MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Binafsi sina Shaka na utendaji wa huyu bwana kwa nafasi ya ukuu wa Wilaya maana wapo wakuu wa wilaya wachanga zaidi yake!
Lakini ni kwanini mtu anaanza kazi mara ya kwanza kwa nafasi kubwa kama ile ndani ya wilaya kubwa ndani ya jiji lenye Changamoto lukuki zinazohitaji uzoefu wa hali ya juu kama Kinondoni?, wapo wakuu wa wilaya alioanza nao kazi pamoja ambao walipewa halmashauri ndogo zenye changamoto za kawaida ili kuwajengea uzoefu wa kulitumikia taifa zaidi. Makonda angepewa wilaya ndogo ya kawaida kama wilaya ya Babati,Kilindi,Tandahimba au zingine ambazo angeweza kumudu vyema majukumu yake kama walivyo wengine, kulalamika Makonda ni kumuonea tu! Zilaumiwe zaidi mamlaka za uteuzi wa nafasi yake.
Ama kwa hakika utakubaliana na Mimi kua nafasi ya Makonda katika Manispaa ya Kinondoni ilizungukwa na utashi wa maamuzi yaliyotanguliza zaidi siasa mbele kuliko utaifa! Sio kweli kwamba baadhi ya madudu yanayoibuliwa ndani ya Manispaa hiyo yalitokea wakati yeye hajateuliwa kwa nafasi hiyo! Lakini mbona alikua kimya wakati haya yakifanyika ndani ya uongozi wake? Sidhani kama madudu haya yakifanyika halafu yeye akayaona na kukaa kimya! Kufanya hivyo ni kumuonea maana inawezekana alikua akizungukwa na wakongwe wa madili bila hata ya yeye kujua kutokana na uchanga wake katika uongozi.
Kuongoza taasisi ndani ya Chama ni tofauti na kuongoza umma wenye mchanganyiko wa watu vyama mbali mbali,tabia tofauti na kadhalika! Nina uhakika kua makonda alivyokua anapinga ufisadi ndani ya CCM kama kiongozi wa chipukizi na hamasa ni tofauti na kupinga ufisadi ndani ya Manispaa ya Kinondoni ambako kuna idara na taasisi lukuki! Hili halikupimwa kabla ya uteuzi wa nafasi yake.
Ushauri wangu si vyema kuona Makonda akipumzishwa kwa nafasi yake maana hakuna mahali panaonesha kua alihusika na kashfa yeyote ya ufisadi zaidi ya watumishi wengine walio ndani ya Manispaa hiyo, Zaidi itumike busara ya kumhamishia halmashauri nyingine ndogo aendelee kukomaa kiuongozi zaidi, Nchi hii wapo watu makini na wenye uzoefu wa kutosha kiongozi kuongoza Manispaa ya Kinondoni.