Paul Pogba anashindwa kumpa ubingwa Mourinho, N'golo Kante anaelekea kumpa ubingwa Conte

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Mourinho kocha mreno kwa sasa akifundisha Man utd kipindi chake cha usajili alimsajili Paul Pogba kwa gharama za usajili zilizovunja rekodi ya dunia huku muitaliano naye akimsajili kijana wa kifaransa N'golo Kante.

Ligi inavyoenda kama vile Conte ndiye alicheza karata salama zaidi kukiwa na kila dalili Chelsea kubeba kombe msimu huu labda sijui utokee muuujiza gani.

Ukiangalia Conte ameongeza kama wachezaji wawili au watatu tu toka kikosi cha Mourinho pindi akiwa Chelsea David Luiz Na Ngolo Kante sana sana huku The Special One yeye akija na Ibramovic, Pogba, Baily na Mikhitaryan.

Kwa Faida zaidi The special one ndo anafaida kwan anaijua zaid ligi ya Uingereza zaid ya Conte.

Tusubiri tuone nani alicheza karata zuri zaidi aliyemsajili Pogba au aliyekuja na N'golo Kante.
 
Mourihno Kocha Mreno kwa sasa akifundisha Man utd kipindi chake cha usajili alimsajili Paul Pogba kwa gharama za usajili zilizovunja rekodi ya dunia huku Muitaliano naye akimsajili kijana wa Kifaransa Ngolo kante.ligi inavyoenda kama vile Conte ndiye alicheza karata salama zaidi kukiwa na kila dalili Chelsea kubeba Kombe msimu huu labda sijui utokee muuujiza gani.

Ukiangalia Conte ameongeza kama Wachezaji wawili au watatu tu toka kikosi cha Mourihno pindi akiwa Chelsea David Luiz Na Ngolo kante sana sana huku The Special One yeye akija na Ibramovic,pogba,Baily,na Mikhitryan.

Kwa Faida zaidi The special one ndo anafaida kwan anaijua zaid ligi ya Uingereza zaid ya Conte.

Tusubiri tuone nani alicheza karata zuri zaidi aliyemsajili Pogba au aliyekuja na Ngolo Kante.

Kulingana na Ligi ya Uingereza ilivyo, Mourinho alichemsha kumsajiri Pogba kwa gharama zote hizo
Thamani ya Pogba (£89Mil) ni sawa na Moses (£9Mil)+ (Matic £20) + (Kante £30Mil) + (Willian £30Mil), sasa hapo ni dhahiri kabisa kuwa Mou alichemsha na kwa hiyo sababu ilikuwa ngumu sana kuchukua kombe huu mwaka kwani hiyo pesa angeweza kupata wachezaji wanne wenye kuipa ushindi timu
 
pogba aliomba kuchezeshwa Na Carrick Mourinho akampa lakin bado hajafika vile viwango watu walitaka.
Anataka kuwa kama wachezaji wa kibongo kuna siku anacheza mpira mzuri sana ila kuna siku hata kumwangalia hutaki
 
Huyu jamaa huwa ananiboa sana napenda asichezeshwe au awe bench kabisa maana kazi yake ni kuruka ruka tu uwanjani,kama mzigo ambao mourinho atakuwa amepata galasa basi hili analo
 
Kulingana na Ligi ya Uingereza ilivyo, Mourinho alichemsha kumsajiri Pogba kwa gharama zote hizo
Thamani ya Pogba (£89Mil) ni sawa na Moses (£9Mil)+ (Matic £20) + (Kante £30Mil) + (Willian £30Mil), sasa hapo ni dhahiri kabisa kuwa Mou alichemsha na kwa hiyo sababu ilikuwa ngumu sana kuchukua kombe huu mwaka kwani hiyo pesa angeweza kupata wachezaji wanne wenye kuipa ushindi timu
Kwani si pesa ipo we inakuuma nini mkuu?? We need quality not quantity
 
Kwani si pesa ipo we inakuuma nini mkuu?? We need quality not quantity

Sasa kaka unazungumza Quality gani?, yaani Pogba ndio umlinganishe na Konte?, au perfomance ya Victor ndio ulinganishe na Vitu vya kijinga kama Pogba?

Kaka kama wewe ni mpenzi wa soka la ukweli lazima ukubali Man U/ Mou walichemsha kutumia pesa hizo zote kwa mtu mmoja tu as far as EPL is Concerned, ligi kama za Spain au Itali sawa, sio EPL,
 
Ata leo ukiwauza tena kante na Pogba bado thamaniya Pogba itakua juu kuliko kante. Pogbaa anafanyakaziyake vizuri ila timu bado haijapata muunganiko sahihi. anachokitafuta kocha ni muunganiko, kwakuwa vipaji anavyo. Kontea mepata muunganiko ndiomaana anafanya vizuri. Kwaujumla Pogba amefanya kazi sawa na kiwango chafedha au thamaniyake. Muda simrefu nyie mnao mkataa ndio mtakua mkishangilia. Kama kiungo mshambuliaji amefunga magoli, ana assist zakutosha, ana ana shot za kutosha.
Individual ana vitu vingi vya kumfanya awe wa kipekee ,ila timu inahitaji watu wa aina yake kwasasa ina kosa. Timu imekosa watu kama Schools Roy keen Daren Fretcher watu wanaotumia mbinu safi na chafu watu wenye roho zachuma na wanaiambukiza timunzima.Sifa zahawa, watafika maeneo yote uwanjani unaweza kusema hawana namba maalum uwanjani. Pia kuilazimisha timu pinzani na kupata matokeo. ila naamini majira ya kiangazi Kocha ataleta mtu wa Kumsaidia kazi.
 
Acheni hoja mgando nyie alivoikuta man u morinho ni pabaya na pogba hachezi pekeyake
 
Ngolo kiwango chake bado sana kwa Pogba chelsea chemistry ya team ndio inawabeba ila angalia pasi utaona Pogba anapiga nyingi na za uhakika ,ndio mchezaji wa pili england kwa kupiga pasi nyuma ya henderson wa liver.
 
mashabiki wa chelsea bana ligi ilipoanza conte alizibuliwa vibaya sana gem tatu wakaanza kante hana sifa ya kumuweka sesc bench mwezi umeonekana wamesahau kama kuna jua huo ndo unafiki wa mpira matukio haya yanaufanya mpira kuwa mzur


euro takwimu za timu ya taifa zilikaaje wakikutana kwenye kikos kimoja nani anasugua bench?
 
chemist yetu chelsea na mfumo 3-4-3 unatubeba sana jaman. mfumo huu unakuja kuwa 5-3-2 tunaposhambuliwa yaan alonso azpicueta cahil luiz na moses. na unakuwa 2-3-5 mathematcally tunaposhambulia yaan alonso hazad pedro/wilian costa na moses. pia n wazur kwa kaunta atak. mfumo umepata wa2 sahih. muangalie moses na alonso as wingback, mchek luiz cahil na azp, mchek kante na matic, wachek nafowad wetu (PHD) pedro hazad na diego. tim nyngne bado hazjaseto angalia man u, man cit na liva. mpaka mda huu hawajapata X1 kamili wanajarb jarb. nategemea spurs itatusumbua sana kule wakubwa wale
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom