Paul Makonda: Wananchi walioikimbia Dar warudi, Mauti hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila mtu afanye fujo awezavyo na kupiga kelele na vigeregere!

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
945
1,000

Akiwa katika ujenzi wa daraja la Tanzanite, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wake kufanya fujo za hali ya juu ikiwepo kupiga kelele kwa nguvu zote na watu kwenda beach kama ishara ya kumpongeza Rais kwa kuishinda COVID 19.

Pia Makonda amewataka watu wote waliokimbià Corona Dar warudi haraka kwani kifo hakikimbiwi.
1589895784493.png
=====

RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI KURUDI MAKAZINI, AWAELEKEZA WALIOFUNGA BIASHARA KUZIFUNGUA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Watu wote waliofunga Hotel, Migahawa na sehemu za biashara kutokana na hofu ya Corona kuzifungua na kuanza kazi kama kawaida huku akiwataka waendelea kuchukuwa tahadhari kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya.

RC Makonda ametoa wito pia kwa Wale waliokimbilia mikoani kwa kuhofia Corona kuhakikisha wanarudi na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

Aidha RC Makonda ametangaza siku ya Jumapili ya wiki hii kuwa siku ya Sherehe na Shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Janga la Corona ambapo ameeleza kuwa atafurahi kuona kila mmoja anasherekea siku hiyo.


"Rais Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa Makuu aliyotutendea.

Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya kwenye ukuta wa Yerico, kwaiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida" Alisema RC Makonda
 

cmoney

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
2,770
2,000
Na Mungu atusaidie, Huu ni ushindi mkubwa kwa wote wanaomwamini YESU.

Yesu alisema ukiwa na imani kama punje ya haradali basi waweza amisha milima, imani ya MAKONDA na MAGUFULI ndiyo YESU amezungumzia, nakwambieni maisha yanarudi kama zamani, piga keleleeeeeee
NENDA KAWAAMBIE MABWANA WALIOANZISHA DINI HUKO MECCA NA VATICAN...
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 

900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
2,283
2,000
Akiwa katika ujenzi wa daraja la Tanzanite, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi wake kufanya fujo za hali ya juu ikiwepo kupiga kelele kwa nguvu zote na watu kwenda beach kama ishara ya kumpongeza Rais kwa kuishinda COVID 19.

Pia Makonda amewataka watu wote waliokimbià Corona Dar warudi haraka kwani kifo hakikimbiwi.

Chanzo: Global TV Online.
Pia Makonda amewataka watu wote waliokimbià Corona Dar warudi haraka kwani kifo hakikimbiwi, Bashite katuma message kwa Jiwe.
 
Top Bottom