Paul Makonda, Mrisho Gambo waisindikiza Ndege Zimbabwe mpaka Zambia

Safi kwa hatua hii, lakin mambo yetu mengi mbona yanafanyika kiswahili sana, kwani lazima zisindikizwe? Nani kawachagua kusindikiza?

Au labda nao walikuwa na route huko
 
Yani hili Shirika halipo kibiashara kabisa...

Badala ya kuja na mikakati ya kibiashara kila kitu mnafanya siasa..

Hiyo route nimewahi kuitumia ilikuwa ya Fast Jet (Dar-Lusaka-Harare) na Fast Jet ilishaanza kwenda tupu sijui kama mambo yalikuja kubadilika badae..

Nakumbuka one time From Lusaka tulipanda abiria kama 20 hivi na pale Harare walishuka wachache sana na walio board in hawakuzidi abiria wa 5..ndege yote ilikuwa karibia tupu..

Ni route iliyokuwa inachechemea sana kwa wakati ule wa Fast Jet..

ATCL tuelezeni mmefanya mkakati gani wa hiyo route na sio kutuonyesha picha za ma RC.
 
Leo ndio siku rasmi ndege yetu imezindua safari ya Tanzania-Zimbabwe-Zambia.

Ajabu wakuu wa mikoa Paul Makonda na Mrisho Gambo wameonekana wakisindikiza ndege hiyo, yaani gharama za kutoka Tanzania, Zimbabwe to Zambia kwenda na kurudi eti sababu kubwa ni kushuhudia ndege hiyo ikifanya safari ya Kwanza.

Hongereni wakuu wetu wa mikoa kwa uzalendo uliotukuka.
Picha wakiwa uwanja wa Keneth Kaunda Zambia.View attachment 1029194

sijaelewa ndege hiyo imepata abiria wawili ambao ni wakuu wa mikoa
 
Jana nilisikia maagizo ya jiwe kuwa pia ndege iambatane na mawaziri wawili, sasa sijajua ni hawa ndio mawaziri wenyewe
Waangalie hapo
Subpost%203%20-%20Mapokezi%20ya%20safari%20ya%20kwanza%20ya%20ndege%20ya%20Air%20Tanzania%20A...jpeg
 
Ile kauli ya serikali ya kishamba naona iko wazi sasa.
Sasa ushamba upo wapi hapo? KQ ya Kenya ilipoanza safari za Newyork, uhuru alipanga kuambatana na ndege mpaka Newyork ila alibadili mpango time za mwisho japo aliwakilishwa na viongozi waandamizi wa serikali ya Kenya, vivyo hivyo kwa Ethiopia Ilipoanza rasmi kwenda Djibouti, kiongozi wa juu kabisa aliambatana na ndege mpaka Djibouti

Hili ni jambo la kawaida ila washambawashamba kama nyie lazima mlete ujuaji na mara nyingi mnahaibika kama mlivyoleta ushamba wenu juzi ndege iliposukumwa kwa mkono.
 
Leo ndio siku rasmi ndege yetu imezindua safari ya Tanzania-Zimbabwe-Zambia.

Ajabu wakuu wa mikoa Paul Makonda na Mrisho Gambo wameonekana wakisindikiza ndege hiyo, yaani gharama za kutoka Tanzania, Zimbabwe to Zambia kwenda na kurudi eti sababu kubwa ni kushuhudia ndege hiyo ikifanya safari ya Kwanza.

Hongereni wakuu wetu wa mikoa kwa uzalendo uliotukuka.
Picha wakiwa uwanja wa Keneth Kaunda Zambia.

NI jambo la kawaida. Kenya Airways walipofanya safari ya kwanza ya New York raisi Uhuru Kenyatta aliisindikiza.
 
Back
Top Bottom