Pedeshee Ndama Mtoto wa ng'ombe Jambazi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pedeshee Ndama Mtoto wa ng'ombe Jambazi!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wa Kwilondo, Jan 11, 2011.

 1. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  JESHI la Polisi nchini linamshikilia mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani (38) au Ndama mtoto wa Ng'ombe kwa tuhuma za kukutwa na gari la wizi. Pamoja na Ndama, wengine wanaoadaiwa kuhusika na wizi huo ni Sylvester Mashindila (45), Richard Marimi (46), Peter Goyayi (30) au Makoye wakazi wa Mwananyamala kwa Kopa na Charles Mwita (43) mkazi wa Kinondoni.
  Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Kamishna Msaidizi wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walipora gari aina ya Hino lenye namba FDIJKD 11185 maeneo ya Tunduma mkoani Mbeya.
  Kova alisema kikosi Maalum cha Kupambana na Wizi wa Magari ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam kilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wanaodaiwa kumnywesha dawa za kulevya aliyekuwa dereva wa gari hilo kabla ya kumpora.
  Alisema gari hilo lilibeba bidhaa mbalimbali vikiwemo vitanda vinne, magodoro, majokofu, makochi na majiko ya umeme ambapo watuhumiwa hao baada ya kutenda tukio hilo walikimbilia mafichoni jijini Dar es Salaam na kuvihifadhi vitu hivyo Mbezi nyumbani kwa Ndama.


  Source: Tanzania Daima
   
 2. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,362
  Likes Received: 3,194
  Trophy Points: 280
  Hawa matajiri wa bongo na hasa wale wa matanuzi sana hela zao nyinyi ni ujambazi na madawa ya kulevya, mtu aliyepata hela kwa msoto wake kwa asilimia kubwa wako makini katika matumizi.
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Pesa za mapaka!
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huenda amenunua tu vitu vya wizi, si unajua wabongo wanavopenda mteremko, hawataki kutumia msuli.
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa (Ndama) si kuna kipindi alikutwa na mifupa ya binadamu akiwa na mwenzie kizaizai?
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kama amenunuwa mali ya wizi, na yeye ni mwizi, tena huyo ndio mbaya zaidi, hawa majambazi wanajuwa kuwa soko lipo la haraka haraka kwa hiyo wanazidisha spidi.
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Ninavyojua yeye na Kizaizai ni madalali wa magari ya wizi
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wabongo tunapenda OVERNIGHT SUCCESS matokeo yake ndio tunaamua kuingia kwenye ishu kama hizo ili uimbwe kwenye mabendi na wakongo waliochoka na kupenda kuandikwa kwenye magazeti ya udaku
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Naam!!! Well said Safari ukienda kununua magari kwa hawa jamaa usije shangaa after few months wamechonga dili ukaibiwa hilo gari halafu likarudi mikononi mwao tena
   
 10. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Utaskia siku mbili kesi imeisha..kisa ushahidi hautoshi
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  PDG NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKITOA TUZO YA HELA KWA FALLY IPUPA
   
 12. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa, mboma polisi walikuwa wakimtafuta cku nyingi. Safari hii kaingia kwenye anga zao.
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Halafu siku hiyo alikuwa na Bodyguard pia sasa nikajiuliza analindwa ili iweje nikasema wabongo tuna kazi kweli kweli
   
 14. S

  Somi JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nilitaka kushangaa ndama wa ng'ombe atawezaje kuiba wakati hata kuzungumza hawezi!
   
 15. Baiskeli

  Baiskeli JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wanakula na wakubwa hao inajulikana. period.
   
 16. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa wengi wao ni wezi,
   
 17. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu hawa sio matajiri ni wezi tu na ni washirikina mbaya niliwahi kumkuta kituo cha polisi stakishari pamoja na mwenzie kizaizai kwa issue za albino na sijui ile maneno iliishia wapi
   
 18. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  huyo body guard nyuma ni dreva wa msofe anaitwa kitobo...dugu moja!
   
 19. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  Ishu zao zipo pale Polisi Oyesterbay wnajuana sana na mapolisi wanakula nao ukitaka kujua vikao vyao huwa kwa Macheni, mango Garden, PR Camp, The Billionea club, ni group kubwa, wamo pia na wakina msofe lakini hawa ishu za magari hawafanyi wao ni Noti feki, Unga na madin feki, hipo haja ya jeshi la police Oyster bay kubadilishwa lote pamoja na wapelezi wao, ukiwata kuwakata utakapoona group la wazaire wakiomba pesa pale Makaburini Soko la TX , kuna mambo mengi kinondoni kuna watu wanakesi ya kukutwa na bastola alafu zinaisha hivi hivi kuna jamaa mmoja anaitwa gasto huyu kwa kuchong afunguo na kutishia kuu ili anyanganywe ndio zak lakini hajawai kukamatwa, kweli kinondoni kunatisha
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  No wonder ni Kada wa CCM!
   
Loading...