Pedeshee Ndama akwepa kifungo kwa kulipa faini ya milioni 200

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
MFANYABIASHARA Ndama Shaban Hussein maarufu kama Ndama Risasi au Ndama Mtoto ya Ng'ombe, jana aliachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana na kulipa faini ya Sh. milioni 200.

NDAMA NDAMA.jpg
Ndama alipata dhamana hiyo baada ya kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Dola za Marekani 270,195 (sawa na Sh. milioni 594.4) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Ndama pia alipata dhamana hiyo baada ya kulipa faini ya Sh. milioni 200, adhabu aliyopewa na mahakama kutokana na kukiri kosa la kutakatisha Dola za Marekani 540,000 Juni 9, mwaka huu.

Awali Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaotoka taasisi ya serikali au inayotambulika, kutoa mahakamani Dola za Marekani taslimu 270,195 (sawa na Sh. 594,424,000).

Juni 13, mwaka huu mshtakiwa alilipa faini ya Sh. milioni 200 na jana aliwasilisha hati za mali yenye thamani ya zaidi ya Sh. 594.

Mbali na shtaka la kutakatisha fedha, pia anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonyesha kuwa kampuni ya Muru Platinum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha makasha manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 ya thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Pia anadaiwa Machi 6, 2014, Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonyesha kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

Aidha anadaiwa Februari 20, 2014, alighushi fomu ya forodha yenye namba za usajili R.28092 akionesha kampuni ya Muru imeilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dola za Marekani 331,200 kama kodi ya uingizaji wa bidhaa ambazo zina uzito wa kilogramu 207 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kutoka Congo.

Shtaka lingine anadaiwa Februari 20, 2014, alighushi nyaraka ya bima kutoka Phoenix of Tanzania Assurance Company Ltd akionyesha kampuni ya Muru imeyawekea bima maboksi manne yaliyokuwa na dhahabu hizo.

Anadaiwa kati ya Februari 26 na Machi 3, 2014, Dar es Salaam kwa njia ya udanganyifu alijipatia kutoka kwa kampuni ya nchini Australia ya Trade TJL DTYL Limited Dola za Marekani 540,000 baada ya kudanganya atawapa na kusafirisha dhahabu hizo.

Chanzo: Nipashe
 
Pia Akina mramba na yona nao wamefungwa kifungo cha nje ..

Masikini hana haki duniani kama unabisha nenda ukonga ukashuhudie
 
Hawa wa janja wangeachwa tu kwani Hawaiibii nchi... miwaziri iliyopita ndio imeumiza watu... huyo angekuwa anauza madawa ya kulevya ningemlaani
 
Pedeshee ndama mutoto ya ng'ombe..yuko vizuri
 

Attachments

  • IMG-20170615-WA0062.jpg
    IMG-20170615-WA0062.jpg
    100.1 KB · Views: 34
TZ bwana kesi ya kutakatisha zaidi ya sh bilioni moja mtu anahukumiwa faini ya milion 200
 
TZ bwana kesi ya kutakatisha zaidi ya sh bilioni moja mtu anahukumiwa faini ya milion 200
Mkuu awamu hii inataka kukusanya fedha kwa njia nyingi kadri iwezekanavyo; kwenye matetemeko, misiba na hata kwenye kutakatisha fedha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom