Paul Makonda: Wananchi walioikimbia Dar warudi, Mauti hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila mtu afanye fujo awezavyo na kupiga kelele na vigeregere!

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,064
1,500
Danieli 5:1-5
[1]Belshaza, mfalme, aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa akanywa divai mbele ya elfu hao.

[2]Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile vyombo vya dhahabu na fedha, ambavyo baba yake, Nebukadreza, alivitoa katika hekalu lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.

[3]Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu, vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwako Yerusalemu; na mfalme na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wakavinywea.

[4]Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.

[5]Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu, vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nyumba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika.
Mkuu wa mkoa ametaka jumapili tucheze mziki mnene kusheherekea kuisha kwa Corona.

Ila Ushauri tu, aache siasa kwenye maisha ya watu, atadaiwa damu hii kuanzia kwa Keegani mpaka kizazi cha nne.
Nawashauri watu wafuatao wasitoke nje hiyo siku.

Kama uliwahi:
1. kushuhudia maduka ya ushirika, RTC, TES au
2 uliwahi kuyaona maduka ya viatu ya BORA na MORO SHOES better yet.
3. kama uliwahi kujipaka mafuta ya Yu au Yolanda...
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
3,424
2,000
Na Mungu atusaidie, Huu ni ushindi mkubwa kwa wote wanaomwamini YESU.

Yesu alisema ukiwa na imani kama punje ya haradali basi waweza amisha milima, imani ya MAKONDA na MAGUFULI ndiyo YESU amezungumzia, nakwambieni maisha yanarudi kama zamani, piga keleleeeeeee
Unakufuru ujue, na Mungu siyo binamu yako.
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
10,899
2,000
Mtanzania ni mtu wa namna ya kipekee duniani. Kama masihara corona imechemka yenyewe. Siwezi kuamini kuwa maombi yamefanya kazi, wala Siwezi kuamini kuwa juhudi za wizara ya afya zimefanya kazi. Ni kinga ya asili ndio iliyofanya kazi. Juhudi tulizochukua huku Afrika na Tanzania juu ya COVID 19 ni kiduchu sana...
Umechelewa kaka. Propaganda na siasa tayari zimeshatake over


Sent using Jamii Forums mobile app
 

hjayhals

JF-Expert Member
Feb 13, 2013
696
500
Aina ya viongozi wanaojinadi kumpenda Mungu na hawajui Mungu anataka nini kutoka kwao. Hivi kweli kama maradhi yameondoka ndo tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa kufanya fujo, kupiga kelele na kunywa pombe? Shame!
 

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
3,400
2,000
MH Rais wangu mpenzi kwanza shikmooo, pili nisichelewe nakujulisha kuwa sifati maelekezo yako ila natii Amri ya Mh mkuu wa mkoa wangu Makonda.

Maelekezo yako ni kuwa tuwe na siku tatu za kushukuru baada ya zile tatu za kumuomba Mungu dhidi ya corona na kweli Mungu amejibu maombi yetu.

Mimi nafata ya Makonda ya kutaka tusherekeeee na si vinginevyo,maana wakati tumefunga tukiomba Mungu nilimuona mteule wako Dc wa Dodoma wakifanya ujinga na walevi sasa leo wewe ametangaza tufunge na kumshukuru MUNGU huyu ametangaza tule Bata mimi nimeamua kulingana na yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom