Peggy: Mdoli mwenye nguvu za giza ambaye ameripotiwa kusababishia watu matatizo waangaliapo video yake

Military Genius

JF-Expert Member
Mar 3, 2019
760
1,445
IMG-20200409-WA0080.jpg



MDOLI PEGGY (Peggy Doll).

Kwa Mujibu wa Wataalamu wa Kuchunguza Mambo ya Kutisha Kutoka UK, Wanasema kuwa Zaidi ya Watu 80 Wameripoti Kuumwa Hasa Maumivu Makali ya Kifua na Kukosa Pumzi au Kupata Matatizo Mengine Baada tuu ya Kuitazama Video ya Mdoli huyu Kama Kichwa Kuuma N.K.

Taarifa Kuhusu Mdoli huyu wa Kutisha Ziliandikwa Sana na Mitandao Mikubwa Duniani Ukiwemo Mtandao wa 'Daily Mail Online' wa UK Uliopost April 17, 2015, Habari ilikuwa na Kichwa:-

"Watch at your own Risk: Video of 'Haunted' Doll causes EIGHTY Viewers to Reportedly Suffer Chest Pains, Nausea and Crippling Headaches"

Mbali na Watu Kuripoti Kuumwa Hivyo, Kuna Wengine pia Waliripoti Kuwa Ndugu zao Wamepata Matatizo ya Akili Baada tuu ya Kutazama Video ya Mdoli huu Katika Mitandao, na Hata Zaidi ya Comments 5000 za Watu Katika Video hiyo YouTube Zinalalamika Hivyo. Nimekuwekea link Kwenye Bio Ukaitazame pia Ukihitaji.

Kundi la Wachunguzi Kutoka UK Lililojiita 'Haunted Doll's Social Media Group' Liliamua Kuanza Kazi ya Kumchunguza Mdoli huyu na Wakabaini Kuwa Kwa Mara ya Kwanza Mdoli huyu Alikuwa Akimilikiwa na Mwanamke Mmoja Aliyezaliwa Mwaka 1946 UK na Alifariki kwa Ugonjwa Pumu (Pumzi Kubana).

Walienda Mbali Zaidi na Kusema Kuwa Whenda pia Mmiliki wa Kwanza wa Mdoli Huyu Alihusishwa na Mauwaji/Kuuwawa, Kisanga Ndipo Kilipoanzia.

Watu Wengi Wamekuwa Wakilalamika Kuwa Computer zao Zime-Stack Wanapotazama Video ya Mdoli huyu, Chumba Kuaanza Kupata Ubaridi N.K na Whenda Usiyaone Haya Muda Unapotazama Video ya Mdoli huyu, Kuna Uwezekano wa Kuja Kuona hata Baada ya Muda fulani.

Wengine Wamelamika Kuota Ndoto Mbaya Usiku Baada tuu ya Kutazama Video ya Mdoli huyu, Kuna Mwanamke Anasema Amewahi Kuota Ndoto Akipewa Onyo na Mdoli huyu Kuhusu Paka Wake, Kuamka Asubuhi Akakuta Paka Wake Anaumwa!, Kesho Yake Akafa.

Mwingine Anasema Baada ya Kutazama Video na Kuanza Kujisikia Vibaya, Akaandika Katika Mtandao wake wa Facebook vile Alijisikia, Ajabu ni Kuwa Kila Akiingia fb Akawa anaona ile Post yake inajipost Upya na Zinakuwa Nyingi!, Baada ya Kupost tena Akiomba Msamaha Hali hiyo ikaisha.

Kwasasa Mdoli huyu Yuko Chini ya 'Jayne Harris' Mchunguzi wa Mambo ya Kutisha Kutoka UK, Hii ni Baada ya Mmiliki wake wa Awali Kufariki kwa Kifua Kubana, Inaelezwa Chanzo Cha Kifo Chake pia ni Mdoli huyu Aliyekua Akimtisha kwa Kumtokea Ndotoni Usiku.

Jayne Anasema Mara Nyingi Hupoteza Documents zake za Kiuchunguzi Kuhusu Mdoli huyu na Huwa Haelewi ni wapi Zinapotelea!. Mara Nyingine Huota ndoto Akipewa onyo Kwamba Asimwambie Mtu Yeyote Kuhusu Majibu ya Uchunguzi Anayoyapata Kuhusu Mdoli huyu na ndiyo Sababu ya Documents zake Kupotea Kimazingara.

Anasema Kunasiku Aliumwa Sana nusu Afe, Alipopona tuu Aliamua Kwenda Kumtupa Mdoli Huyo mbali na Kuacha Kumchunguza, Ajabu ni Kuwa Baada ya Kurudi Nyumbani Akamkuta tena Ndani!. Anasema Anapitia sana Hali za Ajabu Lakini Amezoea kwani Uchunguzi Kuhusu Mambo Haya ya Kutisha Ameuanza Muda Mrefu.

Moja Kati ya Vifaa Anavyotumia Jayne Katika Uchunguzi wake Kuhusu Mizimu ni Pamoja na 'K-II Meter', Hiki ni Kifaa Chenye Mwanga wa Rangi tofauti, Kinauwezo wa Kurekodi Shughuli Zinazofanywa na Viumbe Visivyoonekana Kama Majini N.K.

"Watch at Your Own Risk!"
VIEDO

MWISHO.

@military_Genius
 
Kuweni makini sana ndugu kuna sites ukizifungua na kutazama kilichopo utaingiliwa na mapepo mara moja na unaweza ukateseka sana kuondokana nayo.

Hata huyo mdoli ni mojawapo usijaribu kabisa kuangalia zipo sites nyingi tu ni za kishetani nakwambia utajuta maisha yako kama ukiziangalia.
 
Yaani hakuna mlejesho hata mmoja.. acheni uwoga nyie. Mimi nipo nawasubiri mrejesho.👹👹👹👹👹👿👿👿👿😱😱😱😈😈😈😈👺👺👺💀💀💀💀🕵🕵🕵🕵🕵🕵
 
Back
Top Bottom