SUPER PREDATOR
JF-Expert Member
- Apr 29, 2014
- 2,093
- 725
Jana akiwa kanisani mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kujiamini sana kupita kiasi alitoa kauli ya vitisho kwa wananchi kuwa hataruhusu wananchi kwenye wilaya yake ya Kinondoni kubaki vituoni baada ya kupiga kura hata kama ni mita mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.
Suala hili lipo mahakamani na bado halijatolewa ufafanuzi wa mahakama kuu. Sasa wakati tunasubiri maamuzi ya mahakama kuu inashangaza sana kuona mkuu wa wilaya anatoa kauli ya vitisho kama hiyo, hivi kwa mfano mahakama kuu ikiamua kuwa wananchi wana haki ya kusubiria matokeo atarudi tena makanisani kuwatangazia wananchi kuwa wana haki ya kubaki vituoni?, na jumapili iliyobaki ndiyo hiyo ya uchaguzi.