Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,429
Waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga amekana kuhusika kabisa na kampuni ya Lugumi ambayo kwa sasa inakabiliwa na kashfa nzito ya rushwa na uhujumu uchumi ambayo ilipewa tenda ya kufunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole kwenye vituo vyote vya polisi kwenye Wilaya zote nchini na kushindwa kukamilisha tenda hiyo.
Juhudi mbalimbali zinazofanywa kuujua ukweli wa sakata hili umepelekea taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini(TAKUKURU) kutoa tamko la kuifungulia kesi mahakamani kampuni hii ya Lugumi pamoja na jeshi la polisi na kufanya uchunguzi wa kina wa sakata hili.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) imewaita bungeni IGP pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo watakuwa na kikao leo bungeni Dodoma na baadae baada ya kikao hicho ndipo wataweza kuongea na waandishi wa habari kuhusu suala hili.