Paula anaweza kuwa msichana mwenye mafanikio mpaka dunia ikashangaa

SIERA

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,396
2,000
View attachment 1849613

Nimeona mitandao ikimbeza sana Supastaa wetu mpya wa kike Tanzania mtoto wa Kajala aitwae Paula.

Wengi wanamchukulia Paula kama mtoto wa kike aliyeshindikana na amepoteza uelekeo wa maisha.

Wengine sababu ya elimu sababu hakufanya vizuri darasani. Na kuna wanafki wanasema kaanza mapenzi akiwa mdogo.

Mimi nataka niwaambie endapo Paula akisimamiwa vizuri na akaitumia mitandao kama sehemu ya kupiga hela basi atakuwa na pesa nyingi mpaka watu washangae.

Anachohitaji sasa hivi ni kupata management nzuri na branding nzuri.

Habari za Paula zinafatiliwa kuliko sociolite yoyote wa kike kwa hapa bongo sasa hivi. Huu ni mtaji mkubwa sana kwake kuliko hivyo veti mnavyoona ndio dili. Kazi ni kwake kubadili kelele za mitandao kuwa pesa atajenga ataendesha gari analotaka na anaweza kuwa na biashara kubwa tu akiwa na umri mdogo.

Watu wa showbiz nafikiri watanielewa zaidi.

Management ya kufanya kazi gani kipaji gani?!
 

SIERA

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,396
2,000
Upo gizani sana, pengine hujui hata socialite wanatengenezaje pesa.
Paula tayri ni brand anachotakiwa ni kuset trend then pesa itamfata kama mfereji wa maji.

Bongo hakuna uhaba wa pesa bongo kuna uhaba wa watengeneza pesa. Watu wana opt kusoma sana sababu ndio only way waliokalilishwa watatoboa.

Ku trend kwa kudanga au nini Embu tuelezee?!
 

SIERA

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,396
2,000
Brand!!!! kama hana product endelevu ya kupeleka sokoni yenye demand kubwa ni kumpoteza maboya mtoto wa watu. Hana chochote cha kufanya zaidi ya uvideo vixen, photoshoot kutangaza brand za watu kwa malipo kiduchu labda sana na event appearance nazo kwa malipo kiduchu.

Nchi yetu bado ni masikini, hivyo hivyo na industry bado ni masikini sana, issues kama Gigs na showbize bado hazina pesa kiasi hicho, na kwa wasanii hakuna msanii anaweza kuja na bidhaa yenye brand yake akaipush sokoni ika-boom. Wapo akina Flavian matata baada ya uwekezaji mkubwa wanapush product zao zinatoka lakini sio kwa ukubwa huo.

Paula kutengeneza pesa hizo mnazomuaminisha kupitia jina kibongo bongo ni uongo, labda kutengeneza umaarufu ambao utampa "pesa madafu tu". Njia walizopita akina Kyle Jenner huku haziko applicable.

Kabisa hazipo applicable sbb Hamna watu wa maana wenye akili hizo kibongobongo kufanya mtu awe na bidhaa na watu wakaipenda wakaifuataa..
Iko wp product za Diamond na anapenda na watanzania?!
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,244
2,000
Mfano mzuri mzee mpili now anapiga pesa haswa kusoma haimaanishi ndio kufanikiwa kimaisha mdau umetoa ushauri mzuri
Mzee Mpili hapigi hela ya maana. Akiumwa hata malaria tu wanayanga wataambiwa wachange. Alikuwepo mzee wa 900 itapendeza, alikuwepo Mzee Majuto wote tuliona mwisho wao ambavyo hawakuthaminiwa
 

naiman64

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
6,311
2,000
Si utoto unamsumbua yani kadem ka 18 yrs old kanawaza nini zaidi ya iPhone macho matatu na outing za KFC hapo anaona kamaliza maisha too bad hana kiongozi mzuri! Mama yake ndio anamsikiliza mtoto anataka nini badala ya mtoto kumsikiliza mzazi
Mkuu hasa pale kuna mama? Bint kaanza mabwana yeye anatembea uchi Sisi waafrika hatuna hiyo, halafu kajitoa fahamu. Siku bint akigombana na huyo bwana matusi yote kwa mama tena asithubutu kusuluhisha
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
41,611
2,000
Mkuu hasa pale kuna mama? Bint kaanza mabwana yeye anatembea uchi Sisi waafrika hatuna hiyo, halafu kajitoa fahamu. Siku bint akigombana na huyo bwana matusi yote kwa mama tena asithubutu kusuluhisha
Sie tutasubiria ulimwengu umfunze hata Lulu aliwehushwa na dunia ila alipokaa ndani mwaka mzima akatolewa kwa hisani ya kigogo mmoja ndio ilipokuwa pona yake ila alijifunza kitu na sahizi humuoni akihangaika na kiki toka atoke jela!!
 

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,004
2,000
Kwani Jokate alisaidiwa na elimu yake au ilitokea zari akapendwa na mtu mkubwa.
Akina kingkiba wamepita naye sana

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
Elimu ilifanya akabebeka kirahisi
Kupita na Kingkiba na wengineo si hoja. Elimu inamfanya aendelee kuwa valid baada ya mwili kuchoshwa na hao uliowataja unlike wema ambaye alitegemea mwili tu bila kuwa na elimu
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,802
2,000
Elimu ilifanya akabebeka kirahisi
Kupita na Kingkiba na wengineo si hoja. Elimu inamfanya aendelee kuwa valid baada ya mwili kuchoshwa na hao uliowataja unlike wema ambaye alitegemea mwili tu bila kuwa na elimu
Kinachokufanya umhukumu Wema ni kipi ? Unataka kusema wema ameharibikiwa Sana maisha kuliko graduate wote mjin hapa kisa Hana Elimu ..... Wema sio choka mbaya kama unavyofkri
 

Euroleague

JF-Expert Member
Apr 11, 2020
355
1,000
Kabisa hazipo applicable sbb Hamna watu wa maana wenye akili hizo kibongobongo kufanya mtu awe na bidhaa na watu wakaipenda wakaifuataa..
Iko wp product za Diamond na anapenda na watanzania?!
Kwanza nahisi kama makampuni yamestuka flani hivi yanatoa ubalozi kwa wasanii wapumbavu, mwisho wa siku brand ya bidhaa inashuka ukijumlisha na wanaharakati kusagia kunguni ndio kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom