Paul Makonda amempa makavu meya wa Ubungo Boniface Jacob kwa utovu wa nidhamu

Libya

JF-Expert Member
Nov 11, 2016
783
1,918
Aysee Mimi ningekua meya Jacob tungezichapa! Makonda amemdhalilisha sana meya wa ubungo kumwambia maneno kama haya mbele ya wananchi wake!

Makonda amekosa busara kwanini lakini huyu MTU! Hivi wachawi wa nchi hii mnafanya kazi gani.

=======

Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob leo ameumbuliwa hadharani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya meya huyo kukosa nidhamu kwa kudanganya wananchi kuwa yeye ndio amefanikisha mradi wa ujenzi wa Kisima ca Maji Kata ya Mbezi Makabe wakati Rais Dkt.John Magufuli ndio alietoa fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 611 kwaajili ya kumaliza kero za maji kwa wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati wa mwendelezo wa ziara ya ukaguzi miradi ya Maendeleo Mkoa wa Dar es salaam ambapo RC Makonda ameshangazwa kuona Meya anajinadi mbele ya wananchi na viongozi kuwa yeye ndie aliefanikisha upatikanaji wa fedha hizo na ndio alieweka saini badala ya kumshukuru Rais Dkt. John Magufuli alietoa fedha hizo.

RC Makonda amesema kitendo hicho ni utovu wa nidhamu kwa viongozi wanaotoa fedha kwaajili ya kutatua kero za wananchi ambapo amemtaka Meya huyo kuwa na shukrani kwa viongozi bila kujali itikadi za kisiasa.

Mradi wa ujenzi wa kisima cha Maji Mbezi Makabe unagharimu zaidi ya Shilingi Million 611 zilizotolewa na Rais Magufuli na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya Wakazi 75,000.

Kama fedha imekuja tuachane na hayo mengine, Sisi wananchi tunashukuru kwa kuja kwa pesa tunaomba Meya ahakikishe inafanya kazi iliyokusudia. Tunashukuru pia na kwaniaba ya Meya kama hakuona umuhimu kushukuru kwa walioleta pesa.
Sasa tuchape kazi.
 
..Serekali imepora mapato ya halmashauri halafu inalaghai wakaazi wa halmashauri hizo kuwa inawaletea fedha miradi ya maendeleo.

..Meya Jacob yuko sahihi kutokushukuru Raisi Magufuli binafsi.

..Fedha za mradi hazikutoka mfukoni mwa Raisi Magufuli. Fedha hizo zimetoka serekali kuu na serekali kuu ilipata fedha hizo toka kwa halmashauri.
 
Aysee Mimi ningekua meya Jacob tungezichapa! Makonda amemdhalilisha sana meya wa ubungo kumwambia maneno kama haya mbele ya wananchi wake!

Makonda amekosa busara kwanini lakini huyu MTU! Hivi wachawi wa nchi hii mnafanya kazi gani.

=======

Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob leo ameumbuliwa hadharani na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya meya huyo kukosa nidhamu kwa kudanganya wananchi kuwa yeye ndio amefanikisha mradi wa ujenzi wa Kisima ca Maji Kata ya Mbezi Makabe wakati Rais Dkt.John Magufuli ndio alietoa fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 611 kwaajili ya kumaliza kero za maji kwa wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati wa mwendelezo wa ziara ya ukaguzi miradi ya Maendeleo Mkoa wa Dar es salaam ambapo RC Makonda ameshangazwa kuona Meya anajinadi mbele ya wananchi na viongozi kuwa yeye ndie aliefanikisha upatikanaji wa fedha hizo na ndio alieweka saini badala ya kumshukuru Rais Dkt. John Magufuli alietoa fedha hizo.

RC Makonda amesema kitendo hicho ni utovu wa nidhamu kwa viongozi wanaotoa fedha kwaajili ya kutatua kero za wananchi ambapo amemtaka Meya huyo kuwa na shukrani kwa viongozi bila kujali itikadi za kisiasa.

Mradi wa ujenzi wa kisima cha Maji Mbezi Makabe unagharimu zaidi ya Shilingi Million 611 zilizotolewa na Rais Magufuli na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya Wakazi 75,000.

Mwili wa Mzee Mengi ulivyowasili kupitia njia ya Mizigo maarufu Cargo...
Aliondoka kama abiria upande wa VIP amerudi kama parcel...
Dunia tunayoishi si chochote si lolote tuache majivuno, tuache dharau, tuache roho mbaya..
Dunia si sehemu yetu ya Kudumu...
Vyeo tulivyonavyo ni bure tuu
Mafanikio tuliyonayo ni buree
Kila hatua tunayopitia tutambue uwepo wa mungu.

Utukufu upo mbinguni. Hizi tabu mnazotutafutia. Zina mwisho wake. Amina
 
Hivi kumbe huyu Makonda Ni zero kweli mi nilidhani wanamwonea leo nimeamini. Serikali na huyo Raisi wake bila Kodi za wavuja jasho ikiwemo hao waliomchagua meya inabiashara gani ambayo sio ya wakipa Kodi ili jujiingizia pesa?Hili ni somo la uraia kidato Cha pili kwamba serikali ni kikundi kinachokwenda kutumia fedha za walipa Kodi ili kuleta maendeleo na wasimamizi wa hizo fedha ni wawakilishi wao kupitia wabunge na madiwani na wenyeviti wa vijiji. Hili jitu jinga sana linachanganya Kati nidhamu na unafiki yani kwakuwa yenyewe yanashibisha matumbo kwa unafiki wa kusifia hovyo Kama Malaya wa Kongo anafikiri kila mtu anaishi kiujanjaujanja. Aende akamuulize huyo Mungu mtu wake hizo pesa alizopeleka aliuza ng'ombe za Bibi yake ili ziende mbezi kusaidia kero za maji? Onyesha vyeti Makonda ujinga wako Ni mkubwa kuliko ukubwa wenyewe
 
Kama hizo fedha zilikuwa kwenye bajeti ni haki ya meya kutamba kwamba amefanikisha maana yeye ndo Mwenyekiti wa chombo kinacho idhinisha hiyo bajeti ngazi ya LGA. Kama hizo hela hazikufuata channel ya bajeti Rais akaombwa nje ya bajeti akazitoa huyo meya asijisifie bure. Lakini kumwambia ni utovu wa nidhamu ni udhalilishaji, yeye Makonda anapotumia maneno 'katika mkoa wangu wa Dar es Salaam' sio utovu wa nidhamu? Kwa mantiki yake mikoa yote ni ya Rais maana ndiye anayewateua kuisimamia hivyo ikiwa anadhani kumtaja Rais kwa kila jambo ndio nidhamu ya mtanzania basi nayeye ajitathmini ktk hiyo nidhamu. Katika nchi zinazofuata mfumo wa 'Local Government Authority' Meya ni kiongozi mzito sana kiutawala kwenye eneo lake kuliko anavyo fikiri.
 
Makonda hajaiva kisiasa siku baba akiondoka atatamani ardhi ipasuke imfunike. Gari anayotembelea linashangaza kwani ni la garama kubwa fedha zake zingejenga visima 200 na kununua madawati 2000 na vifaa vya shule 10 na zaidi
 
kuna kitu ambacho makonda haelewi labda ni kutokana na upro wake mdogo wa kuchanganua mambo/ wizi wa vyeti. raisi magufuli ni kama wazir wa TAMISEMI. Amepora vyanzo vya mapato toka local government. anapoenda kutoa pesa nmahali hatoi kama zakwake anatoa zile alizopoka hanlmashauri ! sijui kama makonda anaelewa haya? huyu jackobo yeye ni msimamizi wa pesa za umma ! kusema kajenga kisima kosa liko wapi? siasa za ushamba na uelewa mdogo
 
Makonda ni mtovu mkubwa wa nidhamu, huwezi kumwambia rais fulani anauza unga baadae unaenda kuwa rafiki na huyo fulani tena nje ya nchi ambako huyo fulani amekimbilia, unamchonganisha rais, makonda ana wivu tu na dharau hana nidhamu kwa viongozi wenzake wa serikali.
 
Huoni hata aibu uzi tangu 24.4 hadi leo umechangiwa na watu 17?
Huu uzi wako ni wa kijinga sana
 
..Serekali imepora mapato ya halmashauri halafu inalaghai wakaazi wa halmashauri hizo kuwa inawaletea fedha miradi ya maendeleo.

..Meya Jacob yuko sahihi kutokushukuru Raisi Magufuli binafsi.

..Fedha za mradi hazikutoka mfukoni mwa Raisi Magufuli. Fedha hizo zimetoka serekali kuu na serekali kuu ilipata fedha hizo toka kwa halmashauri.

Na Halmashauri ndio Wananchi wenyewe ila kwa sababu tuna Malaika Nchi hii baasi watataka apongezwe hata kwa mambo yasio sahihi.

MUHIMU;Pesa hazikutoka Mfukoni kwa Mh Malaika Mkuu.
 
Back
Top Bottom