Pedekezo: Uzi Maalumu; Kwa wale walio na matatizo mbalimbali ya kiafya, Uliza swali au tatizo linalokusibu na madaktari wetu wa j forum Watakusaidia.

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,818
2,000
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Natumai mu wazima Mkiendelea na ujenzi wa Taifa Tanzania kwa walio Dhaifu Mungu awape heri.
Samahani sana Moderators ninapenda kutoa pendekezo kulingana na kichwa kinavyojieleza ili kuweza kisaidia member mbalimbali ambao wako na matatizo ya kiafya waweze kupatiwa ufumbuzi juu ya changamoto za kiafya zinazowakabilu kutoka kwa madaktari walioko humu jamvini.

Mpango unaweza kwenda hivi.
Kwanza kabisa kwa wale ambao ni wahudumhmu wa Afya au wataalamu wa Afya kwa ridhaa yao waweze tambulikana pamoja na sehemu walizobobea.
Ili kwamba member akihitaji ushauri au usaidizi wa kiafya aweze kumtag kwenye reply then mhusika aliyekuwa tagged anajibu au hata mwingine ataeona kama iko ndani ya uwezo wake anaweza saidia.
Kwa hio hapa chini kuwe na list ya wataalamu wa afya na sehemu walizobobea wakitaka.
Hili wazo lilinijia kutokana na kwamba unaweza kuta uko mbali na huduma za Afya. Alafu ukapata changamoto, na kumbe io changamoto si kubwa ukipata ushauri.
Kama inawezekana itakuwa good thing.

Ila samahani kwa mpangilio Mbovu. Kama hili linawezekana inaweza fanya namna nzuri, ili ieleweke kwa kila mmoja.
Natumia wahusika watafanyia kazi..!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom