Elections 2015 Paul Makonda unapata wapi ujasiri wa kukataza wananchi kusubiria matokeo ya kura?

Jana akiwa kanisani mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kujiamini sana kupita kiasi alitoa kauli ya vitisho kwa wananchi kuwa hataruhusu wananchi kwenye wilaya yake ya Kinondoni kubaki vituoni baada ya kupiga kura hata kama ni mita mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Suala hili lipo mahakamani na bado halijatolewa ufafanuzi wa mahakama kuu. Sasa wakati tunasubiri maamuzi ya mahakama kuu inashangaza sana kuona mkuu wa wilaya anatoa kauli ya vitisho kama hiyo, hivi kwa mfano mahakama kuu ikiamua kuwa wananchi wana haki ya kusubiria matokeo atarudi tena makanisani kuwatangazia wananchi kuwa wana haki ya kubaki vituoni?, na jumapili iliyobaki ndiyo hiyo ya uchaguzi.

Wameshiba wamevembewa wamejisahau#tuwatoe October 25
 
yeye ndio kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya au ulitaka atangaze baba yako
Hata kama ni mjinga usipende ujinga wako uonekane wazi....Kwani kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama hapaswi kafuata sheria?Sheria inasema mita 200....huo ukuu wake wa kamati na ulinzi hauko juu ya sheria!PERIOD!
Mishipa imewatoka!kisa kuiba kura...mtailipua hii nchi ninyi!
 
Makonda ndo nani kwanza??? Hiyo Jeuri katoa wapi? Mwambie sie tutalinda kura zetu na yeye na magari yake ya polis tuone nn kitatokea.... tusitishane banah.... sheria inaniruhusu kusimama mita 200 kutoka kituo cha kupga kura
 
Makonda,Nape na Mwigulu ni watu wa kupuuzwa.Ni mavuvuzela au makarai ya zege ya CCM.
Jana akiwa kanisani mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kujiamini sana kupita kiasi alitoa kauli ya vitisho kwa wananchi kuwa hataruhusu wananchi kwenye wilaya yake ya Kinondoni kubaki vituoni baada ya kupiga kura hata kama ni mita mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Suala hili lipo mahakamani na bado halijatolewa ufafanuzi wa mahakama kuu. Sasa wakati tunasubiri maamuzi ya mahakama kuu inashangaza sana kuona mkuu wa wilaya anatoa kauli ya vitisho kama hiyo, hivi kwa mfano mahakama kuu ikiamua kuwa wananchi wana haki ya kusubiria matokeo atarudi tena makanisani kuwatangazia wananchi kuwa wana haki ya kubaki vituoni?, na jumapili iliyobaki ndiyo hiyo ya uchaguzi.
 
Jana akiwa kanisani mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kujiamini sana kupita kiasi alitoa kauli ya vitisho kwa wananchi kuwa hataruhusu wananchi kwenye wilaya yake ya Kinondoni kubaki vituoni baada ya kupiga kura hata kama ni mita mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Suala hili lipo mahakamani na bado halijatolewa ufafanuzi wa mahakama kuu. Sasa wakati tunasubiri maamuzi ya mahakama kuu inashangaza sana kuona mkuu wa wilaya anatoa kauli ya vitisho kama hiyo, hivi kwa mfano mahakama kuu ikiamua kuwa wananchi wana haki ya kusubiria matokeo atarudi tena makanisani kuwatangazia wananchi kuwa wana haki ya kubaki vituoni?, na jumapili iliyobaki ndiyo hiyo ya uchaguzi.

Wajua kuna watu vilaza nchi ndo kama makonda. Njaa ina msumbua, na hawa viongozi waliopo ccm. Uwezo wakufikiri kwa kunamaisha baada ya uchaguzi hawana. Kwamba ccm kung'atuka litakua jambo la kawida kwenye nchi ya mfumo wa vyama vingi.
Huu wote ni ulevi wamadaraka. Na wengi hapo ndo hujisahau kwamba, uongozi ni dhami. Wengi ccm kama akina makonda, wanadhani uongozi wa kisiasa ni ajira ya kudumu. Dah! Tanzania ina safari ndefu ya ukombozi.
 
Jana akiwa kanisani mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kujiamini sana kupita kiasi alitoa kauli ya vitisho kwa wananchi kuwa hataruhusu wananchi kwenye wilaya yake ya Kinondoni kubaki vituoni baada ya kupiga kura hata kama ni mita mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Suala hili lipo mahakamani na bado halijatolewa ufafanuzi wa mahakama kuu. Sasa wakati tunasubiri maamuzi ya mahakama kuu inashangaza sana kuona mkuu wa wilaya anatoa kauli ya vitisho kama hiyo, hivi kwa mfano mahakama kuu ikiamua kuwa wananchi wana haki ya kusubiria matokeo atarudi tena makanisani kuwatangazia wananchi kuwa wana haki ya kubaki vituoni?, na jumapili iliyobaki ndiyo hiyo ya uchaguzi.

Halafu anajipa mamla ya uRAIS jana nilikuwa kwenye TAMASHA flan la jamaa walioacha kutumia Dawa za kulevya sasa kuna wmbo flan tuliimba unahusu HAKI yaani hakuna AMANI bila HAKI kila mtu atimize wajibu wake duh....alipopewa nafasi yakuongea alimwaga Povu za hatari....nilicheka sana
 
Kila jambo lina mipaka yake. Hilo ni zaidi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Hilo linatolewa tamko kitaifa na sio na wilaya moja moja. Ni sawa na mkuu wa Wilaya ya Mbinga kutangaza vita na Malawi kwa vile wilaya yake iko mpakani.
Makonda anatakiwa asubiri kutekeleza maagizo yatakayo tolewa kitaifa kuhusu jambo hilo na sio yeye kusema hatakubali. Kwenye hili Wasimamizi wa uchaguzi, Polisi na waangalizi wa uchaguzi hawapokei maelekezo kutoka kwa ma DC bali tume ya uchaguzi Taifa hivyo hata yeye atulie tuu.
Huku ni kutojua mipaka ya kazi wanazopewa hawa Makada, yeye anasubiri jambo asemalo litangazwe sana Clouds FM akidhani ni sifa.

Viongozi wa CCM wameshakariri kuwa kila mtu anaweza toa tamko na asichukuliwe hatua yeyote.
 
Anayo mamlaka,hivi mtoa post unatambua mamlaka ya mkuu wa wilaya au unaota ndoto za mchana,yeye ni mwaki
ishi wa rais katika wilaya yake na ndio mtunza amani na vyombo vya ulinzi na usalama viko chini yake kwa mamlaka aliyopewa
 
Nani asiejua hiii...au kwaakili yako kwakuwa ni mwakilishi wa Rais anakuwa juu ya Sheria!!
 
Back
Top Bottom