Pele - The Global Icon

Don Clericuzio

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
16,936
40,518
Wakati tukiendelea kumpa pole Messi na Barcelona kwa kipigo kikubwa kutoka kwa Bayern, nimepata nafasi ya kuandika kidogo kuhusu Pele, ni tafsiri kutoka kwenye kitabu chake cha Why Soccer Matters, na kiasi kutoka kwenye machapisho mengine yanayohusu maisha ya huyu nguli.

Nilipata motivation ya kufanya hivyo baada ya discusion kati yangu na Nabii kibonge aliyeleta threads mbili, moja ikiwa ni kuhusu Messi na washabiki wake wanaomwita GOAT, na nyingine ikiwa ni kuhusu Thomas Muller, kama mchezaji asiyepewa heshima anayostahili.

Nilichangia kwa kiasi kidogo sana kwa sababu huwa najitahidi kukwepa kuweka ulinganifu wa nani ni bora zaidi ya mwingine hasa kwa watu waliocheza kwa nyakati tofauti, hapa nazungumzia issue ya nani The Real Goat kati ya Pele, Maradona na Messi.

Lakini nikasema kwa mara nyingine tena nizitafute habari za huyu mjamaa wa kuitwa Pele, yeye mwenyewe hajui hili jina alilipata vipi. Wikipedia wanasema alipewa baada ya yeye kuchapia kumtaja golikipa wa timu ya Vasco Da Gama anayeitwa Bilé. Lakini kwenye kitabu chake cha Why Soccer Matters, Pele anasema alilipewa na watoto wenzake aliokuwa anacheza nao kipindi hicho, maana alikuwa anaanza kama golikipa na mwishoni ndiyo anaingia kucheza ili magoli ya timu yake yasiwe mengi, watoto hao walikuwa wanamfananisha na huyo kipa Bile, ikaenda mpaka kuwa Pele.

Edson Arantes do Nascimento, ndiyo jina halisi la Pele, alilipewa kumuenzi Thomas Edison, inventor wa light bulb. Hata hivyo walilikosea kwa kuondoa i kwenye Edison.

Pele akiwa mdogo ilikuwa ni yeye na mpira, mpira na yeye, mpaka shule alikuwa mtoro sana kwa sababu muda wa kukaa darasani aliona kama anapoteza, ikawa mara nyingi anapewa adhabu ila akawa hakomi, anasema kuna siku alipewa adhabu ya kuita ndege huku amegeukia ubaoni, baada ya hapo ndo akawa mtoro zaidi na zaidi.

Kwenye masimulizi yake, anasema katika harakati za kutafuta hela za kununua viatu na jezi, waliwahi kwenda kuiba karanga kwenye treni la mizigo, walivyoona haitoshi wakaenda kuiba kwenye store, hapa kwenye store anasema hawakufanikiwa, mvua iliibuka ghafla na store yenyewe ilikuwa kwa mfumo wa korongo, udongo ulimfukia mwenzao mmoja na akafariki, huo ndiyo ukawa mwisho wa wao kuiba.

Kocha wake wa kwanza alikuwa ni baba yake ambaye aliitwa Dondinho (hii ni aka), ambaye alikuwa mcheza mpira pia, Dondinho anakumbukwa kwa kufunga goli 5 kwa kichwa ndani ya mechi moja, record ambayo hata Pele hajaifikia.

Akiwa na miaka 15, alichukuliwa na timu ya Santos, alianza kucheza timu ya vijana, game yake ya kwanza na kwenye timu ya wakubwa ilikuwa ya kirafiki ambapo walishinda 6 – 1 huku yeye akifunga magoli 4, baada ya hapo hype ikawa kubwa sana, vyombo vya habari na washabiki wakaanza kushinikiza Pele aingie kwenye timu ya wakubwa.

Mechi yake ya kwanza official ilikuwa dhidi ya Corinthians iliyochezwa tar 7 Sept 1956 ambayo ni siku ya uhuru kwao huko, Pele alifungua akaunti yake ya magoli siku hiyo kwa kufunga goli 1, akaunti iliyokuja kufungwa ikiwa na magoli 1279 (Messi na Ronaldo wana jumla ya magoli 1,470+, hawajafika 1,500). Hizi statistics zinapishana kutegemea na source, kuna wanaotaja 1280, 1282. All in All ni maeneo hayo hayo.

Baada ya hiyo mechi, washabiki wa The Corinthians waliwapigia makofi Santos kwa sababu ya kile walichokiona kwa Pele. Kuna muda timu inafungwa lakini inabidi ukubali ubora wa wapinzani, Man United wanakumbuka siku Ronaldo De Lima anapata hattrick Old Trafford May 2003 akiwa na Madrid na wakasimama kumpa heshima yake. Katika Maisha yake Pele ya mpira, hizi amekutana nazo mara nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote wa Soccer.

Baada yah apo, Pele akawa ni moto, mwaka mmoja mbeleni akaitwa timu ya taifa iliyokuwa inajiandaa kucheza kombe la dunia 1958.

Zikiwa zimebaki siku chache kwenda kombe la dunia, Pele aliumia kwenye mechi ya maandalizi dhidi ya Corinthians, kuna uwezekano mkubwa aliumizwa kwa makusudi kwa sababu Corinthians walikuwa na kinyongo na hasira kwa sababu mchezaji wao Luizinho aliachwa kwenye timu ya taifa na nafasi yake kuchukuliwa na dogo wa miaka 17 ambaye ni Pele.

Injury ilikuwa kubwa kiasi timu ikataka kumwacha, kwa sababu ilionekana kwamba hataweza kupona ndani ya muda mfupi na atayakosa mashindano, wenzake na baadhi ya madokta wakasema wataenda naye hivyo hivyo, kwa umri wake ilisemekana kuna slight chance ya yeye kupona kabla ya wakati. Pele alisafiri na timu, na walikaa mwezi mmoja nje ya Brazil wakifanya maandalizi, wakati huo yeye akitibu jeraha.

World Cup 1958 – Sweden:
Brazil ilikuwa na kikosi chenye wachezaji 22, maarufu kati yao ni Pele mwenyewe, Mario Zagallo (kocha 1970 WC winners, kocha msaidizi 1994 WC winners na kocha 1998 WC first runners), Garrincha (winga machachari huyu), Didi (kiungo mchezeshaji, ndiye mchezaji bora wa mashindano hayo), Zito (sijui kama Zitto Kabwe alichukua jina lake hapa) na Vava.

Brazil iliwekwa kundi moja na Soviet Union (hawa walikuwa wanajiita wazee wa sayansi), England na Austria.

Mechi ya kwanza walianza na Austria, walishinda 3 bila, Pele na Garrincha hawakucheza, mechi ya pili ilikuwa vs England, iliisha 0 – 0, hii nayo Pele na Garrincha hawakucheza, ikabakia mechi ya mwisho wanatakiwa kucheza na Soviet Union ambao walikuwa ni favorite wa mashindano, hii ilikuwa mechi ambayo ushindi ni lazima ili kusonga mbele (au draw).

Mind games zilikuwa zipo toka enzi hizo, wapinzani hawakuwa wanamjua Pele, maana alikuwa dogo tu na kipindi hicho kupata taarifa ilikuwa vigumu sana, kwa hiyo kwenye scout yao hawakumwona, na ilipokuja kutangazwa kikosi, wanashangaa Brazil wameleta mtoto kwenye mashindano. Garrincha naye ndani.

Mechi iliisha 2 bila, magoli yaliyofungwa na Vava, moja likiwa assisted na Didi na lingine likiwa assisted na Pele, ila show yote ilikuwa ya Garrincha siku hiyo. Na magazeti yakifanya kwasifu Brazil, yaliandika, “You Will Get To See Garrincha Again”.

Brazil waliongoza kundi na kusonga mbele, robo fainali wanakutana na Wales, wanashinda 1 – 0, goli la Pele. Goli hili lilikuwa moja ya magoli mazuri ya mashindano hasa pia ukichukulia na umri wake, nitaweka footage ya hili goli post inayofata. Lilikuwa assisted na Didi baada ya kupokea pasi toka kwa Garrincha.

Nusu fainali hii hapa, Brazil vs France, hii haikuwa France ya kina Zidane, France iliyosababisha nihame timu kutoka Brazil na kushabikia France siku ile ya fainal WC 1998. Brazil wanashinda 5 – 2 huku Pele akiwa na goli zake 3, hattrick safi, magoli mengine yalifungwa na Viva na Didi. Kumbuka Pele baada ya kufunga goli dhidi ya Wales, tayari washabiki walianza kuishangilia timu ya Brazili. Pele anasema baada ya mechi kuisha ilikuwa shangwe sana, hasa ukichukulia Fainali ilikuwa inawakutanisha wao na waandaaji, Sweden. Ilikuwa ni Pele, Pele, Pele!

Siku ya Fainali ikafika, Brazil ilibidi watafute jezi mpya kwa sababu ya kuingiliana rangi na jezi ya wenyeji. Wote walikuwa wanatumia njano.

Mechi iliisha kwa 5 – 2, Pele akifunga magoli 2, Vava 2 na Mario Zagallo akifunga goli 1. Goli la Pele la dakika ya 90 lilikuwa goli la kichwa, anasema baada ya kufunga hilo goli ali pass out, sijui kama ni kuzimia au la, lakini anasema alikuja kushtuka akiwa anapepewa, ile kushtuka tu akaanza kulia huku amebebwa na wachezaji wenzake, hapo ndo ikawa mwisho wa mashindano na mwanzo wa dunia kupata nguli wa mpira, PELE!

Maisha baada ya 1958
Pele akiwa na timu yake ya Santos walipata umaarufu san ana wakaanza kucheza mechi za kirafiki ndani nan je ya Brazil, walipata mialiko mingi kila mahali duniani, huku Pele akishangiliwa kila anakokwenda. Mfumo wa malipo ulikuwa ni 100:30, kwamba kama Pele yupo timu ikialikwa inalipwa 100, ila kama Pele hayupo inalipwa 30.

Katika moja ya tours zao, kuna kipindi wakati wakiwa Nigeria, kulifanyika mapinduzi, wale jamaa waliopindua nchi wakataka wambakishe Pele awe mnaijeria kwa lazima, alikuja kutoroshwa akiwa kama rubani wa ndege.

Pele anasimulia kwamba mwaka 1968, wakiwa wanacheza mechi nchini Colombia, refa Guillermo “Chato” alimpa kadi nyekundu, wakati anaondoka kwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo, refa akabadilishwa na Pele akaitwa ili aendelee kucheza, imagine, refa unatoa kadi halafu kadi inakugeuka.

Mara nyingi tunajiuliza, zile goli 1279 alizifikishaje?
Anasema kwenye tours, walizokuwa wanasafiri, walikuwa wanacheza mechi nyingi sana, kuna wakati wanaweza kucheza mechi 4 ndani ya wiki moja, kwa hiyo hii hesabu ya kila mechi goli, na amekuwa kwenye career kwa miaka zaidi ya 17, hivyo anahesabu na hizo mechi za kirafiki.

Magoli ya kimashindano: Santos – 504 (1956 – 1974), New York Cosmos – 37 (1975 – 1977), Brazil 77 goals, inafanya kuwa 618. Yaliyobaki ni ya kirafiki. (Wikipedia)

Kombe la Dunia 1962 – Chile:
Katika mashindano haya, Pele alikuwa ndiye mchezaji bora wa dunia kwa kipindi hicho (Wikipedia). Mwaka mmoja kabla ya hapa, Serikali ya Brazil ilikuwa imemtangaza Pele kuwa National Treasure, kwa hiyo hakutakiwa kuchukuliwa na timu yoyote nje ya Brazil. Wengi huwa tunajiuliza ilikuwaje Pele hakucheza timu kubwa kama Real Madrid, Inter Millan nk, hii ilikuwa ni moja ya sababu kubwa. Lakini pia Brazil na mataifa mengi yalikuwa na taratibu za kutumia wachezaji wa ndani kwenye timu zao za taifa.

Mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Mexico, mechi iliisha 2 – 0, akifunga goli moja na kutoa msaada goli moja. Goli alilofunga aliwachambua mabeki wa 4 na kufunga.

Mechi ya pili dhidi ya Czechoslovakia, aliumia. Hata hivyo ilibidi aendelee kubaki mchezoni mpaka mechi iishe, kipindi hicho ilikuwa hakuna kubadilisha wachezaji, anayeanza lazima amalize, akiumia mtu hakuna wa kubadilisha naye. Pele anasema wapinzani walionesha fair play kwa sababu walimsaidia pia kwa kutomkaba isije wakamuumiza zaidi.

Hakucheza tena mpaka mashindano yanaisha, Brazil waliibuka mabingwa, huku Garrincha akiwa ndiye nyota wa mashindano.

Kombe la Dunia 1966 – England

Brazil hawakufanya vizuri kwenye haya mashindano, kuna sababu kadhaa ambazo Pele anazieleza kuwa chanzo cha wao kufeli, cha kwanza ni siasa, nchi ilikuwa katika hali mbaya ya kisiasa, na hivyo wanasiasa katika kujiokoa wakawa wanaitumia timu ya taifa, anasema kwenye maandalizi walichaguliwa wachezaji 44 ambao waligawanywa katika makundi 4, kila kundi likawa linaenda kucheza mechi katika maeneo tofauti na tofauti nchini kwao, hii ilikuwa kama show games na siyo mazoezi, hivyo timu ikakosa chemistry.

Kitu kingine ilikuwa ni marefa kuruhusu fouls kwenye hayo mashindano, hii ilikuwa mbinu ya kuwapunguza makali South Americans, iliwapa favor Europeans kwa sababu ya maumbo yao kuwa makubwa na nguvu ukilinganisha na South Americans.

Mechi ya kwanza walitoka na ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Bulgaria, Garrincha na Pele wakiwa ndiyo wafungaji, mechi iliisha huku kina Pele wakiwa wametandikwa buti za kutosha na huku refa akikausha.

Mechi ya pili ilikuwa dhidi ya Hungary, hii mechi Pele alipumzishwa, Brazil walipoteza kwa 3 – 1. Hungary ni timu iliyokuwa imewatoa pia mwaka 1954.

Mechi yao ya mwisho ilikuwa dhidi ya Portugal, hii mechi Pele aliumizwa mapema sana lakini ilibidi abaki mpaka mwisho wa mechi kwa sababu kipindi hicho kulikuwa hakuna kufanya mabadiliko. Walipoteza kwa 3 – 1. Safari yao ikaishia hapo, ndoto za kukabidhiwa kombe na Malkia kwenye uwanja wa Wembley hazikufikiwa.

Baada ya mashindano hayo, Pele alitangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa, hasa ikichukuliwa kwamba mchezo umekuwa wa kinyama sana, sharia zimekuwa kandamizi.

Antonio Rattin, namba 10 wa timu ya Argentina kwenye hayo mashindano amewahi kuyaita hayo mashindano, “the most violent World Cup of all time.”.

Brian Viner, mwandishi wa Kiingereza, aliandika kwenye The Independent of London mwaka 2009 kwamba, “several players (for Brazil), but Pelé in particular, suffered some of the most egregiously vindictive man-marking ever seen.”

World Cup 1970 – Mexico
Baada ya kufanya tafakuri ya kutosha, mnyama Pele aliamua kutangaza kurudi tena kwenye timu ya Taifa ili kuisaidia kuchukua komba kwa mara ya tatu.

Chini ya kocha mtata João Saldanha, kiliandaliwa kikosi maalumu kwa ajili kujenga chemistry ya timu, kikosi hicho kilijulikana kama Saldanah’s Beasts.Wachezaji wengi wakitokea Santos na Boltafogo ambazo zilikuwa kama Yanga na Simba kwa kipindi kile kule kwao. Kikosi hicho kilishinda mechi zote 6 za qualifying mwak 1969, hapo Saldanah akavimba kichwa, akaanza udikteta kwenye timu, Pele na wenzake wakashindwa kumvumilia, kocha akafukuzwa.

Hapo ndo kuja Mario Zagallo, huyu ndiye Zagallo aliyekuwa kocha wa Brazil ya kina Ronaldo iliyofungwa na Zidane siku ya fainali mwaka 1998. Zagallo hakuibadilisha sana timu, alibadili wachezaji wachache sana, yeye mfumo wake ulikuwa ni team work zaidi kuliko individual brilliance.

Timu ilisafiri mwezi mmoja kabla ili kuyazoea mazingira ya Mexico, na walivyofika tu ilibidi Serikali ya Mexico iwaombe Brazil wairuhusu serikali impe ulinzi binafsi, na ahamishwe hotel, maana kulikuwa na hatari ya yeye kutekwa. Hilo likafanyika.

Mwaka huo, mfumo wa kadi za njano na nyekundu ulianza kutumika ikiwa ni mbinu ya kuwalinda wachezaji na fouls, pia kubadilisha wachezaji (substitution) ilipitishwa tofauti na mashindano yaliyopita.

Kwa mara ya kwanza pia, mashindano hayo yalionyeshwa kupitia TV za rangi.

Game 1 wanaanza na Czechoslovakia, Brazil anashinda goli 4 – 1 huku Pele akiwa amefunga goli 1, Rivellino 1 na Jairzinho goli 2. Hii timu ni ile Pele aliumia wakiwa wanacheza 1962 na hawakumfanyia figisu za kumuumiza zaidi, wakamsaidia kumaliza mechi salama, ila hakuendelea na mashindano.

Mechi iliyofata ilikuwa dhidi ya England ya kina Bobby Moore na Bobby Chalton ambao walikuwa ndiyo mabingwa watetezi. Brazil alishinda goli 1 bila likifungwa na Jairzinho kwa assist ya Pele. Pele anasema it was one of the unselfish moment, kwa sababu kila mmoja alitaka ushindi bila kujali nani anafunga. Hata pasi aliyoitoa kwa mazingira ya kawaida angetafuta kufunga yeye.

Mechi ya mwisho kwenye makundi walicheza na Romania, Pele alifunga magoli mawili, Jairzinho akifunga goli 1, mechi ikiisha kwa ushindi wa 3 – 2.

Robo fainali wanakutana na Peru, Brazili inashinda 4 -2, magoli kutoka kwa Rivellino, Tostao aliyefunga goli 2 na Jairzinho.

Nusu fainali wanakutana na maadui wao wakubwa, Uruguay, miaka 8 nyuma, Uruguay ilichukua kombe la Dunia lilichozewa nchini Brazil kwa kumfunga mwenyeji 2 -1 kwenye uwanja wa Maracana. So, hii ilikuwa ni nafasi ya kina Pele kulipiza kisasi, maana walikuwa radhi wakose kombe ila wamfunge Uruguay.

Mechi inaisha kwa Brazil kushinda 3 -1, magoli kutoka kwa, Clodoaldo, Rivellino na Jairzinho. Kisasi kikalipwa na Brazil wakafanikiwa kutinga fainali.

Fainali walikutana na Italy ambayo ilikuwa imewatoa wenyeji Mexico kuingia fainali, kwa hiyo umati wa washabiki ulikuwa upande wa Brazil kwa sababu kuu mbili, hiyo ya kutolewa na ya ubora na show wanayoipata kutoka kwenye timu ya Brazil.

Mechi iliisha kwa Brazil kushinda 4 – 1, magoli kutoka kwa Pele, Gerson, Jairzinho na Carlos Alberto, hili goli la Carlos Alberto ilikuwa alifunge Pele ila akampa mwenzake afunge ambaye alikuwa ni team mate kwenye team ya Santos n ani beki, hivyo Pele akiwa kwenye nafasi ya kufunga akamwona jamaa anakuja akampasia na kufunga goli.

Jairzinho alimaliza mashindano kwa kufunga kila mechi, record iliyoendelea kuwepo mpaka leo, 2002 Ronaldo de Lima alitishia kuivunja hii record, alikosa mechi moja dhidi ya Uturuki.

Gerd Müller kutoka West Germany alimaliza kama mfungaji bora kwa magoli 10 na mchezaji bora wa mashindano.

Baada ya mashindano hayo, Pele alitangaza rasmi kustaafu timu ya taifa na akacheza mechi kadhaa za exhibition kama farewell games.

1974 alistaafu kucheza mpira, akaaga timu Santos.

Akiwa amesha retire, vigogo wa timu ya Marekani, New York Cosmos wakamwomba ajiunge nao ili kukuza mchezo wa Soccer nchini humo.

Ilikuwa ngumu sana kwake kwenda kucheza huko kwa sababu alikuwa declared kama National Treasure, hivyo ilibidi Henry Kissinger, Secretary of The State atume barua kwa Rais wa Brazil kusema kama Pele akiruhusiwa kucheza Marekani, ita boost mahusiano ya hizi nchi mbili.

Pele akaruhusiwa, akasign mkataba na akacheza kwa misimu 3, 1975 – 1977.

Pele amestaafu since 1977, ni miaka 43 mpaka sasa, lakini ameendelea kuwa icon wa mpira. Nadhani ni watu wachache sana linapotajwa jina la Pele linakuwa geni kwao.

Pele kama angecheza mpira katika kipindi hiki cha mitandao ya simu na urahisi wa kupata taarifa, ninaamini huu mjadala wa nani ni mchezaji bora wa wakati wote usingekuwepo.

He demonstrated on the biggest stage at very young age, he continued at his old age. With all racism that was there by then, Pele alishindwa kuzuilika, hakukuwa na namna na ilibidi mataifa yamkubali tu kwa kila namna.

Alitumika kama ambassador kwa mashirika mengi sana, na alikuwa na endorsements za kutosha kutoka makampuni ya wazungu, they adored him.

Credits to Why Soccer Matters, Wikipedia, Youtube na All Sports Columnist wa JF.
 
Hii dunia ngumu sana Pele nae alikula house girl na kuzaa nae Omary Mahita nae alibugia house girl na kuzaa nae. Wakina mama fanye mahouse girl mema maana wanatumika zaidi. Kama Pele alibugia house Girl mimi ni nani nisipitenae.
 
Back
Top Bottom