Paul Makonda: Utawala wa awamu ya nne ulikuwa na matabaka kati ya viongozi na wananchi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa, Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ni bora kuliko Serikali ya awamu ya nne, anaandika Faki Sosi.

Makonda ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amesema Serikali iliyopita ilikuwa na matabaka kati ya viongozi na wananchi tofauti na ilivyo sasa.

Makonda alikuwa akizungumza katika kipindi cha Terminal cha Clouds Fm alasiri.

"Serikali ya sasa inafanya kazi nzuri zaidi. Kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi kwa sababu, kiongozi ana sifa ya kuwasikiliza anaowaongoza lakini mtawala hana sifa hiyo "alisema makonda.

Amejinasibu kuwa mkoa wake wa Dar es salaam umekuwa mkoa wa kipekee, kwani viongozi wanashirikiana na wananchi moja kwa moja.

Chanzo:
Mpekuzi
 
Hivi kiukweli ni kiongozi gani anaesikiliza watu wake? Jk alikuwa akikubali kazungumza na wapinzani Meza moja, wakati mwingine alikuwa akiwaita Ikulu
 
Na kweli ilikuwa ya matabaka, ya hovyo na ndio sababu watu kama yeye wakawa sehemu ya serikali hiyo.
 
Makonda anadharau sana utafikiri JK hakufanya lolote ni moja ya vijana wala shisha tuu japo yeye anakataza...magufuli wake hashauriki kabisa kaxi kujipendekeza tuuu
 
Kazi za kulaumu tu hazisaidiii...tabaka lakini kivitendo yanaonekana walichofanya..sasa tunasubiri yenu...bado hamjafanya maendeleo tukaweza kulinganisha.
JK bado amefanya mengi sana mna kazi kuyafunika....hapa nazungumzia maendeo...katika kisecta...usije uka comment mambo ya wafanya kazi hewa...ntakuuliza wizara ya ujenzi walikuwapo wangapi awamu ya nne
 
Naona kama awamu hii... mazungumzo meeeeeeengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Sijui lakini kila mtu ana plan zake ila kwa mimi ninayeijua kidogo China ilipotoka na yale ma-cultural revolution na GREAT LEAP FORWARD na nini sijui.

Ukisoma kidogo histoy kwenye AGRICULTURAL REVOLUTION NA INDUSTRIAL REVOLUTION na ukitaka kupata uhalisia wa tunachokihitaji na muda tunaotumia kupiga porojo........aisee bado saana.

Tufanye kazi, tuache wananchi ndio waone hiyo gap kama imeondoka au vipi.
 
Makonda anadharau sana utafikiri JK hakufanya lolote ni moja ya vijana wala shisha tuu japo yeye anakataza...magufuli wake hashauriki kabisa kaxi kujipendekeza tuuu

Anasahau kuwa awamu anayoitumikia imeibukia mikononi kwa huyo anayemponda, ni kama yule dogo anayeshughulikia mambo ya mazingira
 
aache unafiki wake. alipokuwa uv-ccm mbona hakuyaongea haya.amepewa ujiko sasa anajisahau. ati kiongozi anaewasikiliza watu anaowaongoza, sijui anamzungumzia nani!
 
JK alijenga barabara nyingi sana za kuunganisha mikoa, tunaona matunda yake kwa mabasi ya mwendo kasi, Train za Pugu, Ubungo na kadhalika, Kivuko kikubwa sana Kigamboni , Daraja la Kigamboni na mambo mengi huko mikoani , tunamshukuru na kumuombea Mungu, sasa ni wakati wa Uongozi huu nao kujitahidi iache Legacy yake ambayo sisi tutakaa tuienzi miaka na miaka!
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa, Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ni bora kuliko Serikali ya awamu ya nne, anaandika Faki Sosi.

Makonda ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amesema Serikali iliyopita ilikuwa na matabaka kati ya viongozi na wananchi tofauti na ilivyo sasa.

Makonda alikuwa akizungumza katika kipindi cha Terminal cha Clouds Fm alasiri.

"Serikali ya sasa inafanya kazi nzuri zaidi. Kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi kwa sababu, kiongozi ana sifa ya kuwasikiliza anaowaongoza lakini mtawala hana sifa hiyo "alisema makonda.

Amejinasibu kuwa mkoa wake wa Dar es salaam umekuwa mkoa wa kipekee, kwani viongozi wanashirikiana na wananchi moja kwa moja.

Chanzo:
Mpekuzi
Huyo tusha mchoka na hiyo yoote ni kupalilia ugali wake, bila serikali ya awamu ya 4 nani angemtambua huyo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom