hawana upendeleo wala kufahamiana na huwa wanachukua watu kutegemeana na aina ya project walio nayo,hiyo project ikiisha mnaachana ila kwa kuwa unakuwa umeshafanya nao,ikitokea project nyingine wanakuita(Kimsingi kwao project haziishi,zipo kila iitwapo leo maana ndo kazi yao pekee).

For more information about Synovate (Ipsos) and how to join you can PM me.
 
erolink wanapenda watu wenye elimu ndogo dip na form 6 leaver ili waendelee kuwepo kazini degree na masters huwaga wanawatoroka mapema so ka ulipeleka cv kwa cheti cha degree jaribu kwa kutumia cheti cha 6 blv me watakuita week hii hiii kuhusu Repoa kuna secretary nasikia anachanaga cv za watu ila ipo siku yake Ongeza recruit centers nyingine wadogo zetu wakajaribu bahati
 
Sehemu nyingine ya kupeleka ni ISON-BPO ni kampuni ya customer care wanafanya na Airtel hawa wana ofisi jengo la Quality Plaza/Quality Centre (haya majengo huwa nayachanganya) lenyewe ni lile mall.. Ofisi yao ipo ndani ukiingia ghorofa ya kwanza kushoto.. Nilipelekaga CV na niliitwa kwenye interview ila sikwenda maana nilishapata sehemu ingine. Pale huwa wanaajiri mara kwa mara.. Kwa kuanzia si mbaya japo ujira ni mdogo sana lakini si sawa na kukaa bure nyumbani
 
Ok mkituwekea na qualifications wanazohitaji ni vizur zaid..pia idea km mfano hizo kuwa wanapendelea zaid watu wa aina gani itatusaidia kweny kuandaa c.v
 
Sehemu nyingine ya kupeleka ni ISON-BPO ni kampuni ya customer care wanafanya na Airtel hawa wana ofisi jengo la Quality Plaza/Quality Centre (haya majengo huwa nayachanganya) lenyewe ni lile mall.. Ofisi yao ipo ndani ukiingia ghorofa ya kwanza kushoto.. Nilipelekaga CV na niliitwa kwenye interview ila sikwenda maana nilishapata sehemu ingine. Pale huwa wanaajiri mara kwa mara.. Kwa kuanzia si mbaya japo ujira ni mdogo sana lakini si sawa na kukaa bure nyumbani
wapo sehemu gani
 
Back
Top Bottom