Paul Makonda apokea saruji mifuko 1640 kutoka kwa wadau wa maendeleo

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
DC KINONDONI, PAUL MAKONDA APOKEA SARUJI MIFUKO 1640 KUTOKA KWA WADAU WA MAENDELEO KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARY

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.

Lori lilibeba saruji hiyo likiwa eneo la tukio.

DC Makonda na wageni wake wakiwa eneo la tukio kabla ya makabidhiano ya saruji hiyo.

Mhe. Bulembo akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo.

Wanahabari wakizungumza na watoa msaada huo.
 
natumaini ameisha chakachua hadi kutangazwa hiyo jamaa kaishapiga kama nusu yake.

swissme
 
Naona baada ya Kubenea kumtuliza na hivyo kumpeleka mafichoni...naona d.c ameamua kurudi kwa kasi tena
 
Kwa nini hawatoi misaada kimya kimya? Binafsi huwa siamini watoa misaada ambao wanapenda kijitangaza, tenda wema uende zako usingoje shukurani. Hata mahandiko ya Mungu usema mkono wa kulia ukitoa msaada/hela hukana sababu ya mkono wa kushoto kijua kilicho jiri.
 
Huyo ndio Makonda mchapa kazi tunayemtaka sio wale wanao enda bungeni kazi kuongelea na kushangilia chupi na shanga zilizovuliwa zinapoongelewa badala ya kuchapa kazi majimboni mwao na kuleta maendeleo kama haya ya Makonda
Mkuu sio kosa lako,ni upofu ulionao
 
Hii nayo ni habari ya kuleta JF,tena Jukwaa la Siasa

Ptuuuuuuuuuuuuuuuu
Ulitaka ipelekwe wapi mkuu!? Kama Bwana Lowasa akisimama kusalimiana na wakulima Dumila inaletwa hapa JF tena jukwaa hili hili la Siasa......Hili suala la Maendeleo ili kujenga shule ambazo watasoma watoto wetu bila kujali Itikadi ya Chama chochote cha siasa. Tuwe na busara kidogo kwenye mambo ya msingi.
 
Kwa nini hawatoi misaada kimya kimya?

Misaada mingi hupotea ISIPOWEKWA WAZI.Hata michango ya harusi inatakiwa ijulikane wazi wazi nani katoa nini vinginevyo kamati ya pesa inaziiba zingine .
Huo unaitwa uwazi.Ulichopokea kwa ajili ya jumuiya unakianika wazi.Au ulitaka ile staili ya Lowasa ya kusema marafiki zangu wananichangia.Halafu hasemi kapewa nini shilingi ngapi? Wewe unaona mtu tu anasafiri na madege tu.

Wengi waliochangia kampeni watakuwa waliliwa pesa zao kwa kisingizio hicho cha siri
 
Ulitaka ipelekwe wapi mkuu!? Kama Bwana Lowasa akisimama kusalimiana na wakulima Dumila inaletwa hapa JF tena jukwaa hili hili la Siasa......Hili suala la Maendeleo ili kujenga shule ambazo watasoma watoto wetu bila kujali Itikadi ya Chama chochote cha siasa. Tuwe na busara kidogo kwenye mambo ya msingi.
Lowasa anakujaje hapa Mkuu
 
Kwa nini hawatoi misaada kimya kimya? Binafsi huwa siamini watoa misaada ambao wanapenda kijitangaza, tenda wema uende zako usingoje shukurani. Hata mahandiko ya Mungu usema mkono wa kulia ukitoa msaada/hela hukana sababu ya mkono wa kushoto kijua kilicho jiri.
huo ushauri wako,hakuna kichwa cha ccm kinacho weza kuufata!ccm bila publicity haiwezekani
 
Lowasa anakujaje hapa Mkuu

Alikuwa anapokea mapesa mengi halafu anagawa kama misaada mbele ya waandishi wa habari kama michango toka kwa rafiki zake!! Ila hao rafiki zake alikuwa hawaweki wazi kama Makonda alivyofanya.Alikuwa hayuko wazi.
Kwenye michango mtu anakiwa kuwa wazi.Wengi walimchangia ikafanywa siri lakini kutakuwa na waliolizwa kwenye huo usiri
 
Kwa nini hawatoi misaada kimya kimya?

Baadhi ya wajanja CHADEMA wangependa iwe siri.Aliyetoa asijulikane hadharani na kilichotolewa kisijulikane hadharani.Wangechukua mifuko 30 tu kwenda kupaka simenti mahali halafu yote inayobaki wangepeleka kwenye duka la hardware yake kuiuza!

SABODO alitoa mamilioni ya pesa kujenga chuo CHA chadema kimya kimya mpaka leo hakipo.Ila kuna siku likafyatuka hadharani ndio ikajulikana.Kuna hela zilitolewa kwa ajili ya kuchimba visima ziko wapi au visima viko wapi wekeni picha!!!! Mambo ya siri kwenye kutoa ni hatari
 
Hii nayo ni habari ya kuleta JF,tena Jukwaa la Siasa

Ptuuuuuuuuuuuuuuuu
KUBENEA AKACHUKUE YAKE ; KAZI YA MBUNGE ANAFANYA MKUU WA WILAYA
KUBEBEA KATELEKEZA WAPIGA KURA
 
Huyo ndio Makonda mchapa kazi tunayemtaka sio wale wanao enda bungeni kazi kuongelea na kushangilia chupi na shanga zilizovuliwa zinapoongelewa badala ya kuchapa kazi majimboni mwao na kuleta maendeleo kama haya ya Makonda
JMP no 2 makaonda
 
Back
Top Bottom