Pauni ya Uingereza yazidi kuporomoka

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
140919024803_cn_british_scottish_pounds_624x351_epa.jpg

Pauni ya Uingereza yazidi kuporomoka
Siku chache tu baada ya Uingereza kupiga kura ya kujiondoa kwenye muungano wa ulaya, sarafu ya nchi hiyo imeendelea kudorora mapema leo katika soko la ubadilishanaji wa fedha.

Baadhi ya masoko ya hisa katika bara la Asia yameanza kuimarika kufuatia kuporomoka kwa paundi kuanzia Ijumaa iliyopita.

Waziri wa fedha wa Uingereza, bwana George Osborne, amezihakikishia masoko ya Ulaya kuhusu matumaini ya siku zijazo kufuatia kura hiyo ya kujitenga.

Soko la ubadilishanji wa fedha limefunguliwa leo likiwa asilimia 0.8% chini ya kiwango kilichoshuhudiwa ijumaa.

Kigezo cha Soko la hisa la FTSE lilifunguliwa leo likiwa na pointi 6,092.19.

110805051510_cn_hang_seng_fall_640x360_bbcchinese_nocredit.jpg
Image Baadhi ya masoko ya hisa katika bara la Asia yameanza kuimarika kufuatia kuporomoka kwa paundi kuanzia Ijumaa iliyopita.
Pauni ya Uingereza ilibadilishwa na dola $1.3463, za marekani ikiwa ni asilimia 2% chini ya kiwango cha Ijumaa.

Dhidi ya sarafu ya Ulaya Euro inabadilishwa na €1.2170,ikiwa ni asilimia 1.2% chini ya kiwango cha ijumaa.
Waziri wa fedha bwana Osborne amesema kuwa uchumi wa Uingereza utalazimika kujifunga kibwebwe kwani waingereza watalazimika kusubiri kwa muda kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya atakayetoa mwelekeo mwafaka wa taifa.

Huko Asia , serikali zimekuwa zikisaidia soko la ubadilishanaji wa fedha zisiporomoke zaidi na kuathiri vibaya uchumi wa eneo hilo.

BBC Swahili
 
Hii refererendum ilikuwa driven na akili za kibaguzi tuu ,at the end watakachopata British will be net negative
 
Hii refererendum ilikuwa driven na akili za kibaguzi tuu ,at the end watakachopata British will be net negative

EU si ya juzi juzi tu, kwani kabla ya hapo Uchumi wa Uingereza ulikuwa na tatizo gani? Waingereza ni binadamu smart upstairs wamekwisha jipanga na contigency plans chungu nzima za kushinda njama za Marekani na Ujerumani za kutaka kuua uchumi wa Uingereza.

Watashirikiana na Uchina, Singapore, India na Urusi - tuseme mataifa yanayo hunda BRICS ndio maana Waingereza walikuwa wa kwanza kutaka kujiunga na Bank/Monetory Funds za BRICS licha ya America kushinikiza Uingereza isijiunge wenye walikataa na kuomba kuwa member - reasons: they saw it COMING i.e referandum.

Katka sakata hili watakao poteza Big time ni Wamerika - i.e eventually.
 
Back
Top Bottom