Pedeshee Ndama yuko huru mtaani baada ya kulipa faini tsh. 200 milioni

Puyet Babel

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
3,727
2,000
Baada ya kufanikiwa kulipa faini ya milioni 200 hatimae leo mfanyabiashara , Ndama Shabani Hussein, maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe amepata dhamana.

Ndama amepata dhamana baada ya kuwa na wadhamink wawili na kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 600.

Wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimtia hatiani Ndama na kumuhukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya milioni 200 baada ya kukiri shtaka la kutakatisha USD 540,000.

Aidha mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa ilimsomea masharti ya dhamana mshtakiwa huyo iwapo angefanikiwa kulipa kiasi hicho cha milioni 200 ili awe huru katika mashtaka matano yanayoendelea kumkabili mahakamani hapo ambayo upelelezi wake bado haujakamilika.

Katika masharti hayo, Ndama alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na atoe fedha taslimu kiasi cha USD 270,200 ambacho ni sawa na zaidi ya milioni 600 mahakamani hapo ama mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Licha ya kupata dhamana, Ndama amerudishwa gerezani kukamilisha taratibu kabla ya kuachiwa huru.

Hukumu hiyo ya shtaka la sita la kutakatisha fedha ilitolewa baada ya Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa kumsomea maelezo ya awali (PH) Ndama na kuyakubali maelezo ya awali na maelezo yote yanayounda shtaka hilo la kutakatisha fedha, akapatikana na hatiani na kupewa adhabu hiyo.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili Msigwa aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa amekubali shtaka la sita la kutakatisha fedha na maelezo yanayounda shtaka hilo, hawana kumbukumbu za nyuma za makosa dhidi ya Ndama ila ni rai ya upande wa mashtaka kuwa wakati mahakama ikitoa adhabu izingatie matakwa ya kifungu cha 13(a) cha sheria ya kuzuia utakatishaji fedha.

Mfanyabiashara 'pedeshee ndama' arudi uraiani
 

jozzeva

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
2,201
2,000
Jamaa jina lake tu ndio Ndama lakini akili yake ni Fahari au bull yaani ni dume kubwa la Ng'ombe.ongera mkuu kuwa huru.
 

pecial

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
632
500
[QUOTE="Perfectz, post: 21622448, member: 434KWELI DUNIA HAINA HAKI,YANI MIMI FUTARI TU TABU MWINGINE ANATOA FAINI 200M!!!![/QUOTE]
Tena na Mali yenye thamani ya 600M katoa ili apate dhamana
 

impelle

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
804
1,000
Biashara nzuri
Unatakatisha zaidi ya bilioni ,unatiwa hatiani kulipa tsh. 200,000,000/= faida zaid ya mln.800/= ni biashara nzuri
 

Geechie

JF-Expert Member
Oct 26, 2015
976
1,000
Sijawahi sikia mwenye pesa anafungwa,Bali huwa anasumbuliwa tu na misukosuko ambayo inakuja kuisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom