PCCB: Tuna manufaa nayo?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
What did the PCCB Act target?

THE dust is beginning to settle since the bilateral discussion between editors and other media stakeholders on one hand, and the director of the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) on the other.

What transpired was a sure sign that something has changed, that from its earlier position as a source for plenty of what this or any other investigative newspaper was doing, the PCCB is now marking out its territory. This shift in sentiment falls in line with changing atmosphere that government as a whole is becoming a bit edgy or shifty as it faces questions from all sides, suddenly.

They say in Kiswahili ’panapofuka moshi panaficha moto,’ in which case there is little reason for the government and ruling party to resort to ’smoke brigade’ measures each time something comes up, insisting that there is no fire. That is what happened last week in Parliament when Kigoma North MP Zitto Kabwe was spelt out his marching orders for more or less one hundred days out of the legislature. It is in the same vein that PCCB has declared that no corruption exists in the Richmond deal, and now clause 37.1.

This particular provision, were it to have started to apply immediately and take up all interesting subjects being investigated by newspapers, would lead to a blackout on most investigative reporting.. But as the provision shows, it is entirely up to PCCB to decide what it must now put a stop to its being reported by newspapers, save in the auspicious event of a statement by the PCCB spokesperson, or a grand interview with the director general. The press doesn’t live with such ’investigative reporting’ so it counts its chicks.

As one editor pointed out at the media-PCCB meeting, for all practical purposes the anti-corruption watchdog has fully, entirely ended its role as a collaborator in informing the public on corruption or investigating leads, and into an adversary. It is doing so because donors forced the organ to play a higher role than it was designed to do, having to follow up and prosecute cases of grand corruption, and it will be remembered that Denmark withheld 4.7bn/- due for its budget support for 2007/08 until the PCCB law was approved in Parliament. This sort of pressure was rather high for the government, so it adopted the legislation to get donor aid.

Under such circumstances it should have been expected that the government was going to put the necessary safeguards on the Act, to ensure that it isn’t compelled to prosecute this or that case because of ’great public demand.’ That means where a case is beginning to weigh a little heavily on it, then such a case will have to undergo a media blackout, and this way only ’low key’ or ’low intensity’ cases of presumed corruption will be getting media coverage. That might be sufficient for the government, not to put a blackout on the manner public coverage occurs but creating ’safe areas’ in some key investigated matters.

That is why an impression is being created that only one major case that has caught the public eye for a while was expressly targeted under 37.1, namely the radar deal question whose investigation could become embarrassing for top level authorities at some date. It is probably in government interest that some shadowy figures named in the deal, who it seems were picking flying habits a bit uncharacteristically, continue flying or be coming back slightly unnoticed. Saying they were here the other day would amount to an offence.
 
Wanatakukuru,
11.09.2007

Mkurugennzi Mkuu,
Takukuru,
S.L.P 4865
Dar es Salaam

Yah: kilio cha wanakukuru tanzania

Tunapenda kuchukua fursa hii kwanza kukupongeza kwa kuteuliwa na kisha kuapishwa kwako kama mkurugenzi mkuu wa takukuru. Hongera sana.

Ni kwa uteuzi huo tunaamini mhe. Rais akisaidiana na wasaidizi wake waliona ni busara wakuteue ushike nafasi hiyo nyeti kwa kuamini unao uwezo. Hii haina maana kuwa wewe ni bora kuliko watanzania wote na haina maana kuwa wewe ndiye mwenye akili watu wote. Hapana. Ni busara tu zilitumika katika kuhakikisha chombo hiki nyeti kinapata mtu wa kukiongoza. Na lazima awe mtu mmoja. Na hatimaye ukawa wewe. Tunakupongeza.

Kinachotusikitisha sisi juu ya mwenendo wako
Si vizuri sana kwetu sisi kukuandikia barua kama hii lakini tumelazimilika baada ya kuona unakotupeleka kama kiongozi mwenye dhamana ya nchi hii siko.

(i) Utakumbuka mwezi wa nane mwaka huu ulikuja marangu pamoja na kufunga mafunzo bali pia kutufundisha kwa mujibu wa ratiba. Ni mengi na kwa nyakati mbalimbali uliyaongea lakina yaliyotuumiza ni kwanza pale mmoja wetu alipokuuliza swali zuri tu na wewe badalia ya kulijibu uling`aka “umetumwa siyo?” Unakumbuka vizuri swali lilihusu oc unayotuma kwetu hasa wilayani kuwa ni ndogo kitu ambacho ni kweli na alitaka kujua ni nini kanaendelea. Kwetu hilo halikuwa jibu sahihi na hasa kutoka kwako kama dg. Eti katumwa. Katumwa na nani?

(ii) Utakumbuka pia ulivyotumia muda mrefu kuwaponda wasaidizi wako kwa maana ya wakurugenzi. Ulithubutu hata kuongea mambo ya ndani ya familia zao kuwa ati hawapati unyumba majumbani kwao na ndiyo maana kutwa nzima wapo ikulu kupeleka majungu. “…ukiona mtu anavaa suruali inayombana kutwa nzima ikulu kunisemea jua kwake mkewe hampi unyumba… elewa mke wake anatembea nje…mimi ndiye ninaye gawa fedha zote za takukuru. Na sanasana research moja au mbili kwa mwaka zinatosha. Yakija maombi mengine napiga chini….. Kazi kuendekeza ushirikina tu”

Haya ni baadhi ya mambo uliyoyaongea na mpaka sasa sielewi kama nayo yalikuwa ni sehemu ya uliyotakiwa kutufundisha na ili tukayafanyie nini. Kama ilitokea tukacheka au kutabasamu kwa uliyokuwa ukiyasema ni kuwa tuliona ni upuuzi mtupu. Kinachotuuma zaidi ni kuwa hujakua wala kukomaa akili pamoja na madaraka makubwa uliyopewa na rais. Inafika mpaka mahala tunadhani una matatizo ya akili. Si bure. Yaani wewe kama dg unawezaje kusimama mbele ya watu unaowajenga kuwa viongozi na kuanza kuongea ujinga kama huo? Masuala ya wakurugennzi wako kutopa unyumba majumbani kwao wewe vinakuhusu nini? Je, una uhakika kuwa hawapati unyumba? Na je hili ni sehemu ya unayotakiwa kuyasimamia kuhakikisha watumishi wako wanapata unyumba?

Ni wewe unayetishia watu ati umatandao kuwanasa wanaokusema vibaya ati ni majungu na kwamba utapambana nao. Je nani mwenye majungu kama si wewe?
Kama hukuwa na kitu cha kutufundisha ni bora ungebaki kwa mkeo. Ukweli ulitupotezea muda kwa kuja kwako. Sana sana umetusaidia kukufahamu zaidi wewe ni mtu wa aina gani?

(iii) ulikuwa mstari wa mbele kulaumu dg aliyestaafu ati alileta makundi. Kwanza ni makundi gain mzee wa watu aliyaunda kama si kutaka kumpakazia tu? Ukweli kwa muda mfupi uliokaa madarakani umefanikiwa kujenga makundi tena ya uhasama ndani ya chombo. Umefanikiwa kuua ari ya kazi kwa vitisho vyako. Makundi kakubwa ukiyoyajenga ndani ya takukuru ni :

(a) kundi la wanao kukusanyia taaarifa za nani anasema nini juu yako. Wewe unawaita watoa taarifa wako. Hawa wamekujaza ujinga na badala ya kufanya kazi waliyoajiriwa nayo sasa kutwa nzima ni kukujaza mambo ya kijinga. Na kwa kuwa wamekufahamu wewe ni mpenda majungu, wanajitahidi sana kuyaleta. Hawa nia pamoja na lilian uliyemhamishia temeke kutokea mbeya na kuwaacha watu wengi wenye matatizo. Tumesikia kuwa ni mpenzi wako na hata ukiwa marangu alikuja na siyo siri tulimwona. Hili la uhusiano tunakuachia wewe na mkeo na huyo binti. Ni private issue. Kwani hata mchungaji aruhusiwa kujitafunia kondoo wake.

(b) kundi la wanaoshirikiana nawe katika mipango yako michafu ya kukiuka taratibu za fedha. Kwa kuwa wananufaika na ubabe wako na hana nguvu za kuhoji inabidi waendelee kunufaika. Mfano ni katika hawa mafundi ambao wewe umewapa kazi ya kupaka rangi majengo ya ofisi nchi nzima bila kufuata taratibu za zabuni. Hivi kweli kuna kikao chochote kilichokaa kuijdili zabuni hiyo? Kwanini unashinikiza kila waendako walale ofisini? Ni utaratibu gani wa kulaza watu wasiohusika ofisini? Je, si kweli kuwa walianzia kufanya kazi nyumbani kwako? Hapa mtu akisema unkula ten percent atakuwa kakosea? Hapo ofisini si una mkuu wa kitengo husika? Hivi kweli unategemea tuwe na nguvu za kuwachunguza walio nje wakati wewe mwenyewe ni tatizo?

(c) kundi la ambao wewe unaliita kundi la kamazima. Na hili ndilo kundi ambalo kwa vigezo vyako na kwa msaada wa hao uliowaweka wakuletee majungu, ndilo unalolimiza pasipo sababu. Sisi tulio nje ya hao wana mtandao wako hatujui ni kwanini hasa umeamua kuia takukuru kwa kujenga makundi. Haya umekuwa ukiyasema wazi kuwa utapambana nao hadi mwisho. Swali tunalojiliza, hao wewe unaosema hawako upande wako na unaojitahidi kuwachanganya kisaikolojia bila sababu yoyote ndiyo kazi aliyokuagiza mhe. Rais? Kwanini unatugawa katika mafugu mafungu kama nyanya sokoni? Ni kwa maslahi ya nani hasa?

(d) kundi jingine ni wale uliowaacha kama watoto yatima wasio na mlezi. Hili ni kundi ambalo likitaka kuishi kwa amani ni lazima lijikombe kwako. Umefanya takukuru kuwa si sehemu shwari tena. Umeifanya kuwa ni mali ya mtu binafsi ambapo majaaliwa ya mtumishi yanategemea uwezo wake si wa kufanya kazi bali kujikomba kwako na kukuletea majungu tena yasiyokusaidia wewe wala chombo.

(iv) umetumia nafasi yako kama mkurugenzi mkuu kuua utendaji mikoani na wilayani. Siyo majungu, enzi za kamazima ambaye wewe unamwona kama mtu asiye stahili heshima walau tulikuwa wilayani tukipata fedha za kufanyia kazi. Na kweli kazi zilienda. Hakuna mwezi ambao tuliwahi kuletew ths 200000/= kama oc ya mwezi kwa wilaya. Leo tuna pikipiki na gari moja na watumishi wasiopungua 5 unatuletea laki mbili (200000/=)

Tunajua kuwa unajenga hekalu maswa na kwa kutumia fedha za ofisi. Hatukukatazi. Wewe kula upendavyo lakini sisi ambao hatukuapishwa na rais kama unavyodai tupe fedha za kazi. Tunaelewa ndiyo maana hutaki kuwashirikisha wakurugenzi katika kufahamu wala kugawa oc kama ulivyotuambia pale marangu ili ufiche uovu wako. Je ndiyo uwazi tunaowajibika kuuchunguza katika ofisi zingine za umma? Tunaelewa ambavyo umekuwa ukitumia fedha za ofisi kuwalipa watu wanaokufanyia kazi binafsi maswa nyumbani kwenu. Na unaowalipa ni watumishi wa ofisi na wale binafsi. Ukweli umetukatisha tamaa kabisa. Na ndiyo sasa tunaelewa ni kwanini pale marangu ulipoulizwa juu ya kusuasua kwa oc za ofisi na hasa za wilaya uling`aka. Huu si uongozi unaotakiwa katika wakati huu tulio nao kwa sasa na kwa jamii kama yetu ya wasomi, vijana na tunaotegemea kujifunza mengi kutoka kwako kama kiongozi wetu mkuu.

(v) lugha ya matusi, vitisho na kudhalilisha tunavyofahamu sisi ni kinyume cha maadili ya uongozi. Wewe hii ni lugha yako na kisingizio kikubwa ni wewe pekee uliye kabidhiwa jukumu na rais lakini unasahau kuwa chombo hakiwezi kwenda kwa mtu mmoja. Ni kweli alikuapisha wewe peke yako lakini tunaamini alitegemea ushirikiane nasi wote kuhakikisha chombo kinaenda.

Kila anayeingia ofisini kwako ni kutukanwa, kufokewa, kulaumiwa, kutishwa n.k. Unashindwa nini kuelekeza badala ya kutukana? Kiongozi mzuri ni yule anayeelekeza badala ya kutukana. Kwako wewe watumishi wote hawajui kazi, hawawezi kazi, hawafanyi kazi, wanakuonea wivu, washirikina n.k utafanya kazi na nani? Ikifika mahala wewe kila mtu ukamwona mwenye matatizo basi elewa wewe ndiye mwenye matatizo. Tena makubwa.

(vi) umepiga marufuku kwa mtumishi yeyote kuwasiliana kwa njia yoyote wala kumtembelea dg mstaafu na mtu akionekana naye na ukapata ushahidi basi mtumishi huyo ni matatizo matupu. Hivi kamazima ni haini katika nchi hii? Hivi kweli haya ni miongoni mwa uliyoambiwa uje kuyafanya ukiwa dg? Hivi tatizo ni nini hasa? Mbona unachokifanya ni mambo ya kitoto? Sisi tuna hakika hili hukutumwa na mhe rais na wala halimo katika kiapo chako. Ni picha gani unataka kutupa sisi unaotuongoza? Kwamba na wewe ukistaafu watu wasikusalimie hata mkikutana kanisani? Au kwa vile una makazi marekani na hutokuwa tanzania ndiyo maana unataka kutupandia mbegu ya chuki? Au na hili utasema ni jungu? Sisi tunao utaratibu wa kuwaheshimu viongozi wetu waasisi na ndiyo maana hata leo marais wetu wastaafu bado wanapata heshima na upendo kutoka kwa watanzania wote. Ungekuwa rais si ndiyo kabisa marais wote waliotangulia ungewachinja? Tuna amini wewe ni mwanasheria tena mwanasheria mzuri sana ila kwa haya unayoyafanya tunaanza kuwa na wasiwasi na hata uelewa wako wa sheria, jaribu upate muda wa kuisoma katiba ya nchi juu ya uhuru wa raia wa tanzania.

(vii) unavyoharibu upelelezi- ni ukweli usiofichika kuwa hata malengo yetu ya kuwabana wala rushwa wakubwa kama ambavyo watanzania walivyo na matumini makubwa kwetu hayatatimia. Hii ni kwa sababu umekuwa na tabia ya kuwaingilia wapelelezi na kuwaamuru waandike kile utakacho wewe na siyo kulimngana na ushahidi uliokusanywa. Maswali tunayojiuliza ni je nini maana ya upelelezi kama majibu yote unayo hata kabla ya upelelezi kuanza? Lengo lako hasa ni kumlinda na kumkomoa nani katika upelelezi huo? Au mwenzetu una mgao kwa watuhumiwa?

(viii) usivyochanganya ubabe na kazi- wewe umekuwa dap, doi, mhasibu mkuu, mwangalizi wa ofisi, afisa usafiri, bwana zabuni n.k. Kama kila kitu unafanya wewe kuna haja kweli ya kuwa na watu hao katika idara? Mfano rahisi ni ule wa afisa ambaye pamoja na ushahidi kuwa anaumwa na kuwa anatibiwa muhimbili ulilazimisha ahamie singida. Afisa huyo kwa kujielewa afya yake, aliamua kuacha kazi kwa saa 24 na kurudisha mshahara na kitambulisho. Wewe waelewa alikaa nje ya mfumo kwa muda gani hadi ulipoamua kumtafuta na kumrubuni aandike barua ya kuomba arudi kazini nawe ukakubali. Wewe ni mwanasheria na unaelwa kabisa kuwa lilikuwa ni kosa. Aibu yote ya nini? Je angekuwa mototo wa mkulima angeipata nafasi hiyo? Au kwa vile ni mototo wa mkubwa? Na ukaamua kumpanga temeke. Hatujui uliandika nini katika jalada lake lakini huu ni udhaifu mkubwa katika uongozi uliouonyesha. Kama ungewashirikisha wenye fani yao wangekushauii ipasavyo. Haya ndiyo madhara ya kujua kila kitu.

(ix) majivuno, majigambo na mijasifa
Kinachotuharibia ofisi yetu ni kuwa unapenda sana sifa, kutukuzwa, kuabudiwa, na kujiona wewe ndiyo mtu pekee aliyefanikiwa hapa duniani.
Umetangaza nchi nzima juu ya mafanikio yako ndani ya muda mfipi kama dg. Umekuwa ukyataja baadhi kama sheria mpya ya takukuru, ununuzi wa magari, ujenzi wa ofisi ya makao makuu, maslahi ya watumishi n.k na kwamba ni wewe uliyeyaleta. Hatupendi kujibizana newe ana kwa ana ila tunapenda kukuambia kuwa hayo mafanikio wala siyo yako na wala jitihada hazikuanza wewe ulipoteuliwa. Tunafahamu kuwa yote yameanza muda mrefu uliopita. Na wala siyo jitihada a mtu mmoja kama unavyotaka kutulazimasha tuelewe. Ni jitihada za watu wengi wa ndani na nje ya takukuru na hata nje ya nchi.

Kama si kutaka kujipa sifa zisizo zako ili uonekane bora kuliko wegine ni nini basi? Hata aliyeajiriwa leo anakufahamu kuwa ni bwana misifa na ndiyo maana kwa wanaokufahamu wanatumia nafasi hiyohiyo kukuvisha kilemba cha ukoka na kuendelea kukuharibia ofisi. Lakini hawakuharibii ofisi kwani ndiyo style ya uongozi uliyoina ni bora.

(x) Kutotunza siri za watumishi wako- wewe ndiyo baba na mlezi wa kila mtu. Jamii ilakutegemea utunze siri za watumishi wako. Lakini hauko hivyo. Umekuwa ukitoa siri za kila ajaye ofisini kwako kwa wasio husika tena bila kuulizwa. Umekuwa unawafanya watumishi wako wadhalilike mbele ya hao unaokutana nao na kuwasimila juu ya matatizo ya watumishi hao. Ni tabia mbaya kama kiiongozi na ambaye ulitakiwa kukumbatia shida za watumishi wako na kuzitafutia ufumbuzi badala ya kuzitangaza. Ni aibu sana na dalili za kutokomaa kiakili. Na hiyo ndiyo gharama za kupenda sana sifa.

(xi) kudhalilisha viongozi wenzako – tangu umingia madarakani umekuwa ni mtu wa kuwatuhumu wakurugenzi wenzio uchawi, ati hawakupi ushirikiano na mambo chungu mzima. Umekuwa mstari wa mbele kuwasema vibaya mbele yetu wakati sisi tunawaheshimu nyie wote kama viongozi wetu. Unapowasema vibaya mbele yetu lengo hasa linakuwa ni lipi? Lengo lako ni ili wewe tukuone bora kuliko hao au tuwadharau wao? Nyie kama mna matatizo kama viongozi ni kwa nini hasa msikae pamoja mkayamaliza badala ya wewe kuanza kuwasema vibaya mbele yetu?tabia hiyo siyo ya kiungwana hata kidogo na haikupi heshima bali kukuona kama mtu usiyeelewa nini maana ya kuwa kiongozi. Kama yupo mtu yoyote anayekuunga mkono katika hili huyo ni mnafiki na hakutakii mema. Ni busara ukatumia muda huu kama kiongozi kuachana na tabia hiyo na kuanza kufikiri kama mtu mzima na kiongozi mwenye dhamana ya juu katika chombo hiki.

Hivi wewe ni lini hasa utakua na kuachana na mambo ya kitoto? Mambo ya kusengenyana ni mambo ya kitoto na mambo ya watu ambao hawana kazi ya kufanya.

Ni nini msimamo wetu

Hadi kufikia mahala pa kuandika barua hii ndefu ni kuwa tumechoka. Hakuna dalili zozote za wewe kujirekebisha na badala yake chombo unakipeleka kusiko. Matarajio ya watanzania ni mkubwa kwetu na wanchokitaka ni ufanisi katika mapambano haya makali.

Watanzania hawataki kusikia juu ya sifa ni amajigambo yako kwani katika tathmini ya nini tumefanya hayatakuwemo. Watanzania wanajua kuwa hii ni taasisi ya wasomi na inaongozwa na wasomi na inakuwa aibu haya yakitoka na wakafamu kuwa kiongozi wetu ni mtu wa aina gani.

Tumechoka na majigamgo yako sasa tunataka kazi. Tunataka ukweli juu ya nini kinakwamisha kazi zisifanyike mikoani. Kwani hatuletewi fedha?

Usipobadilika na kuanza kujali kazi na kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha za serikali tutalazimika kufanya yafuatayo;

a) Tutayaanika katika vyombo vya habari kwani ushahidi wote tunao ili jamii ijue nini hasa kinaendelea ndani ya chombo.

b) Tutayasambaza katika tovuti ili kila aliye ndani na nje apate kuyasoma na kuyaelewa kwa nafasi.

Inauma kukuandikia barua kama hii lakini yametufika shingoni kwani sasa takukuru imekuwa kama kampuni ya mtu binafsi. Tunakuheshimu kama kiongozi wetu lakini umeshidwa kujitambua wewe ni nani na una wajibu gani kwa watanzania.

Kwa kuwa wanaokuzunguka hawakuambii ukweli juu ya tabia yako sisi tumekuwa wakweli kukusaidia ujitambue. Inatuuma kuona umeamua kuwa karibu na wanaoiharibu takukuru na kuchafua sura ya chombo nje.

Waliopo makao makuu wanaelewa vyema hata namna unavyodictate manunuzi na utoaji wa zabuni kwa njia za rushwa. Hili hatulisemi kwa leo.


Mungu ibariki tanzania


Nakala :
katibu mkuu kiongozi
Ikulu - Dar es Salaam (hii ndiyo hali halisi)

Wakuu wa takukuru mikoa
Tanzania bara- haya ndiyo tuliyoyapata marangu
 
Dah,

Nadhani hii ndiyo attachment iliyokuwa password protected.

Sasa hawa kweli watazuia Rushwa kwa mwendo huu? What's going on?!?
 
Takukuru ni kukuru kakala tu hawana uwezo na meno ya kufuatilia rushwa.
 
duh, hii nchi tuna kazi! Hao ndio wazuia rushwa!

Yani basi tu, vitengo nyeti kama hiki havitakiwi kuwa hivi. Kama yaliyoandikwa ni ya kweli basi kuna mengi mabovu katika system nzima ya taasisi hii yanayotakiwa kutibiwa haraka ili kazi iliyokusudiwa ifanyike. Lakini si nilisikia wako chini ya ofisi ya rais na wao wameridhia kabisa na wanajisikia huru kwa kuwa chini ya ofisi ya rais?

Ah, inachosha sana hii
 
Kwa mtindo huu, ile imani ndogo ilikuwa imebakia kwa PCCB imeyeyuka. At least bureau ingelikua inaripoti kwa bunge labda kungekua na tofauti (sina hakika). I'm tired, "Tanzania is sinking.........."
 
Kwa mtindo huu, ile imani ndogo ilikuwa imebakia kwa PCCB imeyeyuka. At least bureau ingelikua inaripoti kwa bunge labda kungekua na tofauti (sina hakika). I'm tired, "Tanzania is sinking.........."

Bob, kwa Bunge hili tulonalo la rubber stamps sidhani kama kungekuwa na tofauti yeyote.... kama tungekuwa na bunge lenye nguvu ya kutetea maslahi ya nchi sawa...not only Tanzania is sinking but as well stinking ...safari ni ndefu
 
I love JF! YOU GET NEWS WHEN THEY ARE STILL HOT...
Tanzania yetu ndio hiyo
 
Ohh poor Tanzania,
Lakini kitovu ni nini hasa?"Like father,like son",so goes the saying,kama JK mwenyewe ni msanii tosha kabisa,na ongezea hapa kuwa huyu Hosea mwenyewe ndo alitumika kummaliza Sumaye back then (the rest is history),so what we're witnessing now ni matokeo ya watu kutafuta madaraka kwa udi na uvumba ndani ya sisiemu,hivyo wanaamua kupay back ofisis za umma kwa marafiki waliowawezesha kuingia pale Magogoni.Kiini ni usanii wa JK,if at all JK had been a serious man even for a second in all his life time,perhaps things would have shown some significant sings of seriousness but as long as he ramins the way he is...ohh I pity Tanzania,sanasana tutazidi kusikia kashfa juu ya kashfa...by the way huyu bwana Hosea nasikia ni Msabato...
 
Wana JF walishasema hii TAKUKURU ni bomu haina mwelekeo wowote ni danganya toto tu. Sasa mambo yanafichuka! Usanii kama kazi!
 
Kwa mtindo huu, ile imani ndogo ilikuwa imebakia kwa PCCB imeyeyuka. At least bureau ingelikua inaripoti kwa bunge labda kungekua na tofauti (sina hakika). I'm tired, "Tanzania is sinking.........."


Tanzania sank when her creator sank in 1999 in Butiama. Fuulstop.

Inatia uchungu sana kuoanwatu waliokabidhiwa kazi ya kusafisha uozo nao wameoza kuliko wanaohitaji kusafishwa.
Irritating!
 
Wana JF walishasema hii TAKUKURU ni bomu haina mwelekeo wowote ni danganya toto tu. Sasa mambo yanafichuka! Usanii kama kazi!

Ohh poor Tanzania,
Lakini kitovu ni nini hasa?"Like father,like son",so goes the saying,kama JK mwenyewe ni msanii tosha kabisa,na ongezea hapa kuwa huyu Hosea mwenyewe ndo alitumika kummaliza Sumaye back then (the rest is history),so what we're witnessing now ni matokeo ya watu kutafuta madaraka kwa udi na uvumba ndani ya sisiemu,hivyo wanaamua kupay back ofisis za umma kwa marafiki waliowawezesha kuingia pale Magogoni.Kiini ni usanii wa JK,if at all JK had been a serious man even for a second in all his life time,perhaps things would have shown some significant sings of seriousness but as long as he ramins the way he is...ohh I pity Tanzania,sanasana tutazidi kusikia kashfa juu ya kashfa...by the way huyu bwana Hosea nasikia ni Msabato...

Kwa kweli nadhani hali ya Tanzania ni mbaya kuliko ninavyodhania.
Yaani hamu yote ya kuwa na Takukuru imeniisha, nimenyong'onyea kabisa.
 
Tatizo lililopo ni dogo tu ili tusonge mbele na uzuiaji wa rushwa ni lazima iwepo aina ya kuchunguzana ile ya Mafia style yaani hata mtoto wako inabidi umuogope,Muungwana ni lazima aunde vyombo na sio chombo kimoja tu,tena inavyotakiwa hivi vyombo inabidi visijuane nani yumo na nani hayumo,inawezekana kabisa humo humo ndani ya takukuru wakaingizwa au kikaundwa chombo ambacho,kitakuwa mwiba ndani ya mwiba yaani japo wamo ndani ya takukuru lakini wana kazi nyengine vile vile na hapa ndipo usalama wa Taifa unapotakiwa kupaangalia sana kwani chombo hiki kisipowekwa chini ya uchunguzi wa siri nyeti kinaweza kuliangamiza Taifa kama ugonjwa usiojulikana ambao umekumba wanakijiji.
 
Ile sheria mpya iliyozaa TAKUKURU nafikiri ilikuwa kuwafurahisha DONORS but in reality ni uozo mtupu. Any way hawa ndo watawala maswaiba wa JK.
 
Kama mkuu wa kukamata RUSHWA naye ni mla RUSHWA tusitegemea neema ya MUNGU kuwa TZ inaweza kuwa rushwa-free.
 
Mimi ningependa kukupongeza kwa ujasiri wako na uwazi wengine tumekuwa tunakufa na tai shingoni. Poke shukrani zangu za wazi na pia hiyo ambayo nitakutumia moja kwa moja - private message. Kama ni wa kusikia atasikia lakini kama ni sikio lakufa ... sijui itakuwaje?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom