Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa, Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ni bora kuliko Serikali ya awamu ya nne, anaandika Faki Sosi.
Makonda ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amesema Serikali iliyopita ilikuwa na matabaka kati ya viongozi na wananchi tofauti na ilivyo sasa.
Makonda alikuwa akizungumza katika kipindi cha Terminal cha Clouds Fm alasiri.
"Serikali ya sasa inafanya kazi nzuri zaidi. Kuna tofauti kubwa kati ya watawala na viongozi kwa sababu, kiongozi ana sifa ya kuwasikiliza anaowaongoza lakini mtawala hana sifa hiyo "alisema makonda.
Amejinasibu kuwa mkoa wake wa Dar es salaam umekuwa mkoa wa kipekee, kwani viongozi wanashirikiana na wananchi moja kwa moja.
Chanzo: Mpekuzi