PD 8: CCM kutuongoza kwenye mabadiliko tuyakatayo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PD 8: CCM kutuongoza kwenye mabadiliko tuyakatayo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 26, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Ukweli umebakia kuwa ukweli CCM bado inapendwa na kukubalika mijini na vijijini. Hili halina shaka. CCM kuweza kuendelea kutawala bado kupo kwa miongo kadhaa ijayo. Hilo nalo silishuku sana. Kwamba, kizazi kipya cha viongozi wa CCM kinazidi kupanda taratibu hilo nalo halina shaka.

  Kwamba lengo la Chama cha Mapinduzi liko wazi kabisa kwa mtu yeyote kulielewa. Siyo lengo la kubuni, kuhisi au kulikisia. Lengo hilo kubwa limeanishwa katika Ibara ya
  Hilo ndilo lengo la kwanza la CCM kwani kutoka hapo malengo mengine yanafuatia. Kwa kulinganisha hata hivyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeyagawa madhumuni yake sehemu kubwa tatu (ya kisiasa, ya kiuchumi na kijamii). Katika madhumuni ya kisiasa yapatayo 6 hakuna lengo la "kushinda uchaguzi mkuu au wa serikali za mitaa". Hili ni muhimu kwani malengo mengine yote yanategemea kwa chama kuwa madarakani!

  Hii ina maana ya kuwa CCM kama chama kinajua kabisa hakiwezi kufanya jambo lolote na hakiwezi kutekeleza sera yoyote bila kuweka kipaumbele chake sawa. Kwao kushinda uchaguzi ndio msingi wa mambo mengine yoyote na kutokana na hilo watafanya lolote wawezalo kuhakikisha wanashinda hata ikibidi kutumia njia za panya, hadaa, au mbinu za kisiasa ambazo zimekuwa zikizaa matunda. Siwalaumu kwani wanajua lengo lao la kwanza ni nini!

  Tukilielewa hili tutaelewa kuwa si rahisi kuiondoa CCM madarakani au kuinyima nafasi ya kutawala. Ni sawa na jaribio la kumkamata simba mwindaji nyikani ili afugwe kwa maonesho au kujaribu kumtoa samaki majini ili umfuge kwenye chupa!

  CCM haitoachia madaraka kiurahisi, haiwezi kuachia madaraka kwa sababu tungependa ifanye hivyo, na kwa haki haipaswi kuachia madaraka kwa sababu kuna watu hawaipendi, no sir! CCM kama chama cha siasa kina sababu, haki, na nia ya kung'ang'ania madarakani kwa muda mrefu na kwa mbinde au kwa upinde. Ndiyo historia ya watawala wote duniani.

  Hivyo mabadiliko basi yatakuwa magumu.

  Mabadiliko hayaji kiurahisi na CCM hakiwezi kutengeneza mazingira ya mabadiliko ambayo yatasababisha chenyewe kiondolewe madarakani. Kama chama kimejifunza yaliyotokea Kenya, Zambia na Malawi, kimejifunza yaliyotokea Zimbabwe na hakiko tayari kurudia makosa yale yale. CCM kitakkuwa ni chama cha wapuuzi na wajinga endapo kitasababisha na kusimamia mabadiliko ambayo yatasababisha chenyewe king'olewe na watoto wake wakae pembeni ya meza kuu ya utawala na ulaji. Hapana ma'am, CCM haiwezi kufanya hivyo hata taifa zima likiwa usingizini.

  Kwa upande mwingine hata hivyo, CCM inaweza kabisa (naamini ndivyo inavyopanga) kufanya mabadiliko ya kukifanya kikae madarakani zaidi na kukubalika zaidi. Mabadiliko hayo si mengi wala si makubwa. Kinahitaji kufanya mabadiliko ya ishara na alama; mabadiliko ya picha na sauti. Mabadiliko ya nyimbo na kibwagizo. Kwa wengine mabadiliko hayo yanatosha kabisa.

  Pamoja na hayo kuna mabadiliko ambayo CCM haiwezi kuepuka kufanya kwani kutofanya hivyo kunatishia uhai wa chama chenyewe. Mabadiliko haya yanategemea sana nani atashinda katika siasa za ndani za chama (intraparty politics). Katika makala yangu moja ya kesho nimetuma ujumbe wa wazi kwa kiongozi mmoja wa CCM ambaye kambi yake inaamini itashinda siasa hizi. Endapo upande wa mtu huyo utashinda, basi CCM itajikuta inalazimishwa kubadilika na kufungua uwanja wa kushindwa kwake.

  Lakini ninaamini upande huo hauwezi kushinda kwani tuliyoyaona Busanda yametuma ujumbe wa wazi kuwa bado CCM inaweza kushinda bila upande huo.

  Kwa wale wengine wanaotaka mabadiliko ni lazima watambue kuwa tunaweza kupoteza kita kimoja kimoja lakini tukashinda vita. Dalili za upepo bado zinaelekea upande wa mabadiliko ya kweli. Japo pole pole. Kama merikebu iendayo pole pole na kupigwa na upepo, ndivyo hivyo hivyo mabadiliko tuyatakayo yanavyokaribia. ni mabadiliko ya fikra kwanza, kabla ya mabadiliko ya kura.

  Busanda, Tarime, Mbeya Vijijini, Kiteto na hadi Tunduru kote kumeonesha kuwa mabadiliko ya fikra yameanza, kama vile cheche mbugani, na kama vile manyunyu ya mvua ndivyo hivyo hivyo moto mkubwa utaanza taratibu, kama kwa ukimya huku mlio wa majani kuungua na harufu ya nyasi kupaa ndivyo itakavyokuwa.

  Tusiwe na haraka wala papara; tusikate tamaa wala kujiona duni. Mabadiliko tuyakatayo yanakuja, labda pole pole sana kuliko ambavyo tungependa. Tungependa mabadiliko yawe "sasa". Tungetaka kila uchaguzi mdogo wapinzani "washinde". Tungependa kuona CCM inaumbuka na kuabika mbele ya wapiga kura. Njozi hizo mara kadhaa sasa zimezimwa kama mtu ambamizapo mbu ukutani; na kama aliyekanyaga sisimizi ndivyo matamanio hayo yamefutwa katika mioyo yetu.

  Ni mwoga hata hivyo atakayekata tamaa, ni dhaifu ambaye anajisikia kushindwa, ni mwongo ambaye hauoni ukweli uliopo mbele yetu. Moto wa mabadiliko umeanza, upepo wa ushindi unavuma taratibu, na sauti za mashujaa wapambani zinasikika kwa mbali; Vinakuja, kama vile kutoka upeoni tunaweza kuona moshi wake. Vinakuja, kama king'ora cha utangulizi vinasikika; vinakuja, kama nyota ya alfajiri kumulika. Hakuna atakayaweza kuzuia, siyo CCM wala makuwadi wa ufisadi.

  Yawezekana hivyo, CCM ndiyo ikawa chanzo cha mabadiliko hayo. Yawezekana CCM ikawa ndilo tumaini la mwisho la vita dhidi ya ufisadi, yawezekana CCM ikawa ile merikebu tuitakayo, sitoshangaa. Nimekulia ndani ya CCM, nimejifunza itikadi yake, naijua misingi yake, na naijua vyema kuweza kuamini, kuwa yawezekana kabisa mabadiliko tuyatakayo yataletwa na CCM.

  Nafahamu hiyo ni orodha ya "yawezekanayo". Lakini, pia yawezekana kabisa kuwa CCM ndiyo kizuizi kikubwa cha mabadiliko hayo. Jukumu letu basi ni kutambua kipi ni kipi na kukifuatilia kwa nguvu zote.

  Binafsi naamini mabadiliko ya kweli yatatoka na yataletwa na Watanzania wenyewe. Yataletwa kwa machozi na kupolekewa kwa kicheko. Bado hatujalia vya kutosha ingawa tunataka kucheka sana. Bado hatujachubuka miguu kwa kutembea na kuota malengelenge kwa kukimbia. Bado Watanzania hawajaonja uchungu wa utawala wa kifisadi. Tunaishi katika ulimwengu wa kufikirika. Bado hatujakasirika vya kutosha (mabadiliko yote ya kweli asili yake ni hasira!). Bado hatujadhalilika vya kutosha.

  Tusikate tamaa, tusipepese macho, na tusirudi nyuma kwa kujisalimisha isipokuwa kwa kujipanga tena. CCM wataendelea kusonga mbele kama mashujaa walioshinda, na wanastahili kusonga mbele. Wataendelea kusogea zaidi hadi watufikishe mahali ambapo hatuwezi kurudi nyuma tena. Hapo ndipo songombingo litakapoanza, hapo ndipo sauti za wapiganaji wa kweli na mashujaa wasiosalimu amri zitakaposikika, kwani ni hapo ndipo tutajua kuwa tunachopigania ni zaidi ya sisi kusimama, tutakuwa tunapigania uhai wetu na urithi wetu.

  Mapambano haya siyo sawa na mbio za mita 100; hii ni marathoni. Si mapambano yanayofikiria 2010 au 2015, ni mapambano yanayoangalia 2020 na baadaye. Kwa wenye pumzi ndogo ni bora kukaa pembeni; wenye haraka ni bora wakafanye jambo jingine, na wenye pupa ni bora watulie watazame.

  Kesho, ni mwanzo tu! Inua kichwa chako, simama wima, tazama mbele na acha kumung'unya maneno. Jifunge mkando wako. Kuna mapambano mbele. Huwezi, rudi mstari wa nyuma, umeshindwa kaa pembeni, hutaki jiondoe. Vinginevyo. Aluta continua!

  Mwanzo tu huu.. bado mapemaaaa!!

  NB: Gazeti lolote linaweza kutumia makala hii.
   
  Last edited: May 26, 2009
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkjj ni ukweli hakuna haja ya kukata tamaa kama hii PRI ya Mexico ilitawala miaka 70 na bado ikaja kupigwa bao na muelekeo ukiwa kama huu wa chama chetu kikuu. Time shall come and not that late!!!!!!!!!!!!

  " For two decades, however, the PRI's strength has declined. Until the 1980's, the party consistently received 70 percent or more of the vote in national elections. But according to a Government analysis of recent elections and polling data, the PRI could count on 42 percent of votes if national elections were held today. The combined votes of the two largest opposition parties would total nearly 52 percent, the study found.

  In fact, the PRI's greatest strength is the opposition's fragmentation into two large parties of nearly equal strength. In recent days the two parties' likely presidential candidates, the leftist Mayor of Mexico City, Cuauhtemoc Cardenas, and the populist governor of Guanajuato State, Vicente Fox, have endorsed putting aside ideological differences to mount a single opposition candidacy. But the legal and political obstacles appear great.

  ''The key for the PRI to win in 2000 is to avoid a split in its own ranks that could siphon off PRI votes,'' said Agustin Basave, a former PRI deputy who has written a party history"
  - Source NY times - March 4, 1999

  We will too make a history some day!!!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unajua na PRI.. ni Chama cha Mapinduzi pia.. ?
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Wazee
  Wala msiwe na homa kwa sababu aliyeshinda Busanda si CCM. Mshindi ni Chadema. Kapanda kutoka 4% mwaka 2005 mpaka 42.7 mwaka 2009. Katika hili si lazima mshindi achukue jimbo.
  Mshindi wa pili ni Malecela na mkewe pamoja na Magufuri. CCM yenyewe ilishindwa na ndipo ikawaomba hawa. Walipokuja, mambo yakaanza kubadilika. Maana yake ni kuwa CCM haipendwi, wanapendwa watu fulani. Hawa hawakwenda Tarime na matokeo mliyaona. Walikwenda Mbeya, matokeo mliyaona.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  May 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Mkuu wangu CCM haiwezi kukuongoza wewe katika mabadiliko uyatakayo.. Unaweza sana kutumia neno TUYATAKAYO lakini ukweli utabakia kwamba ni wewe na wengine wachache wasiofahamu kwamba wananchi wanakichagua chama hiki kwa sababu wanaanmini chama kinawapeleka wakutakako!..Na hayo wayatakayo ni pepo wakisha fika (kufa) ndio watayakuta..

  Nitarudia kusema kwamba Uongozi wa CCM leo hii ni Progressive toka Mwinyi, Mkapa na hadi Kikwete ambao wamekuja tengana tu kwa sababu za Ubinafsi lakini wote wanaamini KUIUZA NCHI yetu ndio solution. Itikadi inayowaongoza woite hawa ni sawa sawa.. wewe na mimi tu ndio hatuelewi..
  Ukitazama mambo yote yanayopingwa na wananchi wengi ni kuuzwa kwa nchi, mafisadi ni matokeo ya kuuzwa kwa nchi,jambo ambalo wapo watu wanaamini linaweza kuondoka ikiwa sheria itafuatwa.. Sheria ipi? hakuna anayeweza kujibu kwani unapouza nchi kuna mikataba ambayo ni lazima ifuate mrengo wa waumini.. Miremngo ambayo ndiyo inafungua miaya hii ya Ufisadi.
  Hivyo yale uyatakayo yanaweza kufikiwa tu ikiwa unaamini kwamba mfumo huu wa Progressive ktk mazingira yetu unaweza kufanya kazi..Na ni katika kutazama mrengo huu ndipo unaweza kuona kule mnakokwenda ili kuifikiria hiyo pepo ya Uyatakayo!
  Hivyo nadhani ni muhimu sana tusimtazame Kikwete kama kiongozi kwani binafsai naamini kabisa anafanya mengi ambayo yanakubalika ktk mfumo huo. Swala la Ufisadi halina dawa isipokuwa tofauti inaweza kuletwa tu ikiwa tunabadilisha mlengwa wa mikataba na urithi wa mali zetu.

  Nitawaomba samahani wanawake (hasa Mama na WomanofSubstanc) kwani nataka kutumia mfano mmoja..

  Huwezi kupambana na Ufuska ikiwa kuna wanaume wanawezeshwa kununua kitendo hicho unachokichukia.. Kuwasaka na kuwafunga wanawake Malaya haiwezi kuondo ufuska ikiwa tunashindwa kuwataza wanaume wanaoshiriki ktk maswala haya na tunashindwa kuwa empower wanawake wetu ktk ajira na uwezo wa kujitegemea... Hivyo ndivyo hali ya mwananchi wa Tanzania chini ya Progressive.. ni sawa na mwanamke malaya ambaye kila siku hutafuta nafasi kama hizi kuingia ktk Ufisadi kwa sababu hawaoni ndani (no other option)..Na kuendelea kuwasaka mafisadi wakati serikali bado inaendelea kuwanunua kwa fedha zao sidhani kama tunaweza kuondokana na adha hii..
  Swala ni kuwatajirisha wananchi, wananchi kuwa mbele ya kila fikra za utajiri wa nchi hii kama mtu aliyeko ktk ndoa..Family comes first.. Tuondokane na zile hulka au imani kwamba mwanamme anayenunua ngono huwa hana makosa ila makosa ni ya mwamamke anayeuza mwili wake..Hii ndio imani ya wananchi wengi kwamba serikali haiwezi kuwa na makosa ktk Ufisadi ila wale wanaouza kina Karamagi... na kitu kinachofanyika ni kuwafukuza au kutengua mkataba imetoka, hasara ya Taifa na Wananchi -Watajiju!
  Nje ya hapo mkuu wangu, hufahamu ukitakacho kwani CCM inafanya mengi Wayatakayo wafuasi wake..
   
 6. T

  Tom JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ktk mfano wako naunga mkono serikali na kina Karamagi wote wametukosea lakini pia naona Mwanaume anayefanya ngono lakini bila kulipia malipo yanayofaa ndio mbaya zaidi kwa jamii kuliko hata huyo mwanamke malaya, hivyo makosa ya kina Karamagi ni zaidi ya makosa ya serikali. Kina Karamagi waadhibiwe na warudishe walichoiba ama kuipunja serikali na faida juu.
  Kama ni kwenda jela basi mwanamke malaya ni miaka tatu na kazi ngumu lakini huyo mwanamume anayefanya ufuska kwa dezo ni faini, miaka kumi jela na kazi ngumu.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mkandara, na wewe na mifano yake matokeo yake ndiyo haya.. maana mfano utapelekwa mbali kweli maana nikifikiria maswali yanayoweza kuibuliwa katika mfano huo..
   
 8. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mwanakijiji/Mkandara, hoja iliyotolewa na Mwanakijiji hapo juu ni hoja yenye mapana na inayojielezea yenyewe.

  Kwa mtazamo wangu, CCM inawajua wananchi wake. Inajua tamaa za wananchi na hulka zao. Inajua mipaka ambapo inaweza kuitumia kabla tu haijawakifu wananchi wake. Zingatia yafuatayo;
  1. Uhuru wa kujenga holela
  2. Uhuru wa kutembea bila kikomo. Siku hizi wanaokaa vijiweni sio wazururaji
  3. Ushiriki mdogo wa wananchi katika kazi za ujenzi wa Taifa. Serikali imechukua jukumu zito la wananchi kujenga miundombinu, kulinda mazingira n.k
  4. Uwezekano wa kuishi (maisha ya wastani) bila kipato halali au kinachoeleweka (hata mijini)
  5. Uwezekano wa kufanya biashara bila kuwa na leseni, kulipa kodi, n.k

  Mkuu mapungufu ya kiuongozi yaliyopo, ndio chachu ya CCM kuendelea kuwepo madarakani, na itaendelea kuwa hivyo hadi hapo serikali itakapoamua kubadilika na kuanza kutawala kwa kufuata sheria. Kumbuka kauli za Mhe. W. Ngeleja kule Busanda alipokuwa akiongea na wachimbaji wadogowadogo. Aliwaambia (bila kunukuu) kuwa endapo CCM itashindwa, watatumia TRA na pia watafuta leseni zao za uchimbaji. Hivyo ndivyo wafanyabiashara wengi wanavyoona CCM inawafaa (pale wanapoachiwa kuendelea kujipatia kipato bila kutimiza masharti mbalimbali ya usajili na kodi). Na hili ndilo chimbuko la umasikni wetu. Inavyoelekea ni kwamba ama wananchi hawajui kuwa umasikini unasababishwa na wao wenyewe, ama hawajali.

  Kwa mawazo yangu pia, mtikisiko mkubwa kabisa unaoweza kuipata CCM katika uchaguzi mkuu ni wa kupoteza majimbo mengi ya Ubunge (<50%). Sioni dalili za wazi za CCM kupoteza kiti cha uRais (walau katika kipindi cha miaka 20 ijayo). Sorry to say this. CCM wanalijua hili. Sababu za hili ni kwamba, wapinzani hawajiamini kiasi cha kuiondoa CCM kwenye kiti hicho, upinzani unashirikiana na CCM katika kushindwa kukichukua kiti hicho, ama CCM inajua jinsi ya kukikwepesha kiti hicho kutoka mikoni mwa wapinzani. Vile vile, mfumo mzima umeandaliwa kuwezesha CCM kushinda hata wasipopata kura za kutosha katika uchaguzi mkuu.
   
 9. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu Recta yani right on a point kuna sababu ambazo zinafanya watu wachague CCM na hizo ulizozitaja ndio hasa Watz wanachotaka na ndio mana wanachagua CCM yani nchi hii kitu kinachoitwa kufuata sheria ama taratibu ni utamaduni wa kigeni sana..! hakuna anaetaka kufanya hayo!
   
 10. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #10
  May 27, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  CCM hajatuongoza kwenye mabadiliko tuyatakayo kwa miaka 48, miaka 48 ijayo haitaweza pia. Wawapishe wengine nao wafanye kazi hiyo. Lakini si hawa wanaojiita wapinzani.... mimi nawaona wapinzani uchwara! Wizi mtupuuuuu!
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  May 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Mkuu mifano yangu mara nyingi huwa ni hali halisi namara zote ni kulingana na mazingira yetu..
  Sasa tazama basi ukweli wa mambo..labda hukunielewa...Nitaendelea kukuchekesha zaidi na mifanoi yangu.. haitakwisha makali yake..

  Ni kweli kabsa wanaume kama kina Karamagi wanatakiwa kufungwa, wanatakiwa kuchukuliwa kama wahalifu lakini sio Tanzania na njdio maana leo hajashughulikiwa kabisa kwa sababu ni mila na desturi yetu kwa mwanamme malaya kutokuwa mkosefu isipokuwa mwanamke..Now, unapojiuliza kwa nini kina Karamagi na wengine wote mafisadi imeshindwa kuwafikisha mahakamani sababu ni hizo mila zetu..Hakuna tafisri wala matumizi ya neno malaya kwa mwanamme..ajabu, ni sifa fulani tofauti na mwanamke..

  Lini umeona mwanamme akifikishwa mahakamani kwa makosa ya kutembea na mwanamke Malaya?... never! na wala yeye hataitwa malaya kwa kuwa mshiriki wa kitendo hicxho isipokuwa mwanamke tu..Why? hakuna sababu wala mjadala..pamoja na kwamba sisi wote tunakubali makosa ya wahusika kulingana na vitabu, lakini ktk utekelezaji wa kisheria utaambiwa leta ushahidi..ama kuwa wa kwanza kurusha jiwe kinyume cha hoja ya Yesu..ambaye aliwabana wanaume waliotaka kumhukumu mwanamke!..Kumbuka hata wao hawakuamini kwamba mwanamme ana makosa..
  Yule Maria Magdalena aliitwa Malaya wakati mwanamke hawezi kuwa malaya bila kuwepo mwanamme, meaning wale waliotaka kumhukumu ndio wao walikuwa wanunuzi..They were guilty as she was!..hilo ndio somo kubwa la aya ile na Nabii Issa (Yesu)..

  Kwa hiyo ndio maana kesi zote za Ufisadi nchini huwa zinakufa na mwanamme siku zote huonekana victims wa mvuto wa mwanamke..Ni exaclty hali inayotokea Tanzania ktk vita ya Ufisadi mkuu wangu... wanaohukumiwa na kupigwa mawe ni wanawake kimaisha..

  Tunawajua Mafisadi, tunayajua wanayoyafanya wakiwa vyumbani na the so called malaya, lakini hatuwezi kuwashtaki wao kwa sababu hatuna ushahidi kuthibiti uchafu wao ila wa mwanamke malaya ndio wazi na unaokubalika. Haya huo ushahidi mkuu wangu uta ukusanya vipi wewe uliyeko nje ya chumba?..Haiwezekani, huwezi kuwa na usahidi unless nawe ulikuwa chumbani wakati vitendo hivyo vikifanyika..kitu ambacho unawaona kina Rostam wakiwarushia hoja hizi kina Mengi, Mtikila, Dr. Slaa na wengineo..kuonyesha tu kwamba hata wao walikuwa vyumbani..Je, walikuwa wakifanya nini kama nao sii Mafisadi!.. Huu ndio uchefuchefu wa siasa zetu tunaozunguka nao kutwa kucha.

  That's whats Up!..CCM inakupeleka kule watakako wengi.. mwanamme hana hatia ktk swala la ndoa isipokuwa ni makosa ya mwanamke malaya..Hivyo - mawili, join them au tafuta nchi nyingine ukaishi lakini nakuhakikishia Ufisadi hauwezi kupigwa vita hadi siku tutakapo kubali kwamba mila na desturi za chama CCM zinakumbatia itikadi chafu..Itikadi zinazotazama upande mmoja tu wa makosa hayo..wakifanya wao hakuna makosa hadi siku utakapo wakuta kitandani na malaya na u collect ushahidi..Sijui Upi huo!..Pia uweze kujibu wewe ulikuwa ukifanya nini chumbani..
  Kifupi tuachane na fikra za CCM kutufikisha tukutakako.. haiwezekani kilichobakia aidha tuwe mashoga tushangilie makamuzi au kurudi ktk dini tukamwogopa Mungu na tukubali yaishe..Ni Chaguo lako...
  Hukumu tumwachie Mungu!
   
 12. Joyum

  Joyum Senior Member

  #12
  May 28, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka Nyerere alisha sema upinzani wa kweli utatoka CCM, sina hakika sana ni katika hotuba ipi lakini kwa ujumla hali inavyoonekana, CCM bado itakuwepo madarakani kwa kirefu. Kitu kimoja tu tunachotakiwa kujua, itafikia mwisho hata hao wanaojiita CCM damu damu watachoshana wenyewe kisha tutayaona mabadiliko halisi na si haya wanayotufanyia maigizo siku hadi siku.
   
Loading...