Pedesheee A LIYUMBA out

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
Jana Mh DR JK alitangaza kuwapa msamaha baadhi ya wafungwa wapatao 3000 kwa vigezo mbalimbali, lakini kina nikichunguza sioni ni wapi Pedeshee Liyumba amebanwa hasa ukifauatilia hukumu yake si ya kifisadi kwa mujibu wa mahakama na muda wa kifungo ni miaka miwili tu na sasa ameshatumikia mwaka.

Wafungwa wengine wasiohusika na msamaha huo kuwa ni wafungwa waliowapa mimba wanafunzi na kuwakatisha masomo, waliohukumiwa kunyongwa na waliojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Wengine ni wale waliohukumiwa kifungo cha maisha, waliofungwa kwa makosa ya ujambazi, wizi wa magari na waliofungwa kwa kunajisi, kubaka na kulawiti.

Msamaha huo pia hauwahusu watu wanaotumikia kifungo cha pili au zaidi, wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi za Parole ya mwaka 1994 na Sheria ya huduma kwa jamii ya mwaka 2002.

"Wafungwa wengine ambao hawamo kwenye msamaha huo ni waliozuia watoto kupata masomo, waliowahi kutoroka chini ya ulinzi, waliohukumiwa kwa makosa ya uharibifu wa miundombinu kama wizi wa nyaya za simu, umeme, njia za reli na transfoma na wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo kwa msamaha wa Rais na bado wanaendelea na kifungo kilichobaki," imeeleza taarifa hiyo.

Rais Kikwete ametoa msamaha huo akitumia Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka kusamehe wafungwa siku za sherehe za Kitaifa ambazo ni Uhuru na Muungano.
 
Ikiwa ana fall kwenye kundi la msamaha, itakuwa ni haki yake ki katiba.
 
Mkubwa mbona title ya thread yako na ulichokiandika haviendani? Au ndo unavutia wachangiaji? Be a great thinker and not a great winker!
 
Akitoka ndugu \basi ujue uganda imefungwa na kilimanjaro leo
yako macho angalia tbc mpira uone lyumba anavyobaki segerea
 
mkubwa mbona title ya thread yako na ulichokiandika haviendani? Au ndo unavutia wachangiaji? Be a great thinker and not a great winker!

ujui bangi si mpaka uvutie chooni hata kwenye ac inalipuka sikuhizi
 
Back
Top Bottom