Sijakuelewa unasemaje? Kwenye nishati unatozwa VAT 21% au ni kodi gani? Nadhani inabidi uangalie haiwezi kuwa VAT.Hizi double taxation ni balaa, maraisi watakaofuata watarithi mambo ya ajabu sana.
Naona Kenya wanatoza 16% kwenye VAT. Hapa kwetu tunatozwa 21% kwenye nishati. I can't wait to leave the "employee" arena.
Ukweli kodi ni kubwa lakini kwa kulinganisha na nini? Ni nini vyanzo mbadala.
Pia Ukiangalia vizuri utaona bajeti ya Tz ni kama imedouble kwa kipindi cha miaka 2-3. Ingawa impact yake yake haionekani kwenye macho ya Watanzania. Ingawa kupungua kwa thamani ya shs kunaweza kuwa chanzo lakini kasi ya depreciation sio hii inayooonekana kwenye budget.
Changamoto nadhani iwe kwenye budget inayozingatia matumizi, vipaumbele na inayopimika. Haiwezekani budget ikawa inaongezeka lakini athari za ongezeko hazionekani kwa Watz.
Lakini pia wafanyabiashara, NGO's na taasisi za dini nazo zinakwepa mno kodi. Ipo haja ya kuitazama mianya hii.