bg_dg_dy
JF-Expert Member
- Feb 27, 2009
- 604
- 489
Mheshima Paul Makonda kijana maarufu na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anahojiwa na TBC kuhusu miaka kumi na minane bila uwepo wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwasisi wa taifa Letu na Baba wa Taifa.
Mwalimu hatuko nae kimwili ila kifikra tupo nae tunaishi misingi yake.
Mwalimu alianzisha vyama vingi vya kisiasa kwa nia njema ila vyama vya kisiasa vimekuwa vikiwana lengo la kujinufaisha.
Aelezea mfano serikali ya awamu ya tano inavyoishi misingi ya mwalimu nyerere, mfano suala la makinikia wasomi wetu kutokuwa wazalendo, Mwalimu awali alituasa tusubirie pale ambapo tutakuwa tupo tayari na kweli tumepata wasomi ila uzalendo umeshindikana.
Agusia swala la mfumo wa uwajibikaji kwa wafanyakazi ulivyowaathiri toka wakiwa vyuoni hadi kutokuishi uzalendo katika sekta ya umma. Mfano anapata fedha kutoka vyanzo tofauti kuanzia bodi ya mkopo na ndugu/jamaa kinachopelekea wanafunzi kupata fedha nyingi na maisha ya utajiri akiwa chuoni tofauti na kipato atakachopata akiwa kazini, hvyo ni chanzo hakika cha mfumo wa rushwa makazini kwa kutengeneza ugumu katika utoaji wa huduma ili kupata pesa zaidi.
Ashauri yafuatayo ili watanzania tuweze kuuishi uzalendo.
1. Takukuru iwezeshwe ifanye kazi yake vizuri.
2. Viongozi wa dini watusaidie kutukumbusha baada ya maisha ya hapa kuna maisha mwingine.
3. Mabadiliko kwenye sekta ya Elimu kuwezesha uzalendo zaidi kwa wanafunzi wetu.
Mfano tuwaangalie Nyerere, Kawawa na Warioba Hindi walivyo waadilifu hadi leo tujifunze kutoka kwao.
Pia somo la uzalendo hautoshi, bali viongozi na waalimu wauishi uzalendo wanaoutangaza na kusisitiza.
Mwisho, mwalimu nyerere alijiamini na aliamini katika umoja. Hvyo watanzania ninawasihi tuungane tushikamane tuweze kulifikisha taifa pale alipopataka mwalimu nyerere. Mungu atubariki na tumshirikishe Mungu katika yote.