Paulo afuata nyayo za Nape, atuma ujumbe kumwombea msamaha kwa aliowakosea

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Vikwazo vya kiuchumi si tatizo Sana kwa bilionea Paul, vikwazo vya madaraka ni kikwazo kikubwa kufikia ndoto zake hapa Duniani. Upo mkwamo ndani yake na Hana budi kuvuka vinginevyo mkwamo huu utafifisha kila hatua aliyowahi kupiga kwenye siasa.

Tunajifunza kwa waliofanikiwa,naamu tunajifunza kwa Nape ambaye alipitia mateso ya kutengwa baada ya yakuvuliwa Uwaziri. Nape alifanya Nini? Naomba nikurejeshe siku alipopewa msamaha na JPM, siku hiyo ndipo tulipofunuliwa kwamba kukaa kwake kimya na kuishia kutweet mafumbo kuliambatana na kuwatuma watu mbalimbali wamwombee msamaha kwa JPM na wamwombee appointment. Kwa wanaofuatailia siasa hizi sizizo na tija utagundua JPM hakupenda unafiki bali alimtoa kijana Ikulu na kuingia na kwenye viwanja vya Ikulu kumtangazia msamaha.

Ilikuwa ni furaha moyoni lakini fedhea kwa waliomwona Nape shujaa. Niwakumbushe kwamba JPM alitamka adharani kwamba kijana Nape amewatuma watu mbalimbali na hakuona sababu ya kumsamehe, ila ameamua kumsamehe baada ya kuombwa na Mama Maria. Siasa Zina utumwa ndani yake.

Kwa wanaopenda kujua zaidi kuhusu alichofanyiwa Nape siku ya kupatiwa msamaha nenda YouTube wamehifadhi taarifa hii kwa ajili ya kizazi kijacho.

Naamu huu utaratibu ndio wanaotumia kina Kigwangalla wanaotuhumiwa kukwapua fedha za Maliasili enzi hizo na Paul ambaye aliwekwa kanda na Mzee wetu jasiri. Msamaha umeanzia Msoga haujakamilika ni mwisho utakwenda kuhitimishwa Chamwino Kama mambo yatakaa sawa.

Wanasema kwenye chama chetu tunaongoza kwa kubebana na kusameana bila kujali uzito wa misamaha hiyo na madhara yake kwa watu. Tunaamini kwenye msamaha usioendana na msamaha kwa sababu tu tunajiandaa kuifanya nchi yetu ya koo flani hivyo mvahakato wa Sasa ndani umejikita kwenye zimwi likujualo.

Watu wale wale wanaoana, wanarithishana madaraka kutawala watu walewale waliotawaliwa toka ukoloni. Kila la kheri Paul kwenye safari yako ya kupatana na wabaya wako urejee kwenye STK.
 
Paul atarudi siku Mpango au Chongolo watakapoachia viti vyao. Aliwadhalilisha vyakutosha.
IMG_20210527_183902.jpg
 
Ilw dharau kwa PM nadhaninilipita kipimo....sikuo lilizidi kuchwa....alitaka PM aqe anasujudu kwa RC kusa wote wateuliwa na eti rank moja bendeea sawa daaa....alijisahau hutu mtoto.....pensi nyanya anaenda ziara kupokelewa vyombo rasmi ulinzi usalama ...mdharau ilizidi acha apambane hali yake
 
Hell No !!! People should learn to realize the consequences of their actions (hence they should thoroughly think before acting). Otherwise such behaviours will be repetitive.
 
Ilw dharau kwa PM nadhaninilipita kipimo....sikuo lilizidi kuchwa....alitaka PM aqe anasujudu kwa RC kusa wote wateuliwa na eti rank moja bendeea sawa daaa....alijisahau hutu mtoto.....pensi nyanya anaenda ziara kupokelewa vyombo rasmi ulinzi usalama ...mdharau ilizidi acha apambane hali yake
Kuna watu hawafai kubebwa, ukimbeba anakunyea na kukojoa kabisa
 
Vikwazo vya kiuchumi si tatizo Sana kwa bilionea Paul, vikwazo vya madaraka ni kikwazo kikubwa kufikia ndoto zake hapa Duniani. Upo mkwamo ndani yake na Hana budi kuvuka vinginevyo mkwamo huu utafifisha kila hatua aliyowahi kupiga kwenye siasa.
Huyo hawezi kupata msamaha kutokea Msoga, alimdhalilisha sana rafiki yake wa enzi zile za kufunga gidamu za viatu! Yeye atulie tu!
 
Vikwazo vya kiuchumi si tatizo Sana kwa bilionea Paul, vikwazo vya madaraka ni kikwazo kikubwa kufikia ndoto zake hapa Duniani. Upo mkwamo ndani yake na Hana budi kuvuka vinginevyo mkwamo huu utafifisha kila hatua aliyowahi kupiga kwenye siasa.

Tun
Huwezi mlinganisha Nape na Paulo.
Nape tayari aliwiva kisiasa na hakuwa mporaji wa mali za umma na za watu binafsi.
Nape hakuwa na jinai, kutofautiana Nape na JPM ni misimamo ya kisiasa ambayo kuomba radhi mtu unaeleweka.

Paulo ni fisadi, na alifisadi mali nyingi za watu binafsi.
Paulo na Sabaya ngoma droo!
Unakumbuka yale ma BMW aliyopora toka kwa wafanyabiashara?
Nyumba za Masaki na kwingineko?
Paulo ana jinai and he should come clean.
Hata Mama akisema anamsamehe tutashangaa, kwa nini Sabaya afungwe na Paulo asepe kiulainii!
 
Back
Top Bottom