Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,967
- 11,212
Katika viongozi vijana ninao anza kuwakubali huyu jamaa anastahili tuzo ya kiongozi bora kwa vijana katika muda mfupi aliowekwa kwenye public office.
Siku zote niliamini asilimia kubwa ya shida nyingi za watanzania ni zao la wafanyakazi wa serikari na si vyama vya siasa. Tumetengeneza sheria nyingi na nzuri tu kupitia copy and paste ya sheria za wengine mfano 'Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Mwaka 2004'. Hii sheria inataka mahusiano mazuri kazini kwa njia ya mikataba, mazingira bora ya kazi na kuweza kubalance power za mtoa ajira na muajiriwa kupitia vikundi vyao.
Mantiki ya sheria yoyote ni kuleta mabadiliko yanayo tarajiwa na kunakuwa na regulator wake kuhakikisha sheria inafuatwa kama ilivyotarajiwa vinginevyo kuna adhabu za fine ya serikari au kulipa fidia kwa mfanyakazi kwa ukiukwaji wa sheria. Chini ya 'Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Mwaka 2004' msimamizi wake ni idara ya kazi na malengo yake ya usimamizi wameyabainisha wazi kwenye website yao.
Sasa leo inakuwaje atoke mkuu wa wilaya kwenda kusikiliza vilio vya wafanyakazi vinavyo ambatana na ukiukwaji wa sheria. Inawezekana vipi mtu anafanyakazi kwa miaka nane kama kibarua bila ya mkataba, holiday pay, pengine na pension plan kutoka kazini? na idara ya kazi hipo na sheria wanaijua inasemaje kuhusu ukiukwaji huo. Sidhani kama Makonda ana mamlaka ya kutoa maagizo lakini the goodwill gesture is unquestionable.
Kuna wanaobisha lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanaopewa kuziongoza hizi taasisi za serikari awana uwezo ndio zao la hivi vitu vyenye malalamiko ndani ya jamii na si kitu kingine.
Last edited by a moderator: