Elections 2015 Paul Makonda unapata wapi ujasiri wa kukataza wananchi kusubiria matokeo ya kura?

Awa akina makonda na Jk watatuletea uvunjifu wa amani.
Sheria inatamka pasipo na kificho mita 200.
Iwe ni kulinda kura au kusubiri matokeo sheria inasema mita 200.
Kama walitaka kuzifuta hizi mita 200 basi wangepeleka mswada wa dharula kwenye bunge la makinda.
 
Jana akiwa kanisani mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kujiamini sana kupita kiasi alitoa kauli ya vitisho kwa wananchi kuwa hataruhusu wananchi kwenye wilaya yake ya Kinondoni kubaki vituoni baada ya kupiga kura hata kama ni mita mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Suala hili lipo mahakamani na bado halijatolewa ufafanuzi wa mahakama kuu. Sasa wakati tunasubiri maamuzi ya mahakama kuu inashangaza sana kuona mkuu wa wilaya anatoa kauli ya vitisho kama hiyo, hivi kwa mfano mahakama kuu ikiamua kuwa wananchi wana haki ya kusubiria matokeo atarudi tena makanisani kuwatangazia wananchi kuwa wana haki ya kubaki vituoni?, na jumapili iliyobaki ndiyo hiyo ya uchaguzi.

yeye ndio kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya au ulitaka atangaze baba yako
 
yeye ndio kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya au ulitaka atangaze baba yako

Sawa nafahamu lakini anatakiwa kufuata sheria za nchi na kuheshimu muhimili wa mahakama, ila sijapendezwa na jinsi swali lako ulivyoliuliza maana lina dhihaka ya namna fulani
 
yeye ndio kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya au ulitaka atangaze baba yako

Kila jambo lina mipaka yake. Hilo ni zaidi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Hilo linatolewa tamko kitaifa na sio na wilaya moja moja. Ni sawa na mkuu wa Wilaya ya Mbinga kutangaza vita na Malawi kwa vile wilaya yake iko mpakani.
Makonda anatakiwa asubiri kutekeleza maagizo yatakayo tolewa kitaifa kuhusu jambo hilo na sio yeye kusema hatakubali. Kwenye hili Wasimamizi wa uchaguzi, Polisi na waangalizi wa uchaguzi hawapokei maelekezo kutoka kwa ma DC bali tume ya uchaguzi Taifa hivyo hata yeye atulie tuu.
Huku ni kutojua mipaka ya kazi wanazopewa hawa Makada, yeye anasubiri jambo asemalo litangazwe sana Clouds FM akidhani ni sifa.
 
Jana akiwa kanisani mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa kujiamini sana kupita kiasi alitoa kauli ya vitisho kwa wananchi kuwa hataruhusu wananchi kwenye wilaya yake ya Kinondoni kubaki vituoni baada ya kupiga kura hata kama ni mita mia mbili kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.

Suala hili lipo mahakamani na bado halijatolewa ufafanuzi wa mahakama kuu. Sasa wakati tunasubiri maamuzi ya mahakama kuu inashangaza sana kuona mkuu wa wilaya anatoa kauli ya vitisho kama hiyo, hivi kwa mfano mahakama kuu ikiamua kuwa wananchi wana haki ya kusubiria matokeo atarudi tena makanisani kuwatangazia wananchi kuwa wana haki ya kubaki vituoni?, na jumapili iliyobaki ndiyo hiyo ya uchaguzi.

Huna hata haja ya kutafari kauli za kipuuzi ambazo hazijapimwa mkuu,hiv unadhani polisi au hasa ffu ni wengi kiasi gani kuweza kuthibiti asilimia kubwa ya wapiga kura walioamua kusubiri matokeo vituoni kwa siku moja au kwa wakati mmoja,okay fine hata wakiamua kutumia na wanajeshi bado hawataweza ni jambo linalotokea kwa wakati mmoja
 
Kauli yake inaweza kuvunja amani ikiachwa hivihivi bila kutolewa ufafanuzi.
 
Kwa akili yako fupi unadhani ccm itaiba kura za nani kama sio za UKAWA? Za TLP? au DOVUTWA? wakishaiba hizo zitafika ngapi kwa ujumla wake? hahaha
VIVA UKAWA!!!!
Wewe lofa tu! Unafikiri UKAWA mna wanachama zaidi ya milioni5? Wasio na vyama tuliojiandikisha tupo wengi zaidi ya milioni 10!
 
Me nijuavyo haka ni kapuuzi fulani tu,na iwe lowassa ama magufuli hawatakataka kabisa kuwa sehemu ya serikali,hana adabu
 
Back
Top Bottom