PCCB kudhibiti mapato Chalenji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PCCB kudhibiti mapato Chalenji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 2, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,756
  Trophy Points: 280
  Hawa PCCB kazi imewashinda. Chombo hichi kiliundwa kupambana na rushwa. Pamoja na kuwa rushwa inashamiri Tanzania hakuna lolote wanalolifanya ili kuiondoa rushwa au kuipunguza, sasa wanaenda kusimamia mapato ya Chalenji! :confused:
  Hivi kusimamia mapato ya mashindano ya chalenji kunaingiliana vipi na kupambana na rushwa!? Hakuna vyombo vingine vinavyoweza kufanya kazi hiyo badala ya PCCB ili wao waendelee kupambana na rushwa!?


  PCCB kudhibiti mapato Chalenji

  na Makuburi Ally
  Tanzania Daima

  KAMPUNI ya ulinzi ya KK ya Afrika Kusini iliyo na tawi lake jijini Dar es Salaam, ndiyo itakayohusika na usalama na ukusanyaji wa mapato ya mechi za Kombe la Chalenji zitakazofanyika nchini kuanzia Desemba 8.
  Michuano hiyo itakayopigwa katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, itashirikisha timu 11 zilizogawanywa katika makundi matatu ambako mawili yatakuwa Dar es Salaam na moja Arusha.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, mbali ya kampuni hiyo, katika suala la udhibiti wa mapato, KK watashirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB).

  Mwakalebela alisema, uamuzi huo umelenga kuhakikisha michuano hiyo inatawaliwa na usalama wa kutosha na kila anayestahili kulipa, anafanya hivyo bila kutumia ujanja ujanja wa hapa na pale ili mapato yaweze kupatikana.

  Alisema, kampuni hiyo itakuwa ndiyo mdhibiti mkubwa wa masuala ya usalama na mapato, hivyo akatoa wito kwa wale wote ambao huingia mpirani kwa kutumia mbinu, wajiandae kulipa viingilio.

  "Uamuzi wa kuweka kampuni ya ulinzi ni kuondokana na ubabaishaji katika suala la mapato, ambao umekuwa na matatizo makubwa ambayo hutokana na kukumbatia makomandoo," alisema Mwakalebela.

  Katika michuano hiyo, Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' iliyo kundi la A, itakuwa katika kituo cha Dar es Salaam pamoja na timu za kundi B. Bara itakuwa pamoja na Burundi, Kenya na Somalia.

  Kundi B, lina timu za Rwanda, Uganda, Eritrea na Djibouti huku kundi D, litakalokuwa Arusha, litakuwa na timu za Sudan, Ethiopia na Zanzibar. Bara imepangwa kufungua dimba na Kenya.

  Aidha, Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Mbrazil Marcio Maximo, kesho atataja nyota 20 watakaocheza Chalenji, ikiwa ni siku tano kabla ya kuanza kutimua vumbi.

  Maximo anafanya mchujo ikiwa ni baada ya mazoezi ya wiki kadhaa kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo ambayo kwa mara ya mwisho kutwaa ubingwa ilikuwa ni mwaka 1994 chini ya Kocha Syllersaid Mziray.

  Katika hatua nyingine, wakala wa wachezaji wa soka Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Mehdi Rhemtullah, amesema atanataraji kuangalia vipaji katika michuano hiyo.

  Akizungumza jijini jana, Rhemtullah alisema mbali ya michuano ya Chalenji, ataendelea kuangalia vipaji hata katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara itakayoanza kutimua vumbi Januari 12.

  Rhemtullah alisema wachezaji atakaowapata atawatafutia soko katika timu za nchini Denmark na Uswisi na kuwataka wachezaji kuonyesha viwango vyao halisi.
   
 2. D

  Dotori JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2007
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Point! Naona PCCB inatoka nje ya mandate yake ya msingi
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Dec 3, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ok.. I give up! naomba tuwape mji maana hiki kitendawili atakayetegua ana kazi...
   
 4. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2007
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Naona kazi hii wataiweza na kuimudu bila shaka. Kwani wahusika wa viingilio hawaitaji kula Krismasi na Mwaka mpya kabla ya kukamatwa.
   
Loading...