Paul Makonda: Wananchi walioikimbia Dar warudi, Mauti hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila mtu afanye fujo awezavyo na kupiga kelele na vigeregere!

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,471
2,000
Akiwa katika ujenzi wa daraja la Tanzanite, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wake kufanya fujo za hali ya juu ikiwepo kupiga kelele kwa nguvu zote na watu kwenda beach kama ishara ya kumpongeza Rais kwa kuishinda COVID 19.

Pia Makonda amewataka watu wote waliokimbià Corona Dar warudi haraka kwani kifo hakikimbiwi.

Chanzo: Global TV Online.
"Pia Makonda amewataka watu wote waliokimbia Corona Dar warudi haraka kwani kifo hakikimbiwi". Mwisho wa kunukuu!

Hii kauli nimeilewa sana hii maana inawahusu wale wote waliolikimbia Jiji, kisa Corona! Uoga siyo jambo la kujivunia hata kidogo. Dawa ya matatizo ni kuyakabili na siyo kuyakimbia.
 
Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
1,764
2,000
Akiwa katika ujenzi wa daraja la Tanzanite, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wake kufanya fujo za hali ya juu ikiwepo kupiga kelele kwa nguvu zote na watu kwenda beach kama ishara ya kumpongeza Rais kwa kuishinda COVID 19...
Huyu mtu ni wa kumpuuza, Corona ipo na inaua. Huu ushauri wa kipumbavu atakaye ufuata basi atakuwa ni mpumbavu zaidi ya wapumbavu wote duniani.
 
orturoo

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
898
1,000
Akiwa katika ujenzi wa daraja la Tanzanite, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wake kufanya fujo za hali ya juu ikiwepo kupiga kelele kwa nguvu zote na watu kwenda beach kama ishara ya kumpongeza Rais kwa kuishinda COVID 19...
Mungu atusamehe maana tumechanganyikiwa
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,074
2,000
Akiwa katika ujenzi wa daraja la Tanzanite, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wake kufanya fujo za hali ya juu ikiwepo kupiga kelele kwa nguvu zote na watu kwenda beach kama ishara ya kumpongeza Rais kwa kuishinda COVID 19...
Hivi mnajua kuwa watu hawawapeleki wagonjwa wao hospitali..!!? Maana wakipelekwa tu wanawekwa sehemu bila huduma na mwisho hufa... sasa wanaokwenda hospitali kutafuta takwimu, takwimu za huko si za kweli..

By the way, maabara haiaminiki, kwamba korona imeisha mnapata wapi hizo taarifa?
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
4,596
2,000
Usisikilize wanasiasa! Jukumu la afya yako ni wewe mwenyewe. Corona bado ipo. Chukua tahadhari. Jilinde wewe na watu wengine.
Jiulize kwanini hawatoi takwimu?!

Kwa sehemu hiyo inawezekana lakini kwa sehemu pia inategemeana na maamuzi ya hao wanasiasa.

Mfano swala la kufunga na kufungua Shule na vyuo ni wao waliamua na wataamua siku ya kufungua.

Sasa nikuulize mfano ukiwa mwanafunzi wao wakaamua vyuo/Shule zifunguliwe siku fulani na wewe utafanyaje?

Je utabaki nyumbani kujilinda au itabidi uende Shule/ chuo?

Vivyo hivyo kwa watumishi wa umma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom