Pele anaendelea kuimarika, hospitali yasema

a.k.a_Mimi

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
292
113
Legend Pele mgonjwa mahtuti
Jagina wa soka Brazil Pele alikuwa bado anapokea matibabu ya figo Jumamosi lakini hali yake inaendelea kuimarika, hospitali ya Sao Paulo alimolazwa ilisema.

"Hali ya mgonjwa Edson Arantes do Nascimento (Pele) inaimarika, anabaki katika kitengo cha wagonjwa mahututi akipokea matibabu ya figo," taarifa ya hospitali ya Albert Einstein ilisema.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Pele ataendelea kufanyiwa hemodialysis, shughuli inayoosha damu ya mgonjwa kupitia figo bandia kabla ya kuirejesha kwenye mwili.

Kigogo huyo mwenye miaka 74 "yuko katika hali nzuri na anazungumza" na ni "thabiti", taarifa hiyo ilisema, na anaendelea kutibiwa kwa dawa za kumaliza viini na kwamba "matokeo yote (ya kupimwa damu na mkojo) hayajaonyesha tatizo jingine".

Baadhi ya vyombo vya habari huko vilikuwa vikiripoti kuanzia Alhamisi kwamba 'O Rei' (Mfalme) alikuwa akiugua septicaemia na dawa hazikuwa zinamsaidia na kwamba hali yake ilikuwa "tete".

Pele, ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, huchukuliwa sana na wengi kama mchezaji bora zaidi kuwahi kuishi.

Alilazwa hospitalini Jumatatu, na akapatikana na maambukizi ya njia ya mkojo na kupewa dawa za kuua viini.

Alhamisi, hospitali hiyo ilisema aliwekwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi baada ya hali yake "kuwa tete kimatibabu," na kuzua wasiwasi mwingi.

Lakini Pele alisisitiza kupitia mitandao ya kijamii kwamba yuko sawa na kwamba alihamishiwa tu chumba kingine kwa sababu ya kuhifadhi usiri.

"Ningependa kuchukua fursa hii kuwajulisha kwamba ninaendelea vyema," aliandika kwenye akaunti zake Facebook na Twitter.

"Nimebarikiwa sana kupokea upendo wenu na uungaji mkono, na nashukuru Mungu kwamba hali hii si mbaya.

"Nilihamishiwa tu chumba kingine kwa sababu ya usiri pekee. Ingawa nafurahia sana wageni wote wanaofika kunitembelea, nahitaji sana kuendelea na matibabu yangu na kupona kwa amani."

Pele alikuwa awali amefanyiwa upasuaji kutolewa mawe ya figo katika hospitali iyo hiyo Novemba 13.

SuperSport.com
 
Jagina wa soka Brazil Pele alikuwa bado anapokea matibabu ya figo Jumamosi lakini hali yake inaendelea kuimarika, hospitali ya Sao Paulo alimolazwa ilisema.

"Hali ya mgonjwa Edson Arantes do Nascimento (Pele) inaimarika, anabaki katika kitengo cha wagonjwa mahututi akipokea matibabu ya figo,” taarifa ya hospitali ya Albert Einstein ilisema.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Pele ataendelea kufanyiwa hemodialysis, shughuli inayoosha damu ya mgonjwa kupitia figo bandia kabla ya kuirejesha kwenye mwili.

Kigogo huyo mwenye miaka 74 “yuko katika hali nzuri na anazungumza” na ni “thabiti”, taarifa hiyo ilisema, na anaendelea kutibiwa kwa dawa za kumaliza viini na kwamba “matokeo yote (ya kupimwa damu na mkojo) hayajaonyesha tatizo jingine”.

Baadhi ya vyombo vya habari huko vilikuwa vikiripoti kuanzia Alhamisi kwamba 'O Rei' (Mfalme) alikuwa akiugua septicaemia na dawa hazikuwa zinamsaidia na kwamba hali yake ilikuwa “tete”.

Pele, ambaye jina lake halisi ni Edson Arantes do Nascimento, huchukuliwa sana na wengi kama mchezaji bora zaidi kuwahi kuishi.

Alilazwa hospitalini Jumatatu, na akapatikana na maambukizi ya njia ya mkojo na kupewa dawa za kuua viini.

Alhamisi, hospitali hiyo ilisema aliwekwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi baada ya hali yake “kuwa tete kimatibabu,” na kuzua wasiwasi mwingi.

Lakini Pele alisisitiza kupitia mitandao ya kijamii kwamba yuko sawa na kwamba alihamishiwa tu chumba kingine kwa sababu ya kuhifadhi usiri.

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwajulisha kwamba ninaendelea vyema,” aliandika kwenye akaunti zake Facebook na Twitter.

“Nimebarikiwa sana kupokea upendo wenu na uungaji mkono, na nashukuru Mungu kwamba hali hii si mbaya.

“Nilihamishiwa tu chumba kingine kwa sababu ya usiri pekee. Ingawa nafurahia sana wageni wote wanaofika kunitembelea, nahitaji sana kuendelea na matibabu yangu na kupona kwa amani.”

Pele alikuwa awali amefanyiwa upasuaji kutolewa mawe ya figo katika hospitali iyo hiyo Novemba 13.

SuperSport.com
 
Back
Top Bottom